Operation Sangara Tanga imekuwaje?

Operation Sangara Tanga imekuwaje?

Geza Ulole

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2009
Posts
65,136
Reaction score
91,917
Tunataka kufahamu reaction ya wananchi huko Tanga leo imekuwaje? Je Chadema bado wana momentum ile ya mwanzo? Mnyika njoo utupe jibu humu ndani na tunataka na pícha za umati!
 
Tunataka kufahamu reaction ya wananchi huko Tanga leo imekuwaje? Je Chadema bado wana momentum ile ya mwanzo? Mnyika njoo utupe jibu humu ndani na tunataka na pícha za umati!

Hivi nyie mnaotaka Mnyika awape majibu yaliyoambatana na picha ni akina nani ? Hata hivyo kwa kukusaidia, waandishi wanaofuatilia wapo kama huyu hapa.

Operation Sangara - CHADEMA yaitikisa Tanga.
na Asha Bani, Tanga

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe, amesema Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeshindwa kutawala nchi kutokana na kuingia madarakani kwa kutumia fedha za wizi na kuchangiwa na mafisadi.
Mbowe alitoa kauli hiyo jana kwenye viwanja vya Tengamano, mkoani Tanga wakati wa uzinduzi wa Operesheni Sangara, ambapo aliainisha kuwa nchi inayumba kutokana na kukosa uongozi thabiti.
Alisema utawala wa Rais Kikwete na viongozi wengine ndani ya CCM wamekuwa wababaishaji na kushindwa kuwaletea maendeleo na maisha bora waliyowaahidi wananchi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kutawala nchi.
“Nchi inaelekea kubaya hivi sasa, sipendi kumtaja mtu lakini ni ukweli usiofichika kuwa Rais Kikwete ndiye aliyetufikisha hapa, kwani maisha yanazidi kuwa magumu kadiri siku zinavyokwenda,” alisema Mbowe.
Aliongeza kuwa ili kuondokana na hali mbaya inayolikabili taifa kwa sasa, ni vema katika kipindi cha miezi tisa kabla ya kuingia katika uchaguzi mkuu kufanyike mjadala wa kujadili mustakabali wa nchi.
Alisema Kikwete na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, hawawezi kukwepa hali iliyopo hivi sasa, kwani chama wanachokiongoza ndicho kinachotawala na hali inazidi kuwa mbaya badala ya watu kuona neema na maisha bora waliyoahidiwa.
Aidha, Mbowe alisema kuwa amesikitishwa na kitendo cha Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Said Kalembo, kutoa amri ya kukamatwa kwa Mbunge wa Chama cha Wananchi (CUF), Nuru Awadhi Bafadhili, kutokana na kosa la kusema kuwa rais anacheka.
Alisema hakuna ubishi wala la ajabu kuwa rais anacheka na kushindwa kuwaletea wananchi wa Mkoa wa Tanga na mikoa mingine maendeleo, hivyo kinachotakiwa kwa wananchi ni kuwa na mabadiliko ya kweli katika kuchagua kiongozi atakayefaa ili kuweza kuleta maendeleo ya kweli.
“Kalembo anataka tuje Tanga tujadili Mkoa wa Tanga, tujadili mustakabali wa taifa, watu walivyokuwa maskini bila ya kumtaja Kikwete, ni lazima tumguse guse yeye ndiye aliyechangia hali hii.
“Wananchi ndio wanaompa mshahara, kutembea kwenye ndege kwa kutumia fedha za mlipa kodi, ambaye ni maskini hivyo anatakiwa kuwafanyia kazi wananchi ili kuweza kuwa na maendeleo,” alisema Mbowe.
Aidha, alisema kuwa ufisadi ambao unaitikisa nchi kwa sasa unasababishwa na ufadhili wa mafisadi ndani ya CCM, kwa kuwa chama hicho ndicho kinachowakumbatia.
Alisema hakuna ubishi viongozi wengi wameingia madarakani kwa njia ya wizi wa fedha za Benki Kuu (BoT), na wamechota fedha za Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA), ili kumuweka madarakani Kikwete.
Alisema CHADEMA ni chama cha nguvu ya umma na si chama ambacho kinaingia madarakani kwa njia ya ufisadi kama CCM, hivyo aliwataka wananchi wa mkoa huo bila kujali itikadi ya chama kukiunga mkono ili kuweza kuleta ukombozi wa kweli.
Alisema CCM imekuwa ikitawala kutokana na umaskini unaosababishwa na chama hicho, huku chenyewe kikijinufaisha wakati vyama vya upinzani vikihangaika kutafuta uwezo wa kupambana nacho.
Alibainisha kuwa CHADEMA haikwenda Tanga kugombana na CUF, bali imekwenda kuimarisha upinzani na wananchi wanapaswa wausaidie upinzani ili mageuzi ya kweli yapatikane na kuchagiza maendeleo ya mkoa na nchi yalipotea.
Mbowe, aliwataka wananchi wa Mkoa wa Tanga kuchangia chama hicho kwa njia ya mtandao wa simu, kwa kuandika neno CHADEMA kwenda namba 15710, ambapo alisema uzinduzi huo unafanyika kwa mara ya pili katika mkoa huo.
Naye Mbunge wa Viti Maalumu, Grace Kiwelu, alisema CHADEMA ina jumla ya wabunge 11, lakini katika kila mbunge mmoja katika kuwatetea wananchi anabeba nafasi ya wabunge 20 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Alisema wabunge wa CCM pamoja na idadi kubwa yao bungeni wameshindwa kutetea masilahi ya wananchi pamoja na kuboresha maendeleo kama inavyotakiwa.
“Akina mama wengi wamekuwa na tabia ya kurubuniwa kwa kupewa sabuni na vitambaa vya kichwani ili kuwapa kura wanasiasa wa CCM, hiyo mwaka 2010 mnatakiwa kuikataa, kwa kuwa nyie ndio mnaoteseka kwa kupata huduma mbovu za afya na kutaabika kutafuta maji kwa kutembea mwendo mrefu,” alisema Kiwelu.
Naye Mkurugenzi wa Mambo ya Nje, John Mnyika, amesema kuwa CCM aliyokuwa akiisikia na kuishuhudia zamani si ya leo ambayo imejaa mafisadi wanaotafuna rasilimali za taifa pasi na aibu.
Mwanasiasa huyo alisema kuwa vijana wengi wamegeuzwa makarai na CCM kutokana na kutumiwa wakati wa kipindi cha uchaguzi na pindi uchaguzi unapopita husahauliwa kwa kutupwa bila ya kukumbukwa na matokeo yake hudanganywa kwa kuletewa ajira milioni moja.
Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Shinyanga, Philip Magaduha Shilembi, alisema CCM imekuwa nyoka kutokana na kuwa na roho mbaya ya unyanyasaji wa wazee waliokuwa wafanyakazi wa Jumuia ya Afrika Mashariki kuteseka hadi leo kushindwa kuwalipa mafao yao.
Alisema CCM hata siku moja haiwajali wazee lakini CHADEMA inasema daima wazee mbele na ni hazina ya chama pia.
Naye John Mrema, Mkurugenzi wa Bunge na Halmashauri, alisema kuwa CCM imeiangusha na kuufilisi Mkoa wa Tanga kimaendeleo kutokana na kushindwa kusimamia viwanda, jambo lililosababisha kuanguka kwa viwanda katika mkoa huo.
Alisema kesi za ufisaidi zinafanyika kisanii kutokana na kupelekwa mahakamani vidagaa ambao ni kina Basil Mramba, ambao walikuwa madarakani katika kipindi cha Benjamin Mkapa na kumwacha Mkapa ambaye ni sangara kufikishwa mahakamani hadi leo.
Naye Mwenyekiti wa CHADEMA Kagera Wilfred Lwakatare alisema CCM haiwezi kuondoka madarakani hadi kuwepo kwa chama ambacho kitaonyesha nia ya dhati ya kutaka kuingia madarakani na ni CHADEMA.
“Urais si lele mama, ni lazima kuvimba kifua ni lazima pawepo chama mbadala, chama makini kama CHADEMA, ili kuweza kuunga mkono nguvu ya pamoja na wananchi na kuweza kuingia madarakani, kwa kuwa CCM wanatumia nguvu za kifisaidi kuingia madarakani,” alisema Lwakatare.
CHADEMA iko mkoani Tanga katika Operesheni Sangara ikiwa na lengo la kuwapa uhuru wa kweli wakazi wa mkoa huu na kuwafahamisha wananchi mustakabali wa taifa, maisha ya Watanzania wote.
Operesheni hiyo itakuwa katika mkoa huu kwa wiki moja ikipita kata kwa kata na wilaya kwa wilaya.
Nina imani kuwa pamoja na dua za kuku, Chadema, chama mbadala, itaendelea kuwapo.
 
We are hopeful!
And of course, we will support you CHADEMA!
 
Yes you are right Mbowe
Kikwete(11).jpg

President Jakaya Kikwete.
 
Kikwete alichaguliwa na wananchi kutokana na rekodi ya kucheka na mvuto na si kwa rekodi ya utendaji bali. Kwa hiyo anaendeleza rekodi yake.
 
haya sasa ndio matunda yao na pia Hongera sana kwa ajili ya kazi yenu
 
Mbowe%2Bkuhutubia.JPG


Mkutano wa operation sangara Tanga. Hapo ni mbowe akihutubia maelfu ya wananchi wa jiji hilo. Picha kwa hisani ya Michuzi blog.
 
Umati%2Bna%2Bhelkopta.JPG


Kwa mbali ni helkopta iliyo wapeleka viongozi wa CHADEMA ktk mkutano wao wa uzinduzi wa operation sangara mkoani Tanga jana. Picha kwa hisani ya michuzi blog.
 
Mnyika%2Bkuhutubia.JPG


Mh. Myika akiwahutubia maelfu ya wananchi wa jiji la Tanga jana ktk uzinduzi wa operation sangara mkoani humo. Picha zote kwa hisani ya Michuzi blog.
 
Yes you are right Mbowe
Kikwete%2811%29.jpg

President Jakaya Kikwete.
Ikiwa CHADEMA, CUF na vyama vingine vya upinzani havitajiunga na kuunda Umoja na KAMPENI ya pamoja dhidi ya CCM, Huyu Mh. Kwenye picha hapo juu atapeta 2010 Bili KELELE WALA MIKWARUZO. Akiweza tu kuwaweka sawa CCM wenzake kwa Wapinzani ni KIRARE (lugha ya Tanga) au kwa SADALA (lugha ya Moshi/Arusha) kwa ufasaha ni Mteemko tu.
 
Geza Ulole , Vangi na kundi la aina yako nadhani mna matatizo sana na mnapoteza maana kwenye jamvi hili kwa kasi ya udaku ambao kila mnakuja nao . Sasa unawataka Chadema waweke picha toka kila kata wanayo enda ? Sijaelewa kwa kweli .
 
Back
Top Bottom