Onyo: Utumiaji wa mabaunsa bila kufuata taratibu utaleta maafa

Onyo: Utumiaji wa mabaunsa bila kufuata taratibu utaleta maafa

mwehu ndama

JF-Expert Member
Joined
Nov 12, 2019
Posts
2,472
Reaction score
9,542
Kumekua na kasumba ya watu binafsi au kampuni kutumia mabaunsa kama walinzi binafsi na wengine wamekua wakiwatumia mpaka katika migogoro ya ardhi Tena mabaunsa wasiokua na usajili maalumu kupitia jeshi la polisi.

Hawa mabaunsa wamekua wakitumia nguvu kubwa , huku wakiacha majeraha na maumivu makubwa pasipo kujali taratibu za Sheria wala miongozo ya katiba kwa wahanga .kwao maslahi toka kwa waajiri ndio kipaumbele kikubwa.

Ila Mimi nikupe onyo wew unaetaka kujivika ubaunsa katika kumbi za starehe, mtu binafsi au migogoro ya ardhi kwamba hakikisha unatumikia kampuni iliyosajiliwa KIHALALI na kupewa kibali na jeshi la polisi Tz..Tofauti na hivyo yatakukuta kama yaliyomkuta baunsa maeneo ya salasala Dsm
 
Back
Top Bottom