ONYO: Timu itakaayomsajili Bernard Morrison (Toto tundu) itakuwa imekubali kukumbatia Mzinga wa Nyuki

NALIA NGWENA

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2016
Posts
10,587
Reaction score
13,425
NALIA NGWENA niliona aibu Mimi kitendo cha Bernard Morrison kumpora pesa waziri wa sanaa na michezo Mhe. Chana.

Kwa haraka haraka ni kama kitendo cha kuchekesha lakini kwa NALIA NGWENA the great thinker mkombozi wa Fikra mpya kwa kweli siyo Jambo la busara (kiungwana).

Lakini tukio lingine kwenye mchezo wa Mbeya city vs Yanga Toto tundu Bernard Morrison alipokua akishangilia baada ya kutupiwa makopo na takataka the Super Ben alirudisha kwa mashabiki.

Sijui hili limekaaje kikanuni nafikiri Bodi ya ligi na TFF Kama atakua amefanya kosa basi atawajibishwa bila Shaka.

Tukio lingine lililo nichosha zaidi nakuona kabisa Bernad Morrison ni mtovu wa nidhamu ni pale Ikulu, Eng. Hersi kumtambulisha mbele ya Mhe. Rais lakini hakusimama kwa kweli aibu niliona Mimi na ninaimani kabisa Hersi alijisikia vibaya lakini alijikaza tu.

Lakini alipotambulishwa Mzinze alisimama Ila ilipofikia zamu yake aligoma kabisa kusimama.

Timu yoyote ya Tanzania itakayomsajili Bernard Morrison itambue Kabisa itakua imekumbatia mzinga wa Nyuki.

Nawasilisha hoja

 
Aahaaaaa

Morrison hapendi unafiki,
 
Hakuna mchezaji pale
 
Wacha uchawi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…