donlucchese
JF-Expert Member
- Mar 23, 2011
- 17,128
- 21,885
OPERATION ISOTOPE:
Ndege ya Sabena flight 571 ilikua ni ndege ya abiria kutoka Brussels nchini ubelgiji kuelekea mji wa Lod nchini israel kupitia Vienna Austria. Ndege hii ilikua chini ya shirika la ndege la taifa la ubelgiji lililoitwa Sabena.
Mnamo tarehe 8 May 1972 ndege ya abiria aina ya Boeing 707 iliyokua ikiongozwa na rubani muingereza aliyeitwa Ronald Levy ilitekwa na magaidi wanne waliokua wanachama wa kikundi cha kigaidi cha kipalestina kilichoitwa black September organization. Akifuata maelekezo yao, rubani kapteni levy aliitua ndege hiyo katika uwanja wa ndege wa Lod (baadae ulikuja kujulikana kama Ben Gurion International airport).
Mkakati wa utekaji huu ulipangwa na gaidi wa kuitwa Ali Hassan Salameth na ulitekelezwa na kikundi cha wanaume wawili na wanawake wawili waliojifanya kama couples (wapenzi) ambao ni; mkuu wa kikundi hiko aliejulikana kwa jina la Ali Taha Abu Snina, Abed Al-Aziz, Rima Tannous na Theresa Halsa. Walikua wamejihami kwa bunduki mbili (handguns), mabomu mawili ya kutupwa kwa mikono (hand grenades) na mikanda miwili ya milipuko (explosives).
Dakika 20 baadae watekaji hawa waliingia kwenye chumba cha marubani (cockpit). Baadae rubani wa ndege ile kapteni Levy aliwatangazia abiria 90 waliokua ndani ya ndege ile ,"kama jinsi mnavyoona, tuna marafiki ndani ya ndege". Kitu ambacho watekaji hawa hawakufahamu ni kwamba mkewe rubani Ronald Levy alikua ni mmoja wa abiria katika ndege ile.
Baada ya kuimiliki ndege, watekaji waliwatenganisha mateka wakiyahudi kutoka katika mateka wote na kuwaweka sehemu ya nyuma ya ndege. Ndege ilipotua, watekaji walitoa demands zao ambapo walitaka kuachiwa huru kwa wafunga 315 wakipalestina waliofungwa nchini israel kwa makosa mbali mbali ya kigaidi na kutishia kuilipua ndege na abiria wote waliokuwepi ndani. Kapteni levy alifanikiwa kutuma meseji ya siri (coded message) kwa waisrael kuomba msaada.
Waziri wa ulinzi wa kipindi hiko wa israel, Moshe Dayan na waziri wa usafirishaji Shimon Peres ambae baadae alikuja kua waziri mkuu na rais wa israel waliongoza mazungumuzo na watekaji wakati huo huo wakiandaa operation maalum ya uokoaji walioibatiza jina la 'Operation Isotope'. Kapteni levy alinukuliwa baadae akisema alipiga story na watekaji wale kuhusu mambo mengi kama urushaji wa ndege na hata mahusiano ya kimapenzi wakati abiria na wahudumu wa ile ndege wakisubiri kuokolewa.
ITAENDELEA.