Ngekewa,
Well tuna ardhi hatuitumii kutunufaisha kutokana na sababu nyingi ikiwa uvivu ni kubwa yao. Sasa wanakuja watu kuzalisha na kutuachia sehemu yetu ubaya uko wapi? Sisi si wageni na hawa wawekezaji lakini ukweli ni kuwa hatuwezi kuwaepuka kutokana na uvivu wetu. Ni wazuri kukaa mijini kuendeleza Usanii na kuwaacha walio wengi wakiumia kwa kilimo cha jihadi na njaa. Kazi yetu kuuza maneno lakini walio vijijini hufurahia uwekezaji pale unapofanywa kwa uadilifu. Hivyo hivyo mradi huu kama tutakuwa waangalifu utaweza kuleta manufaa makubwa kwetu.
Mimi nadhani kinachotupa shida ni ile miaka 99, wakati kisheria nadhani hati za kumiliki ardhi (lease) kulingana na sheria za sasa hivi huwa zinakupa miaka 99 (Kama sikosei)...na sidhani kama kuna tofauti kati ya mwananchi mzawa na mgeni tena basi naweza sema mgeni ananufaika zaidi kwa taratibu zilizojengwa kumvuta.
Binafsi sitakuwa na tatizo kabisa na Waarabu au Wazungu kuja nchini kuwekesha ikiwa mtazamo wangu kisiasa ni Progressive... Na ndicho wanachokiona Kikwete na CCM kwa sababu ni kundi la watu wanaojiita Progressive ndani ya CCM..
Hivyo mara nyingi mimi napopinga hoja za namna hii hua sitazami mhusika isipokuwa siasa zinazoendana na mpango uliopo. Chini ya mfumo wa hawa jamaa zetu sisi Watanzania wote ni wapangaji tu..hatuna mamlaka ya kumiliki ardhi hivyo kila kinachotokea leo hii ni kutokanma mna mfumo mbaya wa umiliki wa ardhi unaotokana na siasa mbaya za hao wanajiita Progressive.
Mimi as Conservative -Naamnini kabisa kwamba ardhi ni mali ya wananchi na ndio sababu kubwa iliyotusukuma kupigania Uhuru wetu hivyo wageni wanapokuja nchini ni dhahiri hata kama ku lease ardhi ni lazima iwe kwa faida ya wananchi wenyewe na sio kufikiria NJAA iwe sababu ya kutoa ardhi.
Huwezi kumwoza mwanao kwa sababu una njaa, au mume ni tajiri, vibaka wa mtaani wameshindwa kupanda dau, haya ndio yaliyompata baba wa yule mtoto wa kike ktk sinema ya 'Slumdog Millionea'.
Tuache fikra za NJAA..Wazee wetu wa Kariakoo wangefikira njaa wakati ule wa miaka ya 80 wasingeweza leo kuuza nyumba zao kwa dollar 800,000 isipokuwa thamanai ya nyumba hizo ilizidi kupanda ikiwa mikononi mwao..Just 1995 ilikuwa 20,000 na nyuma ya hapo with 10,000 uliweza kununua nyumba Msimbazi na Sikukuu..
Kesho ardhi hii ya kilimo tunayotaka kumpa mwarabu au hata wazungu waliokwsiha chukua watavuna mara kumi na wakisha watauza kwa faida mara 10 wakati mwananchi bado maskini..Njaa ya leo isiwe sababu kabisa ya kuuza nchi kwani binadamu hula mara tatu kwa siku, kushiba kwa mara moja haina maana njaa hiyo haitarudi na kesho ukishikwa njaa tena mwarabu atadai ardhi zaidi ili upate kipande cha mkate.
Ndivyo Wayahudi walivyoweza kuichukua sehemu kubwa ya miji ya Palestine..