Operesheni dhidi ya magari mabovu kuanza Juni 6, 2021

Operesheni dhidi ya magari mabovu kuanza Juni 6, 2021

Trifiki wasio WAAMINIFU hapo kazini alfajiri mpaka usiku mkubwa
 
Hata daladala nyingi tu ni chakavu ila nasikia wamiliki wengi ni wao wenyewe
 
Ushanzi sana huu Wacha Tupaki last week wamengoa Namba na week hii pia wameng'oa tena sasa wacha iwe mbwai tutayapaki tuone na wao walete Mabus yao ya Polisi yabebe Abiria... Gari bovu basi wakamate na serikali kwa Barabara zao Mbovu
 
Mama listaafishe haraka hili zee... Gari Bovu ulijenga barabara nzima?
 
Hizo gari wakizikuta mbovu ndio wanazisimamisha ovyo ovyo hata maeneo yasiyo na parking na kutuongezea misongamano barabarani
 
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameelekeza Makamanda wa Polisi nchini kufanya operesheni dhidi ya magari mabovu ambayo hayapaswi kuwepo barabarani rasmi kesho, ili kuwahakikishia usalama watumiaji wa vyombo vya moto na kuepuka ajali za barabarani.
Watakamata ya walalahoi ili wapate rushwa wataacha ya kwao,
 
Tanzania ni nchi ya ajabu sana wao kila kukicha ni vita na magari badala ya kutengeneza mazingira mazuri wao ni kurudisha nyuma watu gari zinaagizwa za mwaka 2000 huko mtandaoni kwa sababu magari ya miaka ya karibuni kodi haishikiki hamjui kodi ndio tatizo ninyi kila kukicha mnawashambulia raia...gari iwe ya 2014 au 2018 utakagua nini hapo...
 
Sirro katengeneza fursa nyingine kwa askari wa usalama barabarani wapige hela ya "wanyonge"

Mungu wasaidie wanyonge wa Tz
 

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro, ameelekeza Makamanda wa Polisi nchini kufanya operesheni dhidi ya magari mabovu ambayo hayapaswi kuwepo barabarani rasmi kesho, ili kuwahakikishia usalama watumiaji wa vyombo vya moto na kuepuka ajali za barabarani.



ig%20s.jpg


IGP Sirro amesema hayo leo wakati wa kikao kazi cha kufanya tathmini, mafanikio na changamoto ambapo pia ameelekeza kufanyika kwa operesheni ya mwezi mmoja kwa nchi nzima ili kubaini mianya ya uhalifu na wahalifu.

“Nimeelekeza operesheni ya usalama barabarani, kuna makosa ya barabarani yameanza kujitokeza kama mnavyoona ajali iliyotokea Mbeya, Shinyanga, operesheni dhidi ya magari mabovu nayo itaanza kesho, nawaambia ma RTO, wakuu wa matraffik mikoa yote kufanya operesheni dhidi ya magari mabovu ambayo hayatakiwi kuwepo barabarani” amesema IGP Sirro

Awali akitoa tathimini za operesheni ya wiki moja iliyofanyika jijini Dar es Salaam, IGP Sirro amesema wamefanikiwa kukamata silaha za moto pamoja na wahalifu waliokuwa wakijihusisha katika matukio mbalimbali ya kihalifu.

“Wananchi wa Dar es Salaam wametoa ushirikiano mkubwa sana kwa jeshi la polisi tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa sana, silaha nyingi zimekamatwa wahalifu wengi wamekamatwa, nimeongea na wenyeviti wa mtaa na watendaji Kata wote wa Dar es Salam, tumekuwa na mafanikio makubwa nafikiri wana Dar es Salaam wameona, leo tunahitimisha operesheni lakini tunaanza operesheni nyingine tena ya mwezi mzima na ni nchi nzima” amesema IGP Sirro

Hata hivyo IGP Sirro ameendelea kuwaasa wahalifu waliotoka kutokujihusisha na uhalifu wowote kwani Jeshi la Polisi halitosita kuwachuulia hatua za kisheria mara watapojikita katika kufanya uhalifu.
Kule Zanzibar nako wameanza kupita na vipasa sauti magari mabovu yaondolewe barabarani kumbe mpaka amri itoke jamuhuri ya muungano na wao ndio wajitie kupiga marufuku., mama samia naye ameitelekeza Zanzibar.
 
Huu Mchezo ni deal tu haman kingine maana Daladala ndio warengwa wakuu... kudakishana tu then unaachiwa kisha unashikwa na mwingine basi hadi ndio mwezi uishe ni taabu tu... au yaani Ujambazi ukishikiwa bango uishe na wao wanahamia kukamata magari there is something fishy is goin on... Maaaa
 
Back
Top Bottom