Ni hoja zipi hizo mlizozileta zikawa kweli, maana kwa kweli ni zamani sana tangu nione Mtanzania ameandika chochote chenye mantiki au mashiko humu. Wengi mumezoea same old script za mara Kibera mara Turkana mara SGR Mchina ametupiga, na nikiwaalika mtoe facts data kwa data Mchina ametupiga vipi, mnaishia mipasho.
Kuna uzi niliwahi kuleta humu uliotolea taarifa za kitaalam za SGR yetu, nikawaalika tupelekane hatua kwa hatua mkapiga kimya na kuendelea na nyimbo za Mchina amewapiga Wakenya.
Tatizo lenu kubwa ni kwamba mkikaririshwa kitu, yaani hadi Yesu arudi ndio mtakubali kujiongeza au kutumia akli zenu wenyewe.
Huko Kenyan talks binafsi huwa siendi maana ni vigumu sana kuwakuta Wakenya wamekusanyika kwenye mtandao mmoja kama ilivyo kwa Watanzania hapa JF. Ni rahisi sana kuwakusanya Watanzania wajazane kwenye mtandao mmoja na washinde humo kutwa maana ni hulka yenu ya kiujamaa, hivyo mnaweza kushinda humu mkipiga soga. Wakenya wengi labda uwakute kule Twitter, sehemu ambapo anaandika maneno machache na kuendelea na kazi zake za siku.
Wakenya wakikerwa na serikali huwa wanajitokeza nje kabisa tena kwa mamilioni, sio kama Watanzania mtajazana humu mkiandika riwaya za mnavyochukizwa na udikteta halafu ikifika siku ya kuitana kwenye maandamano hakuna hata mmoja ataachia keyboard aingie barabarani.
Mtandao wa kijamii wenye Wakenya ambao nimewahi kutumia muda wangu labda ni
Wazua. Serious talk about wealth.
Lakini muda mwingi huwa nakwenda Twitter