🚨ONYO: Ukinunua gari used kabadilishe Jina

🚨ONYO: Ukinunua gari used kabadilishe Jina

Samatime Magari

Senior Member
Joined
Feb 10, 2017
Posts
119
Reaction score
457
1654866615259.png
Ni Mwishoni mwa mwaka 2021 Kipindi cha sikukuu Kabla hatujaupokea mwaka Kimario alinipigia simu asubuhi asubuhi akaniambia kuna issue very sensitive anahitaji msaada wangu, Nilijaribu kudadisi issue ni nini akaniambia ni muhimu tuonane kwanza ndio ataniambia.
.
Alisisitiza issue ni sensitive sana na ni muhimu nifike kwa wakati ule ule asubuhi. Mind You Kimario anaishi Tabata Kisukuru wakati Mimi nakaaa Kigamboni.
.
Sababu Jamaa ni Mshikaji wangu sana na tushawahi fanya deals kadhaa nikaona isiwe tabu. Nikachukua Punda [Bodaboda] chapu dk kadhaa niko tabata.
.
Kufika Tabata Kisukuru nikamkuta Kimario tension iko juu uso umevimba, Nikamwambia relax brother ukiona jambo limekukuta ujue kuna namna Mungu anafanya kazi utalishinda. .
.
Kumbuka hapa bado sijaambiwa issue ni nini. Nikurudishe nyuma kidogo mwaka 2015 Kimario alinunua gari kutoka kwa Shehe Mmoja hapo Ilala [Toyota Hillux 2010]..
.
Shehe alikua anaitwa Tamim [Umri ulikua umeenda kidogo] na Shehe alikua na wake wawili na watoto wa kutosha tu wa jinsia zote [me na ke ] wakubwa tu.
.
Mwaka jana 2021 Katikati hapa Kumbe Shehe alikata moto ghafla [Inna Lillahi wa inna ilayhi raji'un]. Sasa bana Baada ya wake wa shehe kumaliza Eda taratibu za mirathi zikafata. Wasee wakakaa kugawa mali kwa kufata kanuni na taratibu na kwa mujibu wa sheria za Allah[s.w].

1654866923514.png
1654866985065.png
1654867067677.png


Shehe mzigo ulikuwepo na kuna baadhi ya marafiki zake alikuwa anawaazima/anawapa magari, Sasa to make Long story short katika Listing ya mali za Mzee gari ya Kimario nayo ilikua listed na Vijana katika kukusanya mali za Mzee wakafika kwa Kimario wanataka kuchukua chombo..
.
Kimario Baada ya kuchukua gari hakubadilisha Jina So gari iliendelea kusoma jina la Mzee na Kimario katika kuangalia katika makabrasha yake hakufanikiwa kuona sales agreement ya ile gari na Pesa alilipa cash.. .
.
Basi Vijana wakampa Week 1 akiipata sales agreemenr awajulishe waione. Week ikakata haoni kitu Basi vijana wakasema wanakuja kuchukua gari ya Mzee wao.
.
Sasa siku ananipigia simu ndo ilikua siku ya mwisho kama hana sales agreement basi arudishe gari ya watu maisha yaendelee. Sales agreement ameshaitafuta amekosa na hajui cha kufanya.
.
1654867387059.png
1654867409574.png
1654867470268.png

.
Katika kumbukumbu zangu kumbe niliscan ile document nikaiweka kwenye Email [Google] Kwa Lengo la kumtumia Ila nilikosea badala ya kumtumia Yeye nikajitumia mimi mwenyewe kwenya email yangu ya yahoo, Kufungua email document hii hapa hapa..
.
Kumuonesha Kimario ali act kama amechomwa adrenaline, Hapa ndo nikajua kuna mapenzi ya kipekee kati ya Pickup na mchaga.. .
.
Ile document ili forwadiwa chap kwa Vijana wa the Late Mzee Tamim na issue ikawa sorted. Niwakumbushe issue ya documentation na filing ni muhimu sana unapofanya manunuzi makubwa ya aina yoyote ile..
.
1654867617163.png
1654867634672.png
.
Kama unahitaji gari kuagiza, kununua hapa nchini showroom au mkononi karibu, Tunafanya kazi na dealers wa Japan, UK, Singapore na hapa nchini, dealers wanaotupa gari nzuri kwa ajili yako..
.
Simply njoo WhatsApp [0714547598] au ofisini Posta Phoenix House mkabala na Mkapa tower tutaku assist, Kama uko mkoani na unahitaji kuagiza gari karibu pia..
.
Utatupa hitaji lako tutakupa ushauri then tutakutumia options za gari ukishachagua utapewa invoice na utafanya malipo at cost [no extra cost] huko huko ulipo mpaka gari itafika na utakuja kuichukua au kuletewa ulipo..
.
1654867988410.png
1654868141155.png

.
Natumaini umejifunza kitu kama jibu ni ndio nasi usisahau kushare na wengine ili wasije wakajikuta wanapoteza vyombo na pesa au kuingia matatizoni sababu ya kutobadilisha jina kwenye card ya garu..
.
Asante
Samatime Car Dealers Co Ltd
0714547598
 
Umetoa tahadhari Muhimu sana...ila hao Vijana wa Mzee naona walikuwa Wastaarabu, na huenda Mzee aliwasomesha vizuri na wanajimudu, wanajiheshimu au naweza kusema hawana njaa.

Kawaida familia za ukubwa huo wakiamua kukuzengua pamoja na hiyo sales agreement bado mtafikishana kwenye vyombo vya sheria, plus vitisho na usumbufu wa kila aina.
 
Nna jamaa yangu hapa mpaka leo anaburuzwa na kesi dodoma,gari inaozea polisi dodoma. Dalali alimconnect na muuzaji jamaa kalipa.

Sasa dalali hakukabidhi hela yote wa muuzaji, umiliki wa gari haujabadilishwa walitumwa polisi kutoka dodoma kuja kuichukua.

Sasa mwana anakomaa kila baada ya muda flan kwenda dodoma kuweka kambi dodoma kupigania kesi. Dalali wala hatafutwi. Anakula bata kinondoni!
 
Ni ajabu sana utakuta ndio tabia hii nchi nzima
Elimu inatakiwa sana kuwaelimisha hawa watu

Unaponunua gari au nyumba au kiwanja jambo la kwanza ni kuweka jina lako hata kama kuna hela za kulipa serikalini

Wengine wananunua magari kwa mgongo wa taasisi zozote halafu jina linabaki kwenye taasisi kwa kuwa hawalipi kodi wanapoingiza nchini

Sasa hapo sijui huwa inakuwaje taasisi ikifa ingawa nyingi huwa hazifi kama za Kidini

Ila kuna watu hawaelewi mpaka yawakute
Unaachaje jina la mtu binafsi na haumjui?
Serikali lazima iweke leaflets kila ofisi za TRA au wizara husika na kila mmoja atachukua na kujisomea

Tatizo letu serikali haina mda wa kuelimisha zaidi wananchi wake ingawa vipo vipeperushi vichache sana
 
Nna jamaa yangu hapa mpaka leo anaburuzwa na kesi dodoma,gari inaozea polisi dodoma. Dalali alimconnect na muuzaji jamaa kalipa. Sasa dalali hakukabidhi hela yote wa muuzaji, umiliki wa gari haujabadilishwa walitumwa polisi kutoka dodoma kuja kuichukua. Sasa mwana anakomaa kila baada ya muda flan kwenda dodoma kuweka kambi dodoma kupigania kesi. Dalali wala hatafutwi. Anakula bata kinondoni!
Duh hii ni hatari sana
 
Kiongozi nimefatilia sana madani Yako juu ya elimu ya magari tweeter.

Mwakani mwezi kama huu natarajia kumiliki ka ndinga ka kupigia misele kupitia kwako kutoka Japan.
Nijipange Bei Gani Kwa gari hii.

IST 2007, 1490cc
Or
Vitz RS 2012 yenye 1490cc
 
Back
Top Bottom