Onyo: Usinunue Heligo Kit bila ushauri wa Daktari

Onyo: Usinunue Heligo Kit bila ushauri wa Daktari

Hizo ni akili za doctor wako, lakini ukiumwa na dalili za vidonda vya Tumbo unaenda hospitali unapima h, pirol kwa njia ya damu hakuna kitu.

Unapiga utersound hakuna kitu, unapeleka mavi hakuna kitu, Unatumbukiza mpira tumboni hakuna kitu yaani kifupi hauna vidonda vya tumbo.

Lakini ukila pili pili,.mtindi,ndizi mbivu, maharage, nyama choma,ukinywa maziwa wewe upo kwennye mateso, Lakini sasa baada ya matumizi ya heligo kit na omeprazole kwa muda wa miezi 3.

Bila hata ushauri wa daktari wala which doctor hivi sasa nakula kila kitu na niko fiti.

Hapo umepata somo gani?
Heligo kit inauzwaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Heligokit ni kwa ajili ya vidonda vilivyosababishwa na bacteria Helicobacter pylori na ni combination ya dawa tatu Antibiotics mbili na proton pump inhibitor moja (hizi hupunguza acid tumboni) dawa hizo ni Tinidazole,clarithromycin na lansoprazole.

Omeprazole ni kwa ajili ya vidonda vilivyoletwa na matumizi makubwa ya dawa za maumivu (NSAIDS)

So cha muhimu ni kujua sababu ya vidonda vyako kabla ya kutumia dawa na hii yaweza kujulikana kutoka kwenye history yako au vipimo vya maabara kama H.pylori antigen test from stool or blood.

Na sio kweli kwamba ni kwa vidonda vilivyoshindikana tu
Unajua pia chief hii huenda inasababishwa na nini..

1. Huenda dr. Yupo shallow, hii sababu ambayo sitaki kuiamini saana.

2. Dr. Kutibia wagonjwa wengi kuliko wastani ambao anapaswa kuhudumia, mwishowe dr. Anajikuta amechoka sasa masuala ya kuanza kumdadavulia mtu kumuelezea kwa kina anajionea tabu ndio mwishowe hayo anajibu kumridhisha na kumfukuza mgonjwa kijanja.

Serikali waangalie, madaktari wahudumie wagonjwa kwa wastani wa idadi ya watu kitaaluma( hospitali ziongezwe na madaktari waajiriwe kwa wingi kubalansi mzani)

Hata mashuleni, mwalimu anaefundisha darasa la wanafunzi 40 maximum, ni tofauti kabisa na yule anaefundisha wanafunzi 100+.
Mwanafunzi wa darasa la wanafunzi 40 na huyu 100+ kuna vitu vingi wanatofautiana,
Mwalimu wa darasa la wanafunzi A ni rahisi kujua shida ya mwanafunzi mmoja mmoja, kusaidia n.k, tofauti na huyu wanafunzi 100+
 
Asante nilitumia mwaka jana ilinisaidia!
Habari.
Nikienda Pharmacy niseme nataka Helgo Kit?
Wao watajua moja kwa moja ama natakiwa niwe more specific... Mfano dozi ya siku ngapi etc.
 
Kama umepatikana na H. Pylori:

1: Helgo kit huwa inajitosheleza kwani ni mchanganyiko wa antibiotics na antiacid.
Habari.
Nikienda Pharmacy niseme nataka Helgo Kit watanielewa.
Ama natakiwa nitaje specifics mfano dozi kiasi gani/mg ngapi.
Ama natakiwa niwatajie hiyo lost ya madawa sijui omprazone, trycline, PPI
 
Heligokit ni kwa ajili ya vidonda vilivyosababishwa na bacteria Helicobacter pylori na ni combination ya dawa tatu Antibiotics mbili na proton pump inhibitor moja (hizi hupunguza acid tumboni) dawa hizo ni Tinidazole,clarithromycin na lansoprazole.

Omeprazole ni kwa ajili ya vidonda vilivyoletwa na matumizi makubwa ya dawa za maumivu (NSAIDS)

So cha muhimu ni kujua sababu ya vidonda vyako kabla ya kutumia dawa na hii yaweza kujulikana kutoka kwenye history yako au vipimo vya maabara kama H.pylori antigen test from stool or blood.

Na sio kweli kwamba ni kwa vidonda vilivyoshindikana tu
Habari.
Nikienda Pharmacy niseme nataka Helgo Kit watanielewa.
Ama natakiwa nitaje specifics mfano dozi kiasi gani/mg ngapi.
Ama natakiwa niwatajie hiyo lost ya madawa sijui omprazone, trycline, PPI.

Mfano wakisema hawana hiyo Heligo Kit, naweza kuchukua combination ipi ya dawa + amount zake ikatibu H Pylori.
 
Habari.
Nikienda Pharmacy niseme nataka Helgo Kit watanielewa.
Ama natakiwa nitaje specifics mfano dozi kiasi gani/mg ngapi.
Ama natakiwa niwatajie hiyo lost ya madawa sijui omprazone, trycline, PPI
Kwa Pharmacy wanao uwezo wa kuelewa na kutoa dawa, ingawa hizi ni dawa zinazotolewa kwa kufuata mwongozo wa cheti cha daktari.

Kitu cha msingi kabla ya kwenda duka la dawa:

1: Je una gastritis au vidonda vya tumbo?

2: Je H. Pylori amethibitishwa kuwa moja ya chanzo cha tatizo husika?(Umepima).

3: Je kwa eneo ulilopo, Heligo Kit inafanya kazi vyema? (Haijajenga usugu). Maana kumekuwa na hali ya usugu kutokana na matumizi yasiyo sahihi.

Hapo ndipo wataalamu huweza kutoa dawa tofauti kwa lengo husika.

Ni muhimu kumhusisha mtaalamu wa afya kwenye hili.
 
Kitu cha msingi kabla ya kwenda duka la dawa:

1: Je una gastritis au vidonda vya tumbo?

2: Je H. Pylori amethibitishwa kuwa moja ya chanzo cha tatizo husika?(Umepima).
1. Sina hakika kama nina gastrisis. Lakin sometimes huwa nasumbuliwa na GERD ile umelala horizontal halafu ACID REFLUX inapanda kooni. Unapaliwa.

2. Nasumbuliwa sana na tatizo la gesi/kujamba. Najamba sana mkuu. Muda wote tumbo Lina unguruma.. geri tu muda wote najamba.
Hii naichukulia kama dalili ya H.pylori.

Nakwepa kwenda hospital maana sipendi vile kuingiziwa endoscopy mdomoni, kupeleka kinyesi, kuchomwa ma sindano .

Okay, let's keep other problems constant... But hili la gesi/flatulence/kujamba mkuu linanipa shida sana. Mwaka wa nne huu.

Mpaka naogopa kulala na mtu.
Ama nitumie dawa gani mkuu. Hiyo Helgo Kit si inaweza kunisaidia?
 
Lukonge umeniacha kwenye mataa kaka

Kama ni GERD, tiba yako ya msingi si Heligo Kit. Haitakuwa na msaada wowote kwako. Heligo kit inatumika kama una H. Pylori kama kisababishi cha Gastritis au Peptic ulcer/ vidonda vya tumbo.

Hakiki tatizo lako la msingi, kuna magonjwa huja na dalili za kufanana au yanakuwepo kwa pamoja. Tambua kama una:
1: Gastiritis/kututumka
2: GERD
3: Vijiwe kwenye mfuko wa nyongo.

GERD huweza kuleta Gastritis au Vidonda pia.

Tiba ya GERD huusisha:
1: Dawa
2: Mabadiliko kwenye mfumo wa maisha
3: Upasuaji kama kisababishi chake kinahusiana na upasuaji.

1: Dawa ni zile za ku-control asidi kwenye njia ya chakula.

2: Tiba mwambata kwa wagonjwa wa Gastroesophageal Reflux Disorder (GERD):

1: Epuka vyakula vya mafuta mengi.

2: Epuka vyakula vyenye kuleta muwashawasha kama tangawizi na pilipili.

3: Epuka vyakula vyenye uchachu kama limao, ndimu, machungwa au embe au pasion visiyoiva vizuri.

4: Epuka juice za viwandani na kahawa.

5: Kula saa tatu kabla ya kwenda kulala na usishibe sana.

6: Weka kitanda chako nyuzi 30-45, kwa kuweka kitu kinachoinua godoro upande wa kichwa.

7: Tumia dawa ulizopewa kwa uaminifu.

8: Usitumie dawa za kulainisha misuli/relax bila sababu za msingi.

Kuwaona wataalamu ni vyema ili kutanabaisha tatizo la msingi.
Si kila ukiwnda utapima endoscopy.
 
Kama umepatikana na H. Pylori:

1: Helgo kit huwa inajitosheleza kwani ni mchanganyiko wa antibiotics na antiacid.

2: Wakati mwingine huwa kunatolewa na mchanganyiko wa dawa ambazo hazijachanganywa/unganishwa kwenye package moja, lakini kwa uwezo sawa na ukipata namba moja hapo juu.

NB: Kulingana na aina ya mgonjwa, wakati mwingine huwa kuna haja ya kuendelea na dawa ya ku-control acid kwa muda mrefu baada ya dose hapo juu ya kuondoa H. Pylori kulingana na madhira ambayo huwa yameshatokea kwen
 
Unajua pia chief hii huenda inasababishwa na nini..

1. Huenda dr. Yupo shallow, hii sababu ambayo sitaki kuiamini saana.

2. Dr. Kutibia wagonjwa wengi kuliko wastani ambao anapaswa kuhudumia, mwishowe dr. Anajikuta amechoka sasa masuala ya kuanza kumdadavulia mtu kumuelezea kwa kina anajionea tabu ndio mwishowe hayo anajibu kumridhisha na kumfukuza mgonjwa kijanja.

Serikali waangalie, madaktari wahudumie wagonjwa kwa wastani wa idadi ya watu kitaaluma( hospitali ziongezwe na madaktari waajiriwe kwa wingi kubalansi mzani)

Hata mashuleni, mwalimu anaefundisha darasa la wanafunzi 40 maximum, ni tofauti kabisa na yule anaefundisha wanafunzi 100+.
Mwanafunzi wa darasa la wanafunzi 40 na huyu 100+ kuna vitu vingi wanatofautiana,
Mwalimu wa darasa la wanafunzi A ni rahisi kujua shida ya mwanafunzi mmoja mmoja, kusaidia n.k, tofauti na huyu wanafunzi 100+
Je kma ni mtoto amepatikana na Hpylori anaweza kutumia , mtt wangu alitumia dawa siju 14 lakin bado tumbo halijapoa nkaambiwa ninunue heligokit
 
Je kma ni mtoto amepatikana na Hpylori anaweza kutumia , mtt wangu alitumia dawa siju 14 lakin bado tumbo halijapoa nkaambiwa ninunue heligokit
Kutibia H. Pylori si emergency(hauhitaji haraka). Hizi dawa unazomsukumia kwa wingi zinaweza kuleta shida zaidi/maumivu.

Jambo la msingi ni tathmini nzuri na tiba inayofaa. Unaweza kuanza kwa ku-control acid na vyakula. Tumbo likiendelea vyema baada ya wiki moja au mbili unatibia hiya H. Pylori.
 
Kweli nimeenda hospital wamesema kuna mdudu katk choo kikubwa nimeandikiwa hiyo dawa now Niko day 3 nimepewa za wik mbil ila nikali sana
Natumaini unaendelea vizuri mkuu, ulinunua kiasi gani za week mbili? Mie ndiyo naanza leo,
Nimeambiwa za wiki 2 (80,000/=)
 
Back
Top Bottom