ONYO: Usinunue simu kwa mtu

ONYO: Usinunue simu kwa mtu

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1630916097115.png
Kununua Simu kwa Mtu kumewaweka Watu wengi kwenye matatizo kutokana na Simu husika kuwa na historia ya kuhusika katika matukio ya Uhalifu.

Hakikisha Simu unayonunua ni halali kutoka kwa Muuzaji unayeweza kuthibitisha kwa risiti kwamba alikuuzia Simu hiyo. Usishawishike na bei ndogo zinazotangazwa na Watu binafsi wanaouza Simu.

#JamiiForums #DigitalSafety
 
Word!.

mie mwenyewe nishapigwa, sinunui simu kwa mtu hata iwe laki bora nipoteze ninunue dukani
 
Watu hawana utaratibu wa kuandikishana ndio maana utapeli hauishi.

Hata kwenye kukopeshana hivyo hivyo mtu unamkopa bila maandishi kisa unamjua, akikuzungusha ndio unaanza kujuta

Ukinunua kitu muandikishane tarehe na mpaka siku na muda.

Tena kwa mashahidi.

Hakuna mahali duniani Inakataza kununua kitu kwa mtu ila lazima kuwe na maandishi
 
Kununua simu kwa mtu ni utamaduni ambao utadumu miaka mingi. Suala kubwa ni kwamba unanunua kwa nani?

Kama unanunua kwa wavuta bangi lazima ununue matatizo.
 
Sijawahi kununua simu dukani.

Ila kilichonikutanisha na askari mara nyingi ni mimi kua mtoa lock wa simu za wizi.
 
Back
Top Bottom