Operesheni okoa Yanga sehemu ya pili - 2

moodykabwe

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2015
Posts
625
Reaction score
602
TUENDELEE...

KARIGO ndiye alifanya FITNA za kumuondoa Kocha wa Viungo Msauzi Afrika RIEDOH, alimpigia debe yule Kocha wa viungo wa Taifa Stars ambaye Yanga walimpa ajira ya Muda kabla ya Kocha mwenyewe kukata ajira ya kudumu.

KARIGO ndiye aliyekuwa mpika majungu Mkuu ya kuwaondoa Daktari Mngazija na Kocha Msaidizi Juma Mwambusi na alifanikiwa na ndipo akafanikiwa kuwaingiza 'Watu wake' Dkt Muganda na Nizar Khalfan kama Kocha Msaidizi ambao wote ana maslahi nao hata kama watakataa ukweli unajulikana.

Taarifa za uhakika kabisa ni kwamba, katika tukio la Kuvunja kwa benchi la Ufundi, KARIGO alikuwa amewatega pia Meneja wa timu Hafidh Saleh na mtunza vifaa Mpogolo na Afisa Usalama wa Klabu, lakini amefanikiwa kumpatia Afisa Usalama, Lengo hapa ni kwamba uweke watu wake ambao watakuwa na utii kwake ili afanikishe MPANGO wake ambao hata GSM sijui kama wanaujua.

Kuna Mengi ambayo KARIGO ameyapanga ili kuuvuruga uongozi wa MSOLLA, na kama uongzozi usingesimama imara tayari tulishakuwa tumepoteza Mpambanaji wetu HASSAN BUMBULI ambaye ni Fitna za KARIGO na NUGAZ zilisababisha akafungiwa. Ahsante Uongozi kwa kusimama IMARA, ingawa na wao wanajishaua kwamba walikuwa wakimsaidia.

KARIGO ni rafiki wa SENZO (Mahauari wa Yanga) kwa kutumia urafiki huo KARIGO alitaka kumtumia SENZO awashauri Kamati ya Utendaji wawatimue waajiriwa wa Klabu, mpango wake ilikuwa kumuondoa SIMON PATRICK NA HASSAN BUMBULI. Alifanikiwa kwa SlMON lakini SENZO alishtuka mapema akataa kuingia mkenge kwa BUMBULI kwani SENZO ANAAMINI BUMBULI pekee ndio mwenye Vinasaba halisi vya YANGA wengine ni fake.

Kutokana na SENZO kumgundua kwa sasa KARIGO kwa siri anashirikiana na upande mwingine kumuandalia ZENGWE SENZO aondoke nchini au Wanachama wamchukie Senzo kwa matokeo mabaya ya Timu.

GSM hiki ni kirusi mmeleta bila kujua.Nimeeleza machache tu, lakini kimsingi huyu KARIGO ni kirusi kibaya Sana ndani ya Yanga, yawezekana GSM hawajui hilo, lakini ukweli ni kwamba yeye ana mpango wake wa kuuangusha uongozi wa MSOLLA kupitia nafasi hiyo aliyopewa na GSM.

Anawapiga vita watu aliowakuta Klabuni na kwenye Timu waondoke ili alete watu wake, lakini anasuka mipango michafu ili uongozi utukanwe na Wanachama wafanye Mapinduzi na tayari ana Kamati yake ya Muda mfukoni ambayo anaiwasilisha kwa GSM kwamba itasaidia baada ya vurumai kutokea.

ITAENDELEA...

#SisiNiMashahidiTu
#hallaywsmm[emoji1241]

Pia soma: Operation OKOA YANGA Sehemu ya kwanza 1
 
Yanga endeleeni kupambana mpaka timu ivurugike kabisa.
 
Nyie aliewaita nyani hakukosea mnaleta habari za kusadikika,hii sera ya serikali kuwa kila mtu ajue kusoma na kuandika imeleta shida!!!
Ni bora wengine mngebaki tu na ujinga wenu,baada ya kujua kusoma na kuandika, mmeamua kuandika chochote tu hata kama ni ujinga, ili watu wajue nanyi mpo!!! Next time huu uchafu wako upeleke uko kwenye magroup yenu uko na sio kutuletea hapa na kutuchafulia jukwaa letu!!
 
Wewe mnafiq ambaye unataka kuchonganisha team ya Yanga. Tunajua unataka sana upate nafasi yanga. Umefikiria utoke vipi ndo ukaamua kuja na Utumbo huu. WEWE NDIYE KIRUS KIBAYA NDANI YA YANGA. HAYA UNAYALETA HUKU KULETA TAHARUKI NA MIGOGORO KWENYE CLUB. LENGO LAKO UPATE USEMAJI KWENYE CLUB.UPATE NAFASI. TUNAKUJUA NA YANGA HATUDANGANYIKI NA NINYI NJAA KALI.
 
Kwakweli binafsi nafurahi hawa ndugu zetu japo imechukua sana muda lakini mwishoni wameweza kutambua mchawi ni nani. Viongozi wao wamecheza na akili zao kwa muda mrefu sana.

Kinachoniogopesha hawa wenzetu hawanaga ustaarabu wetu, wanaweza hata kukatana mapanga hali ikiwa mbaya.

Inabidi tuwaombee sana jemeni 😁
 
Kwahiyo Karigo na Nugaz wanawazuia wakina Nchimbi na Farid wasifunge magoli??
 
Ukuzoea kula nyama ya mtu,huwezi kuacha.
Mlianza na TFF ,mkaja kamati ya ligi,Mara
waamuzi,mkabebwa vya kutosha na waamuzi maana wanajua mko hovyo na kweli mkaharibu,Mkamgeukia mwalimu mkatitmua yeye na benchi la ufundi.Kama vile haitoshi kwa sasa mmemgeukia kipa wenu.Mara Mwamnyeto,na Sarpong.
Kwa vile mmezoea,sasa mmeanza kutafutana wenyewe ndani ya uongozi,na ninajua hatimae mtafukuza GSM.

Maana kuna watu mapoyoyo humu ndio yanaishika yanga.Wanatamba watachangishana kuendesha club.Sijui wanafikiri kuendesha club ya mpira ni kama kuendesha genge la kuuza nyanya!

Na mtaendelea kupigwa tu,nami nasema mpigwe tu maana hamna namna
 
Uandishi mrefu unachosha kusoma

Anyway yanga Bora Ni ile ya nguvu ya buku
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…