Operesheni Haki yaiharibu CCM nchi nzima, wachambuzi wa siasa waifananisha na Operesheni Sangara ya 2012

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Taarifa ya sasa duniani na hasa baada ya ccm kurudia makosa yale yale ya miaka yote , ya kukubali kushindwa hoja na kuamua kulitumia Jeshi la polisi kudhibiti Chadema badala ya viongozi wake wa chama akiwemo Shaka Hamdu ambaye ni Katibu wa uenezi na itikadi , zinadokeza kwamba hii Operesheni haki inayoendelea japo ni ya vikao vya ndani imeivuruga kabisa ccm na serikali yake kuliko hata operesheni Sangara ile ya miaka ya 2012 iliyokuwa inafanyika hadharani.




"Ubaya" uliogundulika wa operesheni haki hata kama ni vikao vya ndani ni uwepo wa CHADEMA DIGITAL , ambayo mpaka sasa inasemekana 70% ya vijana wanaojitambua na wasomi wanaitumia , imefanya kazi ya kampeni za operesheni haki ziwe nyepesi mno , IKUMBUKWE KWAMBA VIJANA WASOMI WENGI WA TANZANIA HAWAKUAJIRIWA KWA MIAKA 6 SASA , hii imekuwa ushahidi wa wazi kwa vijana wengi kuthibitisha kushindwa kwa CCM katika kuboresha maisha yao


Habari hii ya moto wa Operesheni haki ndio iliyosababisha shida yote hii kwenye kogamano la Katiba mpya huko Mwanza .

Itaendelea...
 
Ni muda muafaka wa kuendelea kuwakong'ota maharamia kwenzi za kidigitali Hadi watakapokubali kurejea kwenye utii wa sheria zetu na katiba ya taifa hili na upatikanaji wa katiba mpya.
 
Ni muda muafaka wa kuendelea kuwakong'ota maharamia kwenzi za kidigitali Hadi watakapokubali kurejea kwenye utii wa sheria zetu na katiba ya taifa hili na upatikanaji wa katiba mpya.
Maofisa mipango wa Chadema ni hatari mno ! ccm hoi bin taaban, imebaki polisi.
 
Utopolo!
 
CHADEMA ni taasisi inayoongozwa na viongozi wapuuzi na mediocres sana! Ajenda za mlipuko kama hizi za Katiba na Tozo za miamala haziwezi kujenga CHADEMA!

Pangeni namna ya kuijenga CHADEMA kama taasisi imara kiuongozi,kiuchumi then ndo mnaweza kupambana na CCM.
Katika hali ya utulivu CHADEMA haina uongozi imara kama taasisi, haina Ajenda za muda mrefu na ni taasisi dhaifu sana kiuchumi!

Hii ndo sababu CHADEMA inawekeza sana kwenye siasa za matukio kwani watu wajinga wengi ( zaidi ya asilimia 70) wanapenda sana matukio!

Tatizo ambalo viongozi wengi wa CHADEMA kwa sababu ya ujinga wao hawalijui ni kwamba wajinga wengi ( zaidi ya asilimia 70) wanaopenda matukio huwa hawadumu na hayo matukio muda mrefu !

Watashabikia issues za Katiba na Tozo za miamala ndani ya wiki 2_then wanakosa nayo appetite na kutaka tena matukio mapya! CHADEMA mtachukua miongo mingi sana kujifunza na siasa zenu kuleta tija kwa Taifa!!!!
 
Wenzio ndipo wanapoegemea,wanzo mwisho. Wewe unayo akili hivyo watafute wenye akili yako pale mtaa wakijani.uichukue ili urejee humu.
 
Ccm imeleta tija gani aisee,au ndo ya kuendelea kuwafanya watanzania kuwa wajinga
 
Unapoona hizo picha hapo juu za enzi za dr slaa alafu ukifananisha na utopolo huu wa chadema wa siku hizi unabaki kusikitika tu
 
Unapoona hizo picha hapo juu za enzi za dr slaa alafu ukifananisha na utopolo huu wa chadema wa siku hizi unabaki kusikitika tu
Sasa Dr Slaa anashindwaje kukiokoa chama chake kipya cha ccm ?
 
Siasa ya Vyama vingi tunahitaji kuwa na mikakati na ubunifu kila uchao. CCM kimezeeka na sasa kinapaswa kukubali kuachia ngazi
Nakubalina nawe lakini tatizo hakuna mbadala! Hawa CHADEMA wa kiongozi wa tangu mwaka 47? NO! Hawa wanaojua uzinzi na ulaji wa ruzuku? BIla ofisi kila siku ni kutafuna pesa!
Mwaka huu hakuna ruzuku ya maana ndo wanahamasisha ujenzi wa ofisi kwa kujitolea. Au nayo tuingize kwenye muamala wa wana CHADEMA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…