ONYO: Abood Bus waonye Madereva wako, Mwendokasi unaua abiria wasio na hatia

Mkuu kama umekusudia ongea na trafk gar ikisimama au kwenye bus humo umo kuna no za ratco una report usisubir ad ajal itokeee ndio useme nlijua tutapata ajal dereva nlimuona mda mref nk aitosaidia ajal ikishatokea
 
Daah hawa jamaa wote wa mabasi makubwa na wenzao wa serekali wanajikuta wao pekee ndo wenye haki ya kutumia barabara. Wanaovateki hovyo tena hata hawajali uwepo wa gari zingine hasahasa hizi gari ndogondogo.
 
Huyo nahisi atakuwa dereva mmoja anafuga ndevu nyingi jina limenitoka yupo rafu sana.Na huwa Morogoro anatoka wa kwanza.
 
Huwa wanabeti. Kuna siku nimepanda basi nilikaa kule mbeli niliooa dereva na wahudumu wanaongea kiswahili cha kinyume ili abiria tusielewe. Wakawa wanasema kwamba dereva kila siku anawachania mkeka.

Wakawa wanamsifu dereva wa kampuni fulani kwamba hajawahi kuwaangusha, kila anakohamia mikeka inatiki tu.

Kimoyomoyo nikawa najisemea bora huyu anayechana mikeka lakini tunafika salama.
 
Abiria mlitakiwa kumkomalia hapo hapo

Ova
 
Mkuu kama umekusudia ongea na trafk gar ikisimama au kwenye bus humo umo kuna no za ratco una report usisubir ad ajal itokeee ndio useme nlijua tutapata ajal dereva nlimuona mda mref nk aitosaidia ajal ikishatokea
Hizo number za simu za ratco hazimo, yule driver wa truck alikwenda kuwaambia traffic police wa Mdaula, wamemkamata wakampiga fine baada ya abiria kutoa ushahidi
 
Usijaribu hilo!Kuna wakati hata abiria wenzio wanaweza kukugeuka.Waswahili hatuthamini uhai
Upo sahihi hata tuliposimamishwa na polisi mdaula ikawa babeli wengine wanataka kuwahi wanamwombea msamaha wengine wanawataka askari wamuadhibu
 
Huyo nahisi atakuwa dereva mmoja anafuga ndevu nyingi jina limenitoka yupo rafu sana.Na huwa Morogoro anatoka wa kwanza.
Ni huyo ana kimzuzu hivi, kuna mtu mzima (anakaribia ubabu) amemfuata akamuuliza kwanini anaendesha rough akajibu anataka kurudi Dar saa 12 jioni
 
Daah hawa jamaa wote wa mabasi makubwa na wenzao wa serekali wanajikuta wao pekee ndo wenye haki ya kutumia barabara. Wanaovateki hovyo tena hata hawajali uwepo wa gari zingine hasahasa hizi gari ndogondogo.
Lakini yule dereva ana kitu hakiko sawa kichwani ukimchunguza na kumsikiliza utagundua hayuko sawa kisaikolojia
 
Acha gubu mtoto wa kiume hii post ni ya pili kwa siku moja
 
Na wewe pia una shida . Ulishamlalamikia dereva huyo hapo kabla na hadi uzi ukaleta humu , kwa nini usimonye kabla ya safari maana hadi namba za basi unazijua?
Binafsi nikipanda basi halafu kukawa na experience mbaya ya dereva au basi lenyewe nitawaambia ikishindikana sitopanda tena basi hilo.
Watch out!! usije kuleta uzi wa tatu ukiwa kwenye ajali kamili ya basi hilo hilo na dereva huyo huyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…