Forex as foreign exchange markets kwa Tanzania inasimamiwa na BOT. Lakini online trading haitambuliki Nchini, by the way haihusishi Shilingi ya Tanzania. Hivyo BOT hawashughuliki nayo maana haiathiri Shilingi yetu.
Lakini pia hata Nchi zilizo endelea kama US, UK, Australia, Japan n.k watu wanapata faida na wengine wanaunguza. Unapounguza account yako haimaanishi broker ndio kachukua, hapana! Brocker anapata tu sehemu ya hasara unayopata. Kwa kawaida zile hela zinaingia kwenye virtual Market na kuongeza mzunguko huko.
Ikiwa kama biashara zingine risk management ndio msingi, hamna namna yoyote ile nyingine. Ukiwa na capital ya dola 500-1000 kwa bongo na pia ukawa risk manager mzuri. Hata kama wewe ni average trader utafanya vizuri.
Goodluck kwa watakaoanza kutrade, risk management is everything, avoid greedy at every cost.
Regards