Operesheni Haki: Freeman Mbowe kuhamasisha umuhimu wa Katiba jijini Dar es Salaam

Operesheni Haki: Freeman Mbowe kuhamasisha umuhimu wa Katiba jijini Dar es Salaam

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Ile Operesheni iliyotikisa nchi kwa kuhamasisha wananchi juu ya umuhimu wa katiba mpya na Tume huru ya Uchaguzi, ambayo ishatikisa na kuamsha watu wa mikoa 24, sasa imeingia kwenye mkoa wa DSM huku wakazi wake wakisubiri kwa hamu bila kuchoka.

Mwamba Mwenyewe Freeman Mbowe ataongoza mashambulizi bila kuchoka.

Chadema_kaskazini_on_Instagram:_“Ratiba”%22_.jpg
 
🤣🤣🤣🤣

Haki katika katiba tu ya NCHI?

Ile Katiba ya CHADEMA ambayo ilikuwa inasema "MWENYEKITI atakuwa na vipindi viwili vya jumla ya miaka 10" ilibadilishwa kwa RIDHIO LA WANACHADEMA WOTE bila ya manung'uniko ya chinichini eeee?🤣🤣

Msipopewa kibali na POLISI mtafanya mikutano yenu ya hadhara?

Au mnataka yale yaliyotokea "Temeke" yajirudie?

Duuuh.

Rest easy JPM, amen!

#KaziIendelee
 
Duuuh!

Rest easy JPM ,amen!

#KaziIendelee
Kwanini nyie wana CCM hampendi siasa za majukwaani au ni uwezo mdogo?
 
Chadema ndio vinara wa kufanya siasa za majukwani bila kuleta vurugu wala kukurukakara. Polisi goeni ushirikiano wananchi wa vyama mbali mbali wanaoofanya shughuli zao halali za kisiasa.
 
Vyama vingine kama Chauma, TLP, ACT, NCCR na CCM wakianza siasa za majukwaani na mikutano kama hii kula siku mnafikiri kazi itafanyika saa ngapi?
 
Hivi kuna kipengele kwenye katiba kilichozuia mikutano ili kazi ifanyike? Miaka mitano yule dhalimu mwendazake alizuia mikutano na maandamano kwa kisingizio kazi ifanyike lakini hakuna kazi yoyote iliyofanyika.

Ajira nchini hakuna, Wafanyakazi, Wafanyabishara na Wakulima wote wanalia na uchumi uliokuwa unakuwa kwa 7% Sasa umeanguka hadi 4.8% . Acheni kutafuta visingizio visivyo na kichwa wala miguu ili kuzuia upatikanaji wa Katiba mpya?

Hivyo vyama ulivyovitaja vina uwezo wa kufanya mikutano nchini? Vina wafuasi? Hebu viitishe mikutano tuone kama vitapata hata watu 20.
Vyama vingine kama Chauma, TLP, ACT, NCCR na CCM wakianza siasa za majukwaani na mikutano kama hii kula siku mnafikiri kazi itafanyika saa ngapi?
 
Silly thinking and reasoning

Bahati nzuri au mbaya hiyo lugha siifahamu, ila kama umenitukana basi mwenyewe.

Kutumia lugha ya kigeni kwenye mjadala inapotumika lugha ya kwenu au yako nao ni utumwa mkubwa sana wa fikra kuendelea kutukuza visivyokuhusu.
 
Hivi kuna kipengele kwenye katiba kilichozuia mikutano ili kazi ifanyike? Miaka mitano yule dhalimu mwendazake alizuia mikutano na maandamano kwa kisingizio kazi ifanyike lakini hakuna kazi yoyote iliyofanyika. Ajira nchini hakuna, Wafanyakazi, Wafanyabishara na Wakulima wote wanalia na uchumi uliokuwa unakuwa kwa 7% Sasa umeanguka hadi 4.8% . Acheni kutafuta visingizio visivyo na kichwa wala miguu ili kuzuia upatikanaji wa Katiba mpya? Hivyo vyama ulivyovitaja vina uwezo wa kufanya mikutano nchini? Vina wafuasi? Hebu viitishe mikutano tuone kama vitapata hata watu 20.
Ni vyema unakubali uchumi ulikuwa unakua kwq 7% then ukaanguka, ulipokuwa unakua kwa 7% ilikuwa ikitumika katiba hiyohiyo isiyofaa na kuanguka to 4.8% zipo sababu nyingi ikiwemo Covid 19 na nchi kuingia kwenye mtambuka wa kiuchumi ilipoamua kuhamishia nguvu kwenye ujenzi wa miundombinu ya kimkakati.

Hivyo vyama vingine unavyovidharau ndivyo ambavyo kila uchaguzi mnaungana na kutengeneza ukawa lakini leo unatukana wafuasi wao (ukosefu wa shukrani), hao hao wanachama wao wasiodhidi 20 nao wakiamua kuwa busy na mikutano na makongamano tayari ni nguvu kazi hiyo inapoteza muda. CCM nayo yenye wanachama zaidi ya 10m nchi nzima ikiamua mikutano na makongamano kila kukicha unafikiri nani ataenda shamba kulima.

Kupitia katiba hiyo hiyo kila siku mnashiriki chaguzi, mkishindwa katiba mbovu, mkishinda basi chama chenu kinakuwa kinakubarika.
 
Demokrasia siyo uchumi peke yake wewe! Ni pamoja na UHURU na HAKI ya Watanzania kuchagua Wabunge, Madiwani na Rais wamtakaye uhuru wa kuikosoa Serikali bila kuwa na woga na pia uhuru wa vyombo vya habari.

Jifunze maana nzima ya neno demokrasi. Hata hiyo 7% ya uchumi kukua mbona ajira hakuna graduates wanasaga lami, miaka sita sasa hakuna nyongeza ya mishahara na tunaambiwa eti tuna uchumi wa kati!!!!

Uchumi ulikuwa mbovu hata kabla ya COVID-19 ACHA UONGO! COVID ambayo ni ya mwaka jana lakini kwa miaka minne 2015 to 2019 uchumi ulikuwa HOVYO TU! Hata kama si COVID bado ulikuwa HOVYO TU!
Ni vyema unakubali uchumi ulikuwa unakua kwq 7% then ukaanguka, ulipokuwa unakua kwa 7% ilikuwa ikitumika katiba hiyohiyo isiyofaa na kuanguka to 4.8% zipo sababu nyingi ikiwemo Covid 19 na nchi kuingia kwenye mtambuka wa kiuchumi ilipoamua kuhamishia nguvu kwenye ujenzi wa miundombinu ya kimkakati.

Hivyo vyama vingine unavyovidharau ndivyo ambavyo kila uchaguzi mnaungana na kutengeneza ukawa lakini leo unatukana wafuasi wao (ukosefu wa shukrani), hao hao wanachama wao wasiodhidi 20 nao wakiamua kuwa busy na mikutano na makongamano tayari ni nguvu kazi hiyo inapoteza muda. CCM nayo yenye wanachama zaidi ya 10m nchi nzima ikiamua mikutano na makongamano kila kukicha unafikiri nani ataenda shamba kulima.

Kupitia katiba hiyo hiyo kila siku mnashiriki chaguzi, mkishindwa katiba mbovu, mkishinda basi chama chenu kinakuwa kinakubarika.
 
Ila huyu mwamba atakuja kukumhukwa kwa vizazi na vizazi kwa kuongoza mapambano na kukataa kununuliwa na ccm kama walivyo viongozi wa vyama vingine
Siku ukijua FM, ZZK, PM nk wote mwajili wao ni mmoja unaweza kuzimia mara saba, ngoja niishie hapa tuwaachie wenyewe.
 
Siwezi kwenda nikaishia jela

Atangulie mbowe na viongozi wenzake tuone kweli kama wanajiamini
 
Katiba Mpya mali ya watanzania, tunataka kuitoa nchi toka kwenye kikundi kidogo cha watu waliojimilikisha irudi kwetu sote.
 
Kwanini mbowe kwenye hizo porojo zake hazungumzii kabsa wale covid 19?
 
Back
Top Bottom