...Kumbe wao wanajua kutunza rasilimali zao kwa ajili ya Vizazi vyao vijavyo eh? kwa nini na sisi tusiwaambie hizo ekari zetu 500,000 hatuwezi kuwapa kwa sababu ni kwa ajili ya vizazi vyetu vijavyo?????
...Nakubaliana nawewe kwa kiasi kikubwa. Tatizo kama wanavyoongelea wenzangu ni urefu wa mkataba na kiasi bei iliyotolewa. Kama ni miaka 99 kama wengi wanavyosuggest... hii ni noma. Kwao na sisi.
...Ipo siku yaja ndani ya miaka 99 mambo ya ardhi yaliyoikumba Zimbabwe yatatufika nasi. Hasira kutoka kwa wananchi au mmoja wa viongozi. Mambo ya kuuza ardhi yakiwa hivi, itatokea siku 'kichaa' mmoja anauza eneo walilomo na maeneo yanayozunguka eneo hilo kwa miaka mingine 99!!
...Kiongozi wa awamu hii akiuza kata, awamu ijayo atauza tarafa, anayefatia atauza wilaya..... mwingine eneo loooooooote wanaouziwa hawa wakezaji hivi sasa na mkoa wote!!
Mimi nadhani kinachotupa shida ni ile miaka 99, wakati kisheria nadhani hati za kumiliki ardhi (lease) kulingana na sheria za sasa hivi huwa zinakupa miaka 99 (Kama sikosei)...na sidhani kama kuna tofauti kati ya mwananchi mzawa na mgeni tena basi naweza sema mgeni ananufaika zaidi kwa taratibu zilizojengwa kumvuta.Well tuna ardhi hatuitumii kutunufaisha kutokana na sababu nyingi ikiwa uvivu ni kubwa yao. Sasa wanakuja watu kuzalisha na kutuachia sehemu yetu ubaya uko wapi? Sisi si wageni na hawa wawekezaji lakini ukweli ni kuwa hatuwezi kuwaepuka kutokana na uvivu wetu. Ni wazuri kukaa mijini kuendeleza Usanii na kuwaacha walio wengi wakiumia kwa kilimo cha jihadi na njaa. Kazi yetu kuuza maneno lakini walio vijijini hufurahia uwekezaji pale unapofanywa kwa uadilifu. Hivyo hivyo mradi huu kama tutakuwa waangalifu utaweza kuleta manufaa makubwa kwetu.
Tatizo letu hapa ni kuamini kitu at face value. Maadam mtu ataamuwakuleta pumba yoyote ile maadam inakandia Serikali au JK basi tutayasema yote.
Hivyo katika akili zetu unatupitikia kuwa watu wa pande zote mbili watakuwa wapumbavu wa kuingia mikataba kichwa kichwa? Kwa upande wetu tutajaribu kulinda ardhi yetu na kwa upande wa wenzetu watajaribu kulinda fedha zao. Hili suala la kusainiwa mikataba bila ya kufanya utafiti kwa kila upande linawangia akilini? Ndio tunaingia mikataba mibovu lakini tunafanya hivyo baada ya kupitia taratibu zilizowekwa ingawa tunazipindisha hapa na pale mara nyingi.
Sasa hili la kikwete kutia saini mkataba linatoka wapi? Jee mkataba huo aliusaini nani kwa niaba yake au alisaini mwenyewe. Kikawaida wakuu wa nchi hufunguwa milango ya majadiliano juu ya masuala mbalimbali na siamini kuwa JK alipokwenda huko alikuwa anajuwa kuwa Vilemba wanataka ardhi,kwani angejua angemchukuwa waziri wa Kilimo.
Kilichojiri huko bila shaka itakuwa ni scratch my back and I will scratch yours.Tunaweza vkushangaa kuwa pengine JK aliomba mengi kwa niaba ya Watanzania kwani kwa Vilemba kama kiongozi unataka kwa binafsi yako cha kufanya ni kumsifu Mfalme tu na utapewa zako. Ukiona suala la miradi linazungumzwa na Waarabu basi aliyezungumza alizungumza kwa niaba ya nchi.
Hatuwa inayofuata sasa ni kwa Waarau kuleta Wataalamu kustudy huo mradi wa ubia na kwa upande wa Tanzania tutawajibika kufuata taratibu zetu zinazohusiana na masuala kama haya.
Lakini tusije kuwapa ardhi kubwa yoote hiyo. Maana kama Kikwete kagawa ardhi kubwa namna hiyo je sisi wengine ndio tutalima wapi? yaani ikifika wakati wetu na watoto wetu je? Na Miaka 99, ni mingi sana kwa kweli, kama viongozi wetu wanaona kwamba wenyewe hawawezi kuendeleza ardhi mpaka waikodishe kwa watu sio lazima wafikiri na sisi hatutaweza kuishughulikia kama wao! Na watoto wetu wanaweza kuiendeleza piaa, kwa hiyo sio watoe ardi kubwa namna na kwa miaka mingi.Ndugu yangu hii nadhani ni oversimplification! Tuliangalie jambo hili kwa mapana zaidi huku tukizingatia kuwa huko tuendako dunia itakuwa na upungufu mkubwa wa vitu viwili muhimu chakula na maji,looks like wenzetu wanaona mbali maana si wasaudi tu hata wakorea wanatafuta ardhi afrika kwa ari mpya na kasi mpya.Hili ni suala nyeti na pana na la kufuatilia kwa makini.
Mkuu Bishanga,
Kwa nini tusilime wenyewe na kuwauzia chakula? Je, Inaingia akilini kweli kwamba wanataka kulima kwa ajili ya kulisha wananchi wao? Sound to be a shady deal, mzee. Kumbuka kwamba sasa hivi teknolojia pia inabadilika mafuta ya ethanol nayo yanaanza kuchukua mkondo. Hawa jamaa wanaangalia mbali zaidi . Miaka 99 hata 33 si mchezo kwa mwekezaji. Tunaongelea mpaka vizaizi 3.
I will sticky to my position. This deal sound to be shady period.
Asante kwa bandiko hili. Waswahili tunafahamu kirahisi sana kupitia mifano. I like the challenge na tutafakari vizuri. Kwanza jee waarabu watakubali kutukodisha visima ili tuchimbue mafuta - tufue umeme na kutumia kule Pemba kwa haja zetu na kunufaisha watoto wetu?Asante kwa ukweli. Na la kuongeza ni kwamba je kama na sisi tunataka kupata visima vya mafuta huko kwao uarabuni ili tuchimbe mafuta kwa ajili ya matumizi yetu hapa Tanzania watatukubalia hawa waarabu?. Sisi hatujashindwa kuwekeza katika kilimo bali tuna uhaba wa vifaa. Kwanini tusinunue vifaa vya kisasa vya kilimo na kufanya kilimo cha kisasa?. Kilimo ni utii wa mgongo kwa Tanzania, sasa kama tutauza ama kukodisha uti wetu wa mgongo ama muhimili wetu tutabaki na nini cha kutegemea?. Tumeuza mashirika ya umma na makampuni, waliokuwa wafanyakazi wengi wameachishwa kazi tokana na zoezi hilo la kuuza mashirika na makampuni na sasa wamekimbilia kulima na kufuga ili wapate riziki, sasa kama na huko pia wataingiliwa tunataka hawa watu wakimbilia wapi?, je tunataka kuwafanya watanzania wawe watumwa katika nchi yao kwa mtindo wa utumwa mambo leo?.
Tunahitaji uchambuzi wa kina katika hili na kuwa makini huku tukizingatia kwamba kuna vizazi vijavyo katika Tanzania. Wajukuu zetu wasije kufukua makaburi yetu na kutaka kuyafanyia uchunguzi mafuvu yetu kutaka kujua kwanini tulikuwa wapumbavu na wavivu wa kufikiri.
the maths behind the deal.....
kenya 40,000 hectares = wamepewa port yengye thamani tsh 3 trillion = $2 billion
je TZ itakuwaje
500, 000 / 40,000 = 12 and 20,000 hectares free
$2 billion x 12 = $24 billion or tsh 3 trillion x 12= 36 trillion
the govt will be selling us short if the get anything less than $24 billion or tsh 36 trillion
current budget tsh 7 trillion
4 yrs budget= 4 x 7 trillion = 28 trillion
36 trillion - 28 trillion = 8 trillion
kutokana na uchumi kukua 8 trillion itakuwa itajazilia mapungufu ya budget
TZ hectares 500, 000 = $24 billion = tsh 36 trillion
maswali ambayo yanahitaji majibu??
1.would TZ govt get $24 billion from saudis?
2.do you trust this govt to sign such a deal?
3.Je hela zitakazopatikana zitaisaidi hii nchi au zitaishia mifukoni mwa viongozi?
4. kwa nini hawa jamaa walienda serikalini moja kwa moja kwa mkulu bila kupitia TIC, hata mkurugenzi wa TIC hakuwepo na walikuwepo watu kama waziri wa mambo ya ndani(masha)?
5. long term deal in bussiness is 20 -25 yrs, sheria za ardhi bongo za miaka 33, 66, au 99. je miaka 33 haitoshi kurudisha hela yao?
6. je miaka 66 haitoshi kurudisha hela yao?
7. je miaka 99 ni kidogo au mingi?
8. kuna mtu yeyote anaejua nchi ime sign deal ya ardhi kwa ukubwa wa kuanzia hecta 100, 000 kwa zaidi ya miaka 33 au dili ambayo inakaribiana na hii tunaomba utufahamishe...
9.je tz ina hecta ngapi zenye rutuba ambazo sio jangwa?
10. je tukiwapa hecta 500, 000 zenye rutuba watanzania watabakiwa na hecta ngapi zenye rutuba?
11. je baada ya miaka 33 TZ kutakuwa na watu wangapi? je baada ya miaka 66 tutakuwa wangapi? sidhani kama tunaweza kutabiri tutakuwa wangapi baada ya miaka 99 kwa hiyo siulizi hili...

TOfauti ni kuwa wao hawajaomba kwa Fao wala Food Programme na kuepusha kuzidi kuomba chakula kwa Japan ndio JK alipoona bora ubia katika kuzalisha.
Kama tunaweza kufa kwa njaa kuliko kuitowa sehemu ya ardhi kwa ajili ya kilimo kitachotusaidia nasi basi na tuiweke hiyo ardhi na kungoja hao watoto watakaokufa kwa njaa wafufuke na kuja itumia hiyo ardhi.
Asante kwa ukweli. Na la kuongeza ni kwamba je kama na sisi tunataka kupata visima vya mafuta huko kwao uarabuni ili tuchimbe mafuta kwa ajili ya matumizi yetu hapa Tanzania watatukubalia hawa waarabu?. Sisi hatujashindwa kuwekeza katika kilimo bali tuna uhaba wa vifaa. Kwanini tusinunue vifaa vya kisasa vya kilimo na kufanya kilimo cha kisasa?. Kilimo ni utii wa mgongo kwa Tanzania, sasa kama tutauza ama kukodisha uti wetu wa mgongo ama muhimili wetu tutabaki na nini cha kutegemea?. Tumeuza mashirika ya umma na makampuni, waliokuwa wafanyakazi wengi wameachishwa kazi tokana na zoezi hilo la kuuza mashirika na makampuni na sasa wamekimbilia kulima na kufuga ili wapate riziki, sasa kama na huko pia wataingiliwa tunataka hawa watu wakimbilia wapi?, je tunataka kuwafanya watanzania wawe watumwa katika nchi yao kwa mtindo wa utumwa mambo leo?.
Tunahitaji uchambuzi wa kina katika hili na kuwa makini huku tukizingatia kwamba kuna vizazi vijavyo katika Tanzania. Wajukuu zetu wasije kufukua makaburi yetu na kutaka kuyafanyia uchunguzi mafuvu yetu kutaka kujua kwanini tulikuwa wapumbavu na wavivu wa kufikiri.
...Nimependa mno bandiko lako Mkuu! Mimi nadhani kesi inapaswa kuwa ni kwa nini sisi wenyewe hatuwezi kuzilima hizo eka 500,000 na kuwauzia hawa waheshimiwa chakula na sio wapewe ama wasipewe!!!