Onyo kwa wahitimu wanaotarajia kuomba kujiunga na kozi ya diploma ya famasi

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,333
Reaction score
5,845
Naomba nitumie jukwaa hili kuwaonya wazazi na wahititimu wanaotarajia kujiunga na vyuo vya ngazi ya kati kwa program ya famasia.

Kwanza niwaeleze kwa nini ninaandika kutoa tahadhari hii.

Kwa muda mrefu sasa kumekuwa na mfumuko wa ongezeko la vyuo vinavyodahili wanafunzi wengi wa famasi na kutoa wahitimu wengi pia ingawa ni karibu asilimia 50 huwa hawamalizi diploma ukilinganisha na walivyoanza.

Lakini kibaya zaidi ni kwamba hao waliobahatika kumaliza diploma,ni asilimia isiyozidi 30 ndio hufanikiwa kufaulu mitihani ya leseni katika miaka mitatu baada ya kumaliza chuo.

Nasema katika miaka mitatu kwa sababu wengi hufeli mitihani ya leseni na kurudia katika hiyo miaka kabla hawajafaulu.Wanaofaulu mitihani yote kwa mkao mmoja ni asilimia isiyozidi 20!

Sasa naomba niwatahadharishe kwamba;

1. Usikubali kupeleka chuo mwanao chenye wanafunzi zaidi ya 100 kwenye darasa moja.
Vyuo vinafanya uhuni sana ili mwanao afaulu tu lakini atakutana na kigingi sio cha kawaida wakati wa mitihani ya leseni

2. Mzazi omba kujua iwapo chuo kina wakufunzi wa kutosha ikibidi uliza baraza la wafamasia.

Iwapo chuo hakina wakufunzi wa kutosha kwa uwiano wa mkufunzi mmoja kwa wanafunzi 15 achana na chuo hicho bora umpeleke mwanao VETA utanishukuru baadae.

3. Iwapo chuo hakina mpango mzuri wa kupeleka wanafunzi kwenye mafunzo kwa vitendo,yaani mwanafunzi anatafuta mwenyewe afanyie wapi na hakuna usimamizi wa walimu wao,achana na hicho chuo utakuwa unapoteza pesa bure

4. Kama utaweza,uliza chuo unachotaka kujiunga wakwambie idadi ya wahitimu wao wa miaka mitatu tu nyuma walio na leseni.

Kama hawana majibu hiyo itoshe kukuonesha kuwa hawajali na wanachojali ni pesa yako tu unapokuwa hapo chuoni.

Mwisho nihitimishe kwa kusema mafunzo ya famasi yanahitaji ujitume kujifunza mambo mengi bila kumtegemea mkufunzi pekee kwani watunga mitihani hawajali kile unachojua bali kile wao wanachojua na kutaka uwe kama wao Pambana sana ili uwe kama wao.
Alamsiki
 
Yaani diploma ndio ushauri wote huu ukifika bachelor afu kozi pharmacy aisee 😂 😂 😂
Bachelor ni nini unaongea wewe?
Wote wanasomea kutii amri ya kwenye cheti cha dawa kilichoandikwa hata na mtu mwenye certificate ya clinical medicine

Hizo degree za big result now mmeambiwa mwende veta kwa sababu hamna lolote!
Mtu una degrii ila hujui gharama ya kusomesha diploma ni zaidi ya milioni 12 halafu unakuja na dhihaka eti diploma tu!
 
Mwambie huyo mjinga
 
upo sahihi
 
Ukweli mchungu umetimiza wajibu
 
Bachelor ni nini unaongea wewe?
Wote wanasomea kutii amri ya kwenye cheti cha dawa kilichoandikwa hata na mtu mwenye certificate ya clinical medicine

Hizo degree za big result now mmeambiwa mwende veta kwa sababu hamna lolote!
Mtu una degrii ila hujui gharama ya kusomesha diploma ni zaidi ya milioni 12 halafu unakuja na dhihaka eti diploma tu!
Mbona mkali😂
 
Mkuu Cashman unastahili kujengewa mnara.

Sio lazima wote wakuelewe ila umelenga kwenye mshono. Pia changamoto na matatizo Mengi yanayowapata vijana wanaosoma kozi za Diploma ya famasi ni kutokana na udhaifu wa uwajibikaji wa Baraza la famasi( pharmacy council of Tanzania).

Baraza la famasi ndio lenye jukumu la kusimamia na kuhakikisha ubora na viwango vya elimu vinavyotolewa vina ubora unaotakiwa. Kwa mantiki hiyo kushindwa kwa vijana kufaulu mitihani ya leseni ni matokeo mabovu ya uwajibikaji na utendaji wa Baraza la famasia.

Baraza la famasi limekuwa likiendeleza unyonyaji wa kukusanya ada za mitihani kupitia wahitimu.

Utitiri wa kuwepo kwa vyuo vingi vya binafsi vunavyotoa elimu ya diploma ya famasi vimepelekea mazingira ya rushwa au viashiria vya rushwa kutoka kwa wamiliki wa vyuo binafsi kuhakikisha vinaendelea kutambulika na usajili wa baraza.

Baraza la famasi linapaswa kuwajibika kwa kushindwa kutekeleza wajibu wake na kupelekea upotevu wa pesa na rasilimali watu sababu ikimbukwe mamilio ya pesa za ada zinazolipwa kwa wanafunzi zinapotea kama wanafunzi hawapati na kufaulu mitihani ya leseni.
 
Duh!! Sasa itakuaje maana ninadogo nataka nimpeleke akaosomee iyo pharmacy
 
Back
Top Bottom