Operesheni ya kuondoa Spika za matangazo Kariakoo Yaiva!

bless on

JF-Expert Member
Joined
May 22, 2026
Posts
1,213
Reaction score
2,938
Jiji la Dar es Salaam limeanza rasmi operesheni ya kuondoa spika za matangazo ya biashara zinazotajwa kusababisha kelele katika maeneo mbalimbali ya biashara, hususan Kariakoo, kwa lengo la kurejesha utulivu na kuboresha mazingira ya wafanyabiashara pamoja na wanunuzi. Hatua hiyo inalenga kudhibiti matumizi holela ya vipaza sauti na spika kubwa vinavyotumika kutangaza bidhaa katika maduka na maeneo ya wazi.

Kwa miaka mingi, wafanyabiashara wengi wa Kariakoo na masoko mengine wamekuwa wakitumia spika na matangazo yaliyorekodiwa kuvutia wateja, hali iliyosababisha ongezeko kubwa la kelele zinazowakera wanunuzi, wapita njia na hata wafanyabiashara wenzao. Kutokana na hali hiyo, kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kuhusu usumbufu unaotokana na matumizi ya vifaa hivyo.

Hatua ya kuondolewa kwa spika hizo imekuja takribani wiki tatu baada ya gazeti la "Mwananchi" kuchapisha mfululizo wa makala maalumu zilizoangazia changamoto ya kelele za matangazo ya biashara katika masoko ya Dar es Salaam, hususan Kariakoo, ambapo spika zimekuwa sehemu ya kawaida ya ushindani wa kibiashara.

Wakati huo huo, operesheni hiyo inaendana na juhudi za Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambalo hivi karibuni lilizindua mikakati mipya ya kupambana na uchafuzi wa kelele katika miji mikubwa nchini. Serikali inaeleza kuwa kelele kupita kiasi ni miongoni mwa changamoto za kimazingira zinazohitaji kudhibitiwa kwa manufaa ya afya na ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa za Jiji la Dar es Salaam, operesheni hiyo ilianza Juni 2, 2026 katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo ikiwemo Msimbazi, Narung’ombe na Aggrey, maeneo ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya spika za matangazo ya biashara.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema Serikali imepiga marufuku matumizi ya spika katika maduka yote ya Kariakoo na kuwataka wafanyabiashara kutumia mabango ya kawaida kutangaza bidhaa zao. Mpogolo amesema kuruhusu kila mfanyabiashara kuweka spika kungeifanya Kariakoo kupoteza hadhi yake ya soko na kugeuka eneo la kelele zisizoisha.

“Haya, wewe unayeuza sumu ya mende unaweka spika, sumu ya panya unaweka, unayeuza jeans au fulana unaweka; halitakuwa soko tena bali kelele. Kwa hili Serikali tumesema hapana, lazima tuziondoe spika kwenye eneo la Kariakoo,” amesema.
FB_IMG_1780809254437.jpg
 
Bado na pale mbagala, kila baada na nusu mita kuna kipaaza sauti, huyu ana uza hiki yule kingine mwingine nae hivyo hivyo .
Kwa mtu ambaye hujazoea kelele za namna hio pale huwenda jehanamu ina afadhali.
 
Soko la Kariakoo kutoa huduma Masaa 24!
 
iji la Dar es Salaam limeanza rasmi operesheni ya kuondoa spika za matangazo ya biashara zinazotajwa kusababisha kelele katika maeneo mbalimbali ya biashara, hususan Kariakoo, kwa lengo la kurejesha utulivu na kuboresha mazingira ya wafanyabiashara pamoja na wanunuzi. Hatua hiyo inalenga kudhibiti matumizi holela ya vipaza sauti na spika kubwa vinavyotumika kutangaza bidhaa katika maduka na maeneo ya wazi.
Hili litakuja jambo moja zuri Sana lililowahi kufanywa na serikali ya Halmashauri ya Jiji.

Aisee zile kelele Hazina tija yoyote kwani Mteja hafuati Yale makeleke na kila mtu kabandika la kwake mezani ukienda Kariakoo hadi unarudi kichwa kinakuuma
 
Kwa hili naipongeza sana serikali, kwa maana hiyo hii inaenda mpaka kwa hawa wahubiri wa mitaani?
 
Niliishasema humu, NEMC ni ovyo Sana. Mpaka gazeti na watu ndo waambie cha kufanya. Je raia wanaokaa karibu na msikiti au kanisa linalopiga Kelly Sana wanasaidieaje? NEMC ndo dysfunctional organization

NEMC walipaswa kukataza, kuzuia hivyo vipaza sauti nchi nzima sio Kariakoo pekee
 
iji la Dar es Salaam limeanza rasmi operesheni ya kuondoa spika za matangazo ya biashara zinazotajwa kusababisha kelele katika maeneo mbalimbali ya biashara, hususan Kariakoo, kwa lengo la kurejesha utulivu na kuboresha mazingira ya wafanyabiashara pamoja na wanunuzi. Hatua hiyo inalenga kudhibiti matumizi holela ya vipaza sauti na spika kubwa vinavyotumika kutangaza bidhaa katika maduka na maeneo ya wazi.

Kwa miaka mingi, wafanyabiashara wengi wa Kariakoo na masoko mengine wamekuwa wakitumia spika na matangazo yaliyorekodiwa kuvutia wateja, hali iliyosababisha ongezeko kubwa la kelele zinazowakera wanunuzi, wapita njia na hata wafanyabiashara wenzao. Kutokana na hali hiyo, kumekuwa na malalamiko ya mara kwa mara kuhusu usumbufu unaotokana na matumizi ya vifaa hivyo.

Hatua ya kuondolewa kwa spika hizo imekuja takribani wiki tatu baada ya gazeti la "Mwananchi" kuchapisha mfululizo wa makala maalumu zilizoangazia changamoto ya kelele za matangazo ya biashara katika masoko ya Dar es Salaam, hususan Kariakoo, ambapo spika zimekuwa sehemu ya kawaida ya ushindani wa kibiashara.

Wakati huo huo, operesheni hiyo inaendana na juhudi za Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC), ambalo hivi karibuni lilizindua mikakati mipya ya kupambana na uchafuzi wa kelele katika miji mikubwa nchini. Serikali inaeleza kuwa kelele kupita kiasi ni miongoni mwa changamoto za kimazingira zinazohitaji kudhibitiwa kwa manufaa ya afya na ustawi wa wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa za Jiji la Dar es Salaam, operesheni hiyo ilianza Juni 2, 2026 katika mitaa mbalimbali ya Kariakoo ikiwemo Msimbazi, Narung’ombe na Aggrey, maeneo ambayo yamekuwa yakitajwa kuwa na kiwango kikubwa cha matumizi ya spika za matangazo ya biashara.

Akizungumza kuhusu hatua hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Edward Mpogolo, amesema Serikali imepiga marufuku matumizi ya spika katika maduka yote ya Kariakoo na kuwataka wafanyabiashara kutumia mabango ya kawaida kutangaza bidhaa zao. Mpogolo amesema kuruhusu kila mfanyabiashara kuweka spika kungeifanya Kariakoo kupoteza hadhi yake ya soko na kugeuka eneo la kelele zisizoisha.

“Haya, wewe unayeuza sumu ya mende unaweka spika, sumu ya panya unaweka, unayeuza jeans au fulana unaweka; halitakuwa soko tena bali kelele. Kwa hili Serikali tumesema hapana, lazima tuziondoe spika kwenye eneo la Kariakoo,” amesema.
Hapa tuwapigie makofi mwengi serikali ya CCM japo hatua zimechukuliwa kwa kuchelewa sana.
 
Nyie mnataka Dj mark afe na njaa, ni kifo cha hovyo kwa shujaa wa vibanda umiza
 
Back
Top Bottom