Operation Paperclip: Njama ya Kijasusi Ilivyoijenga Marekani Kisayansi na Kiteknolojia

Operation Paperclip: Njama ya Kijasusi Ilivyoijenga Marekani Kisayansi na Kiteknolojia

Damaso

JF-Expert Member
Joined
Jul 18, 2018
Posts
6,236
Reaction score
10,774
Baada ya Vita Kuu ya Pili ya Dunia, dunia ilibadilika kabisa. Mataifa yaligawanyika kati ya mabepari na wakomunisti, na vita vya silaha vikabadilika kuwa vita vya maarifa na teknolojia. Marekani, kwa utimamu ya hali ya juu, ilianzisha mpango wa siri kabisa ulioitwa Operation Paperclip.
images - 2025-07-05T193118.567.jpeg

Huu ulikuwa ni mpango ambao ulikuwa moja ya hatua za kimkakati zilizobadilisha kabisa mwelekeo wa taifa hilo kisayansi, kiteknolojia na hata kijeshi. Ni kipindi ambacho taifa la Marekani lilikuwa likitazama viongozi wa mataifa mengine kwa tahadhari kubwa, watu kama, Joseph Stalin, Karl Donitz, Mao Zedong, Mfalme Hirohito na kadhalika.
images - 2025-07-05T193131.793.jpeg

Operation Paperclip ilikuwa mpango wa kuwasafirisha na kuwaajiri wanasayansi wa Kijerumani waliokuwa wamehudumu chini ya utawala wa Adolf Hitler, hasa katika maeneo ya sayansi ya utengenezaji wa roketi, silaha, vifaa tiba, kemia na fizikia. Mpango huu ulioanza mwaka 1945, huku ikiwaleta zaidi ya wanasayansi 1,600 waliokuwa na maarifa ya hali ya juu, wengi wao wakiwa ni wanachama wa chama cha Nazi, lakini walionekana kuwa muhimu kwa maslahi ya kitaifa ya Marekani.
image.jpg

Lengo kuu la mpango huu halikuwa sio tu kushinda vita vya kiteknolojia dhidi ya Umoja wa Kisovyeti USSR ambayo ilikuwa chini ya mwamba Joseph Stalin, bali pia kuharakisha maendeleo ya kisayansi ndani ya taifa hilo. Wanasayansi hawa walichukuliwa, wakapewa uraia wa Marekani na kuajiriwa katika taasisi nyeti kama vile NASA, Pentagon, NDRC, Taasisi ya Carnegie ya Washington, pamoja na AAAS na bila kusahau wengine walipata nafasi za kuingia maabara za utafiti wa kijeshi ndani ya programu za OSRD pamoja na maabara za USBWL.
images - 2025-07-05T193223.026.jpeg

Mfano bora wa mafanikio ya Operation Paperclip ni Wernher von Braun, mhandisi wa roketi aliyebuni roketi ya V-2 ya Ujerumani, lakini baadaye akageuka kuwa mtu muhimu ndani ya NASA na kuongoza mpango wa Marekani wa kutua mwezini. Bila mchango wake na timu yake kutoka Ujerumani, Marekani huenda isingewahi kufanikisha kutua kwa mwanaadamu kwenye mwezi mwaka 1969 kupitia mpango wake wa Apollo 11.
images - 2025-07-05T193237.583.jpeg

Von Braun ni mzaliwa wa Poland katika mji maarufu wa Wyrzysk, Wernher von Braun alikuwa ni genius wa kipekee sana.
Wernher von Braun alikuwa mhandisi mkuu wa Apollo Saturn V, moja ya roketi ambayo ilileta mapinduzi makubwa katika sayansi ya utengenezaji wa roketi, Apollo Saturn V inabakia kuwa ndio roketi yenye urefu mkubwa kuwa kutengenezwa, ilikuwa ni urefu wa futi 363, roketi hii ilikuwa ina urefu wa futi 60 zaidi ya ile sanamu ya Statue of Liberty.
images - 2025-07-05T193310.471.jpeg

Ni Von Braun ndo alihusika kutengeneza Apollo Saturn V na ndio ilipata bahati ya kubeba watu mashuhuri duniani, Neil Arnnstrong, Michael Collins pamoja na Buzz Aldrin.
a598e39f-6e30-4ce7-ac3e-9173a7a09d1d.jpeg

Mbali na anga, mafanikio ya Operation Paperclip yalisambaa hadi kwenye maendeleo ya silaha, tiba za kisasa, na teknolojia ya kompyuta. Marekani iliwapokonya Umoja wa Kisovyeti hazina kubwa ya akili na maarifa ya Kijerumani kabla hawajaweza kuwakamata wanasayansi hao. Kwa maneno mengine, vita vya tatu havikupiganwa kwa bunduki – vilipiganwa kwa akili, na Marekani ilishinda kwa sababu ya Operation Paperclip.
images - 2025-07-05T193409.449.jpeg

Lakini mpango huu haukukosa utata na makandokando. Uamuzi wa kuwapa uraia na kazi wanasayansi waliokuwa sehemu ya utawala wa kifashisti wa Nazi kulizua maswali ya kimaadili.
images - 2025-07-05T193441.469.jpeg

Wapo waliokuwa na hatia ya kushiriki majaribio ya kikatili dhidi ya binadamu, hasa katika kambi za mateso. Serikali ya Marekani ilifunika baadhi ya rekodi zao ili kuhalalisha ushirikiano nao.
William_Joseph_(Wild_Bill)_Donovan,_Head_of_the_OSS.jpg

Hii inaonyesha kuwa kuna wakati siasa na maslahi ya kitaifa huweza kuzidi maadili ya kibinadamu. Kambi kama vile Breitenau, Lichtenburg, Auschwitz, Gross-Rosen, Kauen, Vaivara, na nyingine nyingi zilikuwa ni moja ya ofisi za wanasayansi ambao walipata kuhusika na project Paperclip kwa namna moja ama nyingine. Watu kama **Arthur Rudolph, Kurt Debus pamoja na Hubertus Strughold, hawa watu walionekana ni Malaika machoni mwa Office of Strategic Services ambayo kwa sasa inaitwa CIA katika programu ya Paperclip.
images - 2025-07-05T193643.192.jpeg

Hubertus Strughold binafsi alikuwa ni mmoja wa wanasayansi makatili kuwahi kutokea, huyu janja alikuwa akifanya majaribio ya kisayansi kwa wafungwa walioko makambini, janja alikuwa ni mtata sana na hakuwahi kuonesha huruma kwenye makambi kama Auschwitz-Birkenau, Dachau, Neuengamme, Sachsenhausen, pamoja na Ravensbruck.
overview-Harry-S-Truman.jpg

Wafungwa walifanyiwa vitu vya kikatili kupita maelezo, kuwekwa kwenye maji ya baridi ili waweze kuelewa concept za hypothermia pamoja na kuwafungia wafungwa kwenye vyumba ambayo vina presha iliyo chini sana.
images - 2025-07-05T193441.469.jpeg

Kulikuwa hakuna kitu wala jambo ambalo unaweza kuongea mbeleni la Major General William Donovan maarufu kama Wild Bill, huyu kamanda ndo anatambulika kama Father of American Intelligence, Mwamba alikuwa akisaidia na watu wakubwa kama Kanali Donald Putt,Major General Hugh Knerr. Mkurugenzi wa kitengo cha utengenezaji wa Roketi, Major General Holger Toftoy.
images - 2025-07-05T193237.583.jpeg

Na fahamu kuwa ni Major General Toftoy ndio alikuhusika moja kwa moja na kumfuata Wernher von Braun na timu yake kutoka Ujerumani na kumleta Marekani.
images - 2025-07-05T193131.793.jpeg

Hata hivyo, kwa jicho la kihistoria na maendeleo duniani, ni wazi kuwa Operation Paperclip ilikuwa mafanikio makubwa ya kimkakati na moja ya programu bora kuwahi kutokea ndani ya taifa la Marekani.
overview-Harry-S-Truman.jpg

Bila hatua hiyo, huenda Marekani isingekuwa taifa linaloongoza kisayansi na kiteknolojia kama ilivyo leo. Mpango huo ulithibitisha kwamba maarifa ni silaha kubwa zaidi ya vita yoyote, na kwamba taifa linalowekeza katika akili, hujenga msingi wa nguvu za baadaye.
William_Joseph_(Wild_Bill)_Donovan,_Head_of_the_OSS.jpg

Operation Paperclip ilibadili sura ya dunia ya kisayansi, na kuiweka Marekani katika nafasi ya juu katika teknolojia, anga, na ulinzi wa taifa. Leo hii, kila mara tunapotazama satelaiti angani au kutumia teknolojia ya kisasa ya tiba, tunagusa matokeo ya moja kwa moja ya njama hii ya kihistoria.
images - 2025-07-05T193409.449.jpeg

Marekani ilitumia ujasusi na busara ya hali ya juu kuteka akili za adui na kuzigeuza kuwa chimbo cha ushindi – somo kubwa kwa mataifa yanayotaka kuendelea.
images - 2025-07-05T193834.435.jpeg

Hongera kwa jeshi la Morocco chini ya Major General Mohammed Berrid kwa kuunganisha nguvu na kampuni ya Bluebird kutoka Israel na kuanza mpango wa kutengeneza Drones, mmetutoa kimasomaso waafrika kwa ujio wa drones kama WanderB, pamoja na SpyX Kamikaze ambazo zimetengenezwa ndani ya Morocco.

Na hii inafungua soko la utengenezaji wa drones huku Morocco akiwa ameshajipata muda. Wakati huo Jeshi la watoto wa Tata Madiba nao wakicheza muziki sawa na Morocco ambao wao wanatarajika kuwa na drone zinazoitwa Milkor 380 MALE UCAV zifike zaidi ya 16 kufika 2026 yaani mwakani.
images - 2025-07-05T193118.567.jpeg

Huku kwetu kusini mwa jangwa la Sahara, majeshi yetu yanakuja na project za kufyatua tofali, kutengeneza matorori ya kubebea mchanga, kufanya furgimation ili kuua kunguni, mende na mbu majumbani, miradi ambayo kiuhalisia haioneshi tunakua kiteknolojia ama kupiga hatua kisayansi.
images - 2025-07-05T193223.026.jpeg

Badala ya kutafuta wanafunzi wenye uwezo mkubwa kuwaendeleza maarifa ili waje na mawazo bunifu tumeishia kutengeneza bunifu za ajabu kweli. Kuna watoto wetu wapo mashuleni wana mawazo bunifu ya kisayansi ila wanakosa watu wa kuwashika mkono.
images - 2025-07-05T194918.572.jpeg

Kama watanzania tunamani kuona jeshi linalosimamiwa na Jenerali Jacob John Mkunda likiwa mfano bora sio tu ndani ya Tanzania bali hata nchi jirani, kutokana na bunifu zinazoumiza kichwa, ninaamini kuwa kupitia vitengo vyenu ndani ya majeshi kuna watu wanatamani sana kugeuza mawazo yao yawe vitendo.
 
NAAM! Vitu zangu hizi... Mambo za I.G FARBEN FACTORY... Kutoka kutengeneza kombora za kisasa za V-2 hadi kemikali za sumu aina ya Tabun...... hongera mleta mada ..... umenikumbusha hiki kitabu cha operation paperclip....in fact teknolojia ya Wanasayansi wa NAZI walikuwa mbele ya muda
 
NAAM! Vitu zangu hizi... Mambo za I.G FARBEN FACTORY... Kutoka kutengeneza kombora za kisasa za V-2 hadi kemikali za sumu aina ya Tabun...... hongera mleta mada ..... umenikumbusha hiki kitabu cha operation paperclip....in fact teknolojia ya Wanasayansi wa NAZI walikuwa mbele ya muda
Kuna hiki kitabu "Operation Paperclip: The Secret Intelligence Program that Brought Nazi Scientists to America" kimeandikwa na Annie Jacobsen ni cha mwaka 2014 aisee ukisoma utaona kuna jamaa walikuwa na akili personal kabsa
 
Kuna hiki kitabu "Operation Paperclip: The Secret Intelligence Program that Brought Nazi Scientists to America" kimeandikwa na Annie Jacobsen ni cha mwaka 2014 aisee ukisoma utaona kuna jamaa walikuwa na akili personal kabsa
Mdau yaani mimi ninayo hard copy ..sema kimetoka baadhi ya kurasa... it's interesting book ever... yaani mwandishi anakwambia kabisa hii operation ya CIA , mmarekani alitaka teknolojia ya mjerumani isiangukie mikononi mwa Mrusi ambaye alikuwa anaingia Ujerumani kupitia poland.... we
. Ni hatari sana..
 
Mdau yaani mimi ninayo hard copy ..sema kimetoka baadhi ya kurasa... it's interesting book ever... yaani mwandishi anakwambia kabisa hii operation ya CIA , mmarekani alitaka teknolojia ya mjerumani isiangukie mikononi mwa Mrusi ambaye alikuwa anaingia Ujerumani kupitia poland.... we
. Ni hatari sana..
Nadhani MVP alikuwa ni Major General Toftoy ni kama alitazama mbele kwamba ingekuwaje kama Stalin angewachukua hawa wanasayansi.
 
I read a book about this "Operation Paperclip: The Secret Intelligence Program that Brought Nazi Scientists to America" by Annie Jacobsen.

Fascinating.
 
I read a book about this "Operation Paperclip: The Secret Intelligence Program that Brought Nazi Scientists to America" by Annie Jacobsen.

Fascinating.
That's great! Congratulations
 
Na ndio maana hata alivyopewa taarifa kuwa hawa kina Von Braun ni wanyama nadhani aliona ni kama kelele tu
Ila warusi bhana kwa pombe ni kama uji na mgonjwa🤣🤣🤣. Wakati wanaingia Poland na kukomboa kambi ya Auschwitz birkenau walikutana na jumba kwenye kijiji kimoja linalotumiwa kuvundikia wine na kuanza kunywa.... huku wajerumani wakipata muda wa kuharibu baadhi ya ushahidi kwenye kambi hii na kutokomea ili baadhi ya teknolojia zisiangukie kwa hawa red army
 
Ila warusi bhana kwa pombe ni kama uji na mgonjwa🤣🤣🤣. Wakati wanaingia Poland na kukomboa kambi ya Auschwitz birkenau walikutana na jumba kwenye kijiji kimoja linalotumiwa kuvundikia wine na kuanza kunywa.... huku wajerumani wakipata muda wa kuharibu baadhi ya ushahidi kwenye kambi hii na kutokomea ili baadhi ya teknolojia zisiangukie kwa hawa red army
Baridi mkuu kwao pombe ni chai
 
Kama watanzania tunamani kuona jeshi linalosimamiwa na Jenerali Jacob John Mkunda likiwa mfano bora sio tu ndani ya Tanzania bali hata nchi jirani, kutokana na bunifu zinazoumiza kichwa, ninaamini kuwa kupitia vitengo vyenu ndani ya majeshi kuna watu wanatamani sana kugeuza mawazo yao yawe vitendo.
Ndio maana tulipelekewa moto na M23......

1751739829260.png
 
Back
Top Bottom