Oparesheni za Kijasusi zilizofanikiwa zaidi katika Historia

Oparesheni za Kijasusi zilizofanikiwa zaidi katika Historia

Wewe ni mjinga na mpumbavu kichwani una goroli za beskeli.
Unajya unavyotutesa kwa, kukoti Uzi mrefu sisi tunao tumia simu?
Ndio maana mnajibiwa hivi " bando ni langu simu yangu halafu unipangie? Kama unateseka unaacha kwa nini uteseke mkuu
 
Ndio maana mnajibiwa hivi " bando ni langu simu yangu halafu unipangie? Kama unateseka unaacha kwa nini uteseke mkuu
Unagongwa na vindege vinavyokula kuku tena kupitia Ass hole.

Ole wako nipate Ban wakat ww ndio umeanza..
 
Atakuwa anaogopa au information hazipo available, ila mm naijua moja walishawahi kuifanya pale uwanja was ndege was Bujumbula miaka ya 1999 kipindi hicho mtu mmoja anaitwa Mojor Pierry Buyoya alikuwa anatuletea vurugu sana hasa baada ya kupata vindege kadhaa, akawa amevipaki hapo uwanjani, vyote viligeuzwa vyuma chakavu!
Mpaka kesho jamaa hawezi sahau!!
Shikamoo kaka[emoji57] nami naomba hiyo mission kwa pm[emoji62]
 
Sasa hivi ntakua nasoma stori nikiwa na muwa mzima kabisa maana ile sehem yakwanza niliiga watoto wakishua nikanunua popcorn hata hazikuchukua round aisee.. Alafu sehem ya pili imenipita nini??
 
OPERATION BARRAS



Jana katika sehemu ya kwanza ya mfululizo wa makala hizi kuhusu Operesheni kubwa tano za kihisistoria nilianza kueleza kuhusu Oparesheni Barras.


Katika sehemu ile ya kwanza nilieleza kuhusu chimbuko la kikundi cha wapiganaji wa *West Side Boys* na namna ambavyo walishiriki katika vita ya wenyewe nchini Sierra Leon.
Mwishoni nilieleza juu ya mfululizo wa matukio mpaka kuelekea kuwateka wanajeshi wa kikosi cha STTT kijijini Mgbeni.


Tuendelee


8c6ebf39fc4b31561dd2236fd1cdefac.jpg





SEHEMU YA PILI



Baada ya serikali ya uingereza kupokea taarifa juu ya kutekwa kwa wanajeshi wake wa kikosi cha STTT jambo la kwanza kabisa ambalo walilifanya ilikuwa ni kutuma timu ya 'negotiators' kwenda nchini Sierra Leon.

Vichwani mwao walikiwa wakiamini kuwa walikuwa wanaweza kuwashaiwshi vijana wa West Side Boys kwa kuwapa vitu vya anasa ili wawaachie wanajeshi wao.


Timu hii ya negotiators iliongozwa na Luteni Kanali Simon Fordham ambaye ndiye alikuwa kamanda mkuu wa kikosi cha 1R IRISH (STTT) kilichopo nchini Sierra Leon.
Pamoja naye alikuwa na wasaidizi kadhaa ambao ni 'professional negotiators' kutoka Metropolitan Police nchini Uingereza.


Licha ya tukio hili kutoka ndani ya ardhi Sierra Leon, lakini Rais Ahmad Kabbah wa nchi alitoa ruhusu yote ya Uingereza wenyewe kuendesha juhudi za kuokoa wanajeshi wao kutokana na suala dhahiri kuwa Sierra Leon hawakuwa na weledi wa kutosha kwa namna yoyoye ile kufanikisha shughuli hiyo.


Kwa hiyo timu hii ya negotiators ikiongozwa na Luteni Kanali Simon Fordham walifanya mawasiliano na uongozi wa West Side Boys ili kuanza mazungumzo. Vijana hao walishikilia msimamo wao wa kutowaachia wanajeshi kwa madai kuwa waliwachokoza kwa makusudi kwa kuingia kwenye himaya yao kijiji cha Mgbeni.
Baada ya mazunguzo marefu sana hatimaye walikukubaliana makutano yao ya kwanza yawe siki ya August 29, 2000 nje kidogo ya kijiji cha Mgbeni kwenye barabara inayochepuka kwenda njia kuu ya Waterloo.

Katika mkutano wao huu wa kwanza upande wa Uingereza uliongozwa na Luteni Kanali Simon Fordham na uoande wa West Side Boys uliongozwa na kiongozi wao mkuu 'Brigedia' Foday Kallay.
Walipokutana, Fordham aliweka msimamo kuwa hawezi kuongea kitu chochote na Kallay mpaka pale ambapo atapewa uhakika kuwa Wanajeshi waliotekwa bado walikuwa hai.

Walibishana kwa muda wa dakika nyingi sana ambapo Brigedoa Foday Kallay akisisitiza kuwa wanajeshi waliotekwa wako hai lakini Luteni Kanali Simon Fordham aliendelea kusisitiza kuwa hawezi kuamini maneni tupu, anataka uthibitisho halisi.


Ili kuepusha mazungumzo yasivunjike, Kallay aliamuru wanajeshi wawili waliotekwa waletwe kutoka kijijini Mgbeni mpaka hapa kikaoni.

Ndani ya dakika chache tu, wapiganaji wake waliwaleta mateka wawili hapo kikoni, kiongozi wa ule msafara uliotekwa ambaye aliitwa Meja Allan Marshall na mwanajeshi mwingine Kapteni Flaherty.

Ukweli ni kwamba negotiators hawa walikuwa wanajua kuwa wanajeshi wao waliotekwa walikuwa hai kabla hata ya kufika hapa, lakini walikiwa na lengo la siri ndani ya akili zao kutaka waletwe hapa wawaone kwa macho yao.

Walipokuwa wakisalimiana na wenzao baada ya kuletwa hapo kikaoni, walipokuwa wanapeana mikono kwa ustadi mkubwa na weledi wa kijeshi Luteni Kanali Simon Fordham alimpa kikaratasi kwa siri Kapteni Flaherty. Karatasi hii ilikuwa ni ramani ya kijiji chote na majengo ya kijiji cha Gberi Bana ambacho mateka hao 11 wa kijeshi walikuwa wanashikiliwa.

ada75e1beb2c40f92d64a8bda8c95cfa.jpg


Kikao kiliendelea na hoja kuu mezani ilikuwa ni kusikiliza 'demands' za West Side Boys wanazotaka kutimizwa ili waweze kuwaachia mateka wa kijeshi walionao.

Orodha yao ilikuwa ni ndefu kweli kweli, kana kwamba matatizo yao yote walikuwa wanataka yaishe kulitia tukio hili. Katika uhalisia wa kawaida ilikuwa ni kama haiwezekani kutimiza matakwa yao yote japokuwa serikali ya Uingereza mwanzoni walikuwa na dhamira nzuri ya kumaliza suala hilo mezani.

Licha ya orodha ya wavitakavyo kuwa ndefu sana, lakini vitu vyenye uzito zaidi vilikuwa ni hivi vifiatavyo;

1. Kupatiwa vifaa vya mawasiliano, hasa simu za satelaiti.

2. Madawa ya matibabu

3. Wapatiwe kinga ya kisheria kuwazuia serikali kuwashitaki wakiamua kuweka mitutu chini.

4. Kufanywa marekebisho kwenye mkataba wa Lome (Lóme Peace Accord)…. Mkataba juu ulisainiwa mwaka 1999 kati ya serikali ya Rais Ahmad Tejan Kabbah na kiongozi wa RFU Bw. Foday Sankoh.

5. Kuachiwa kwa mateka wote wa kikundi cha West Side Boys waliopo kwenye jela za serikali.

6. Kupewa scholarship kwa kiongozi wa juu wa West Side Boys waliokuwa wanataka kwenda kusoma chuo kikuu nchini Uingereza.


Matakwa haya yalikuwa ni ya kiwendawazimu… lakini ndicho ambacho West Side Boys walikuwa wanakitaka ili waweze kuwaachia mateka waliokuwa nao.

afa62cf87baebcc7b94317ddfc3dccc0.jpg


Kikao cha pili kilifanyika siku ya tarehe 31 August.

Katika kikaoni hiki upande wa Uingereza walitimiza matakwa mawili ya West Side Boys… waliwasilisha simu za satelaiti pamoja na madawa ya matibabu.

Kutokana na kutimiza matakwa hayo mawili, West Side Boys walikubali kuwaachia wanajeshi watano kati ya wale 11.

Matakwa haya mawili ya West Side Boys yalikuwa yanatekelezeka tofauti na yale mengine, na ndio maana Uingereza walianza nayo. Yale matakwa mengine yaliyosalia kiuhalisia yalikuwa hayatekelezeki au kama yangetekelezwa basi yangeleta mgogoro mkubwa kuliko ambavyo mgogoro waliokuwa wanataka kuumaliza.


Kwa hiyo ilikuwa dhahiri kabisa kwamba jambo mbadala lilikuwa linahitajika kufanyika.


Uzuri ni kwamba kikundi cha West Side Boys wenyewe walikuwa wamefanyaakosa mawili bila kujijua.


Kosa la kwanza lilikuwa ni mateka wale watano ambao waliwaachia. Walikuwa hawajua kuwa kwenye kile kikao cha kwanza walikabidhiwa kwa siri kikaratasi cha eneo lote ambalo walikuwa wameshikiliwa. Kwa hiyo mpaka siku hii walipokuwa wanaachiwa walikuwa wamekusanya intelijensia ya kutosha kuhusu kijiji cha Gberi Bana.


Kosa la pili, lilitokana na haiba ya ujivuni wa viongozi wa West Side Boys. Walipokabidhiwa tu simu za upepo moja kwa moja waliporejea makao makuu yao walipiga simu kwenda kituo cha habari cha BBC na kufanya mahojiano LIVE kujigamba na kusisitiza kuhusu demands zao zilizosalia.

Kitu ambacho hawakukijua ni kwamba jeshi la Uingereza lilikuwa linafuatilia mawasiliano haya na kufanya 'triangulation' ili kujua kwa ufasaha zaidi simu ilikuwa inapigwa kutoka wapi.


Mateka wale wa kijeshi walioachiwa siku hiyo hiyo haraka sana walisafirishwa kwa chopa mpaka kwenye meli ya kijeshi ya RFA Sir Percivale ambayo ilikuwa pwani ya Africa magharibi ili kwenda kuwasilisha intelijensia waliyo nayo kuhusu kijiji ch a Gberi Bana kwa makamanda wa kijeshi waliokuwa kwenye meli hiyo kutoka Uingereza.



Matakwa ya West Side Boys yalikuwa hayatekelezeki. Jambo mbadala la haraka lilikuwa linatakiwa kufanyika.

Operation Barras ilikuwa inaelekea kuzaliwa.


e907b8985d97d635eb0b6de5ae99f66a.jpg

RFA Sir Percivale ambayo ilikuwa imepaki kwenye pwani ya Afrika Magharibi



Itaendelea....


THE BOLD - 0718 096 811
 
Bado hujaiona hapo juu? Post moja kabla ya post yako?
Mkuu, leo nimeamua kujisomea biblia kufuatilia maisha ya waisrael. Hivi unajua operation za kukomboa mateka zimekuwa zikifanyika katika maisha ya waisrael?

Hebu soma 1 samwel 30:1-31, lkn kama hupendi kusoma sana anzia mstari wa 15. Utaona jinsi Daud alivyo komboa waisrael, wakiwemo wake zake wawili waliotekwa na mashehe wa kifilisti.
 
Back
Top Bottom