Onyo kwa wasanii wanaofuatana na wanasiasa

City Owl

JF-Expert Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
3,475
Reaction score
7,571
Hivi karibuni kumezuka wimbi la wasanii wanaofuatana na wanasiasa kwenye michakato yao ya kutangaza nia. Wao wanadai eti ndio Kazi yao. hawaoni kwamba wanatumiwa kuleta watu walishwe uongo wa mafisadi. Ninyi wasanii nani kawaroga??

Naomba mjue kwamba mnazorotesha jitihada za sisi mashabiki wenu hasa sisi vijana ambao ndo tunahitaji kuwang'oa hao wezi walioko serikalini na kufanya mapinduzi ya kifikra kwa wananchi walio wengi.

Sisi mashabiki ndo tunaingia kwenye show zenu, tunanunua Kazi zenu, tunawapigia kura tuzo za kitaifa na kimataifa (mnapata hela) nyingi kuliko hizo mnazopata kwa kufuatana na hao mafisadi. wasanii msiume mikono inayowalisha kila siku kwa huo wa mwezi mmoja.

Nasema acheni huo uchu wa fedha mara moja. kuweni kama Ali choki au hata Weusi na akina Kala Jeremiah. Wekeni uzalendo mbele vinginevo mnaharibu career zenu.

Sisi tumewasupport, kama leo mnatugeuka; mtaona matokeo.
 
Hapa najua kuna mtu umemsema ila ngoja waje wafuasi wake uwaeleze vizuri
 
ahaaaaaa kumbe ndo maana msanii akiwa na mwanasiasa wa chama X, basi wupande wa pili wanaleta nyuzi za kumponda kumbe kuna siasa ndani yake
 
Ndio maana kura hawapigi watoto, ni mpaka uwe umefikisha miaka 18 tukiamini hana upuuzi kama wa kwako...

Na ushaambiwa linganisha nguvu ya hoja, sasa kama we unaona ""mapenzi au pesa"" itakufanya umchague raisi daaah Taifa linazidi kuelekea pabaya inatakiwa tuangalie upyaa suala la vigezo vya uandikishaji... Musicians are there for entertainment na kuwavuta wasio na hulka ya kuwasikiliza wanasiasa waende kuzipima sera zao.......................................................
 
Mkiniona baada ya Uchaguzi sisklilizi au kucheza muziki wa mwanamuziki yeyote aliyeshiriki kampeni ya mgombea yeyote wa chama chochote, HARAKA SANA NIPELEKENI MIREMBE.
 
Kama wanaitwa kupiga shoo bila kusaidia kutangaza anayetaka kura hiyo nayo ni kazi sio siasa.

Mtu asichukue pesa ndefu kisa siasa? Kazi yao kutumbuiza na wanatumbuiza.

Anayechukua mic na kuongelea siasa ni uamuzi wake kama mwananchi na atajiju.
 
Mkuu hebu iweke kiutamu sijakupata unamaanisha wasanii wasipige shoo za wanasiasa wanaowaalika kutumbuiza hata kama ni kwaajili ya pesa kwa sababu unasema nyinyi/sisi mashabiki wao tunanunua kazi zao na kuingia kwenye shoo zao kwahiyo hiyo pesa tunayowaingizia sisi haina haja ya wao kutaka kupata zaidi kwenye vyanzo vingine hasa kwenye siasa ndo unacho maanisha ??????????????????????????????????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…