MC RAS PAROKO
JF-Expert Member
- Feb 14, 2013
- 623
- 606
Habari za wakati huu mpendwa msomaji. nimeweza kutembelea wilaya ya serengeti iliyo mkoa wa Mara kaskazini mwa Tanzania na katika matembezi yangu hayo kuna baadhi ya mambo nimeyaona ambayo yanaweza kuwasaidia wale wenye mitaji wanaohitaji kufanya biashara.
1. Kufungua supermarket-Eneo la Mugumu ambako nimefanya kautafiti haka nimegundua kuna supermarket moja tu ambayo ni ndogo na wala haikidhi mahitaji ya wakaazi wa eneo hilo. kwani ukiweza kufungua supermarket ambayo itakua kubwa yenye hadhi karibu sawa na Nakumatt utakua tayari umemaliza soko la hivi vi min supermarket ambavyo havina hata jokofu. Kwa upande wa masoko naweza kusema yapo sababu kuna mahoteli ya nyota tano ambayo yana camp ndani ya hifadhi ya serengeti na mji wa karibu ni mugumu baadhi yazo ni SAYARI,BUSHTOPS,KURIA HILLS N.K nimejaribu kufuatilia hadi kwenye mahoteli haya ambako nimepata majibu ya kwamba wao wananunua vitu vyao Arusha na vinasafirisha hadi hotelini kwa grarama ya 1.5 hadi 2ml kwa trip moja. hivyo ukiweza kufungua supermarket eneo hili tayari utajipatia wateja wa kudumu.
2.Kufungua kiwanda kidogo cha mikate-katika sekta hii pia nimeona kuna shida sababu wakaazi wa eneo hili wanategemea mikate kutoka arusha ambako kuna umbali zaidi ya km 400 au inayotoka mwanza na Musoma, hivyo ukiweza kufungua kajikiwanda kako maeneo haya tayari utakua kwenye njia sahihih ya kuaga umaskini.
kwa sasa ni hayo tu nikipata muda nitaendelea na mengine..AHSANTENI