Mtanzanias
JF-Expert Member
- Jul 30, 2021
- 1,747
- 3,725
Nawashangaa sana mashabiki wasiojitambua wala kujielewa na wasioitambua sayansi ya mpira wa miguu. Simba kapigwa 3 mzuka na Raja nongwa na jumba bovu wanaangushiwa Onyango, Mkude, Manula na Nyoni, ni mpuuzi tu anaweza kuongea utumbo kama huo!
Wachezaji wa Simba ndio hao hao wa siku zote na viwango vyao ndio hivyo hivyo, mlitegemea waende Morocco na maajabu ya Musa?
Kama Raja wamewapiga kwenu goli 3 bila majibu mlitegemea kwenda kuwapiga kwao? Au hapa kati kati mmefanya usajili mwingine kabla hamjarudiana na Raja? Uwezo wa Simba ndio umeishia hapo, siku zote quality ndio inaamua kwenye mechi muhimu na sio blah blah, na kule anakoelekea Simba hakuna tena wakina Horoya wala Vipers, kitakachoamua nani aende nusu fainali ni ubora wa timu yako na sio kurudisha basi kinyume nyume wala kuchoma moto uwanja.
Hizo 3 Simba kapigwa wakati Raja kapumzisha wachezaji wake 5 muhimu wakijiandaa na mechi yao na Waydad hivi karibuni na huwezi kuwasikia wakilalamika kuwa wamewachezesha wachezaji wa akiba.
Kila timu inavuna ilichopanda kwenye usajili, wengine walisajili Bendi ya Wakongo lakini inawapa matokeo wakiwatumia wachezaji wenye mikimbio mizuri mkija kushtuka wenzenu watakuwa wamewaacha mbali sana!