Operesheni maalum ya Putin

Operesheni maalum ya Putin

Operesheni maalum" ya Putin haijaenda kulingana na mpango. Kile kilichopaswa kuchukua siku au wiki kadhaa tayari imechukua miezi kadhaa.

Kremlin inaonekana kabisa haikuchukulia upinzani wa Ukraine kwa uzito mkubwa.

Magharibi kuunga mkono Kyiv na wimbi la vikwazo vya kimataifa ambavyo Urusi ingekabiliana nayo. Kaputin ameingia choo cha kike, Achana na Nchi za Magharibi wanachheza na akili za Kaputini. Wana akili sana hao wajamaa.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] unateseka ukiwa wapi mwenzetu.
 
kwahiyo boss unataka kumfananisha hussein na vladimir... uko ni kumtukana vladimir wazi wazi
Ni kweli hawafanani ila pia mazingira ya vita hayafanani. Hii vita inapiganwa kwa akili kubwa kuliko zana za kivita. Wakati wa vita kati ya Marekani na Iraq mataifa mengi ya ulaya yalitangaza wazi wazi kuiunga mkono Marekani, kwa sababu taifa la Iraq halikuwa tishio kwao kama lilivyo taifa la Russia. Sasa elewa kwa mbinu ambazo mataifa ya magharibi yametumia kuisapoti Ukrane kwa sasa pamoja na kwamba hawajionyeshi moja kwa moja ila zimeifanya Russia kupata wakati mgumu na ndio maana Russia amepigana kwa muda mrefu tofauti na alivyotegemea kwamba atapiga Ukrane kwa wiki moja tu. Mpaka sasa putin ana majuto ya ndani kwa ndani yanayomfanya ajutie kuanzisha hii operation.
 
lakini pia unatakiwa kujua kupindua nchi na kuweka uongozi wengine kwa njia ya mapinduz sio swala la miezi miwili au mitatu.
 
Unaweza kuta anaesema hivyo mpaka Sasa anakula kwa mama yake bira kutoa msaada wowote hapo home, hajayajua malengo ya huyo anaemzungumzia lakin anasema malengo yake hayajatimia ukiimuuliza yapi hayo malengo yake anayoyajua yeye hayataji.
Malengo ya Putin tangu awali yalikuwa wazi.
-kuiangusha haraka Serikali ya mchekeshaji zele na kupachika vibaraka wake. Yote hayo alilenga yafanyike ndani yamuda mfupi.
-kuharibu silaha zote za Ukraine na kuifanya ibaki haina tishio LA silaha toka magharibi(deweaponise).
-kuyachukua majimbo yoote ya magharibi mwa Ukraine ya Donbas na Lugansk kuwa majimbo ya Russia.
Ukitazama ilivyo mpaka sasa amekwama pakubwa.
*Silaha nzito zinaendelea kutiririka Ukraine toka magharibi.
*wanajeshi wa urusi hawafanyi vizuri sana kwenye uwanja wa vita kama alivyotarajia mzee Putin.
*majimbo alotamani kuyameza na kuyafanya himaya zake kwa kadiri vita inavyoendelea kuwenda akaanza kuyatapika.
*ubabe alokuwa nao mwanzo unazidi kupungua. Kwasasa anaonekana mnyenyekevu na mpole sana kuliko awali. Mwanzoni alitishia kutoa kipigo kwa kila taifa litakalojiingiza kumsaidia zele,hatujaona akifanya. Morali ya wanajeshi wake imeshuka sana kwenye mapambano.
*anaelekea kuchoshwa na vita alivyovianzisha mwenyewe. Inasemwa vikwazo vimeanza kuuma. Ameamuru serikali itangaze bajeti yake upande wa mapato tu,siyo matumizi.

Sent from my TECNO CA7 using JamiiForums mobile app
 
Operesheni maalum" ya Putin haijaenda kulingana na mpango. Kile kilichopaswa kuchukua siku au wiki kadhaa tayari imechukua miezi kadhaa.

Kremlin inaonekana kabisa haikuchukulia upinzani wa Ukraine kwa uzito mkubwa.

Magharibi kuunga mkono Kyiv na wimbi la vikwazo vya kimataifa ambavyo Urusi ingekabiliana nayo. Kaputin ameingia choo cha kike, Achana na Nchi za Magharibi wanachheza na akili za Kaputini. Wana akili sana hao wajamaa.
The power of IQ
 
Back
Top Bottom