ONYO: Timu itakaayomsajili Bernard Morrison (Toto tundu) itakuwa imekubali kukumbatia Mzinga wa Nyuki

Msizipangie timu, huyu mchezaji aliachwa na Simba kwa utovu wa nidhamu lakini yanga walifikiri wamewakomoa Simba kwa kumsajili lakini hukusikia viongozi au mashabiki wa Simba wakimnenea mabaya kwa kifupi kama mmeshindwana naye achaneni naye kwa amani
 
singida big stars watajiju
 
Alifanyaje ikulu?
Wakati Rais wao Eng Hersi akitambulisha wachezaji kwa Mh Rais alitajwa mara mbili mchezaji chipukizi klabuni Clement Mzinze lakini Morrison ndio akasimama badala ya Clement japo watu walifurahia kama kituko ila ilipofika zamu yake ya kutambulishwa akagoma kusimama tena mara mbili zote, hii haikuwa tabia njema hasa ukiangalia walikuwa wanatambulishwa kwa Rais wa nchi.
 
Msizipangie timu, huyu mchezaji aliachwa na Simba kwa utovu wa nidhamu lakini yanga walifikiri wamewakomoa Simba kwa kumsajili lakini hukusikia viongozi au mashabiki wa Simba wakimnenea mabaya kwa kifupi kama mmeshindwana naye achaneni naye kwa amani
Nakubaliana na wewe, ukimshindwa mke mwache aende usimsindikize Kwa makandokando.
 
Rudisha kwao akale egusi na fufu.
Tz nchi peke hata mkimbizi toka Malawi atatukuzwa
 
Ila Hersi naye kwa nini alimuita "toto tundu"? Tukienda kipro, alikuwa na haki ya kuuchuna. Utani wa kwanza kusimama alipoitwa Mzize nao haukuwa na madhara, ulikuwa ni mkusanyiko wa kufurahi na kusherehekea, kama kuna mtu alikwazika huyo ndiyo ana shida.
 
Yanga hamna utamaduni wa kukosoa viongozi wenu hasa kipindi kama hiki ambacho timu inaonekana kufanya vizuri ila Morrison hakutakiwa kuachwa.

Morrison hata kama kacheza mechi chache ila mchango wake kwenye timu ni mkubwa sana. Ukisema kacheza mechi 15 tu, je umehesabu hata zile ambazo alikuwa tayari kucheza ila hakupangwa? Umehesabu goli alilofunga dhidi ya Marumo ambalo kwa kiasi kikubwa ndiyo lililoipeleka Yanga fainali? Tofauti ya zawadi za fedha na medali kati ya kuishia nusu fainali na kucheza fainali zinatosha kumlipa mshahara wa mwaka mzima, kuvumilia utoro wake na chenchi ikabaki. Labda uniambie sababu kubwa ni alivyogoma kufanyiwa sub ile mechi ya Chamazi au uniambie utani aliofanya Ikulu.

Kuna ule uzi jamaa mmoja aliuliza mahesabu ya kihasibu kuhusu usajili wa Aziz Ki. Goli alilofunga dhidi ya Club Africain lilitosha kufumbia macho madhaifu yake mengine yote aliyoonyesha msimu mzima maana bila lile goli Yanga ndiyo ilikuwa bye bye mashindano ya kimataifa. Ni kwa mtazamo huo huo naangalia thamani ya Morrison.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…