Opportunity ya bishara wilaya ya Serengeti

MC RAS PAROKO

JF-Expert Member
Joined
Feb 14, 2013
Posts
623
Reaction score
606
Habari za wakati huu mpendwa msomaji. nimeweza kutembelea wilaya ya serengeti iliyo mkoa wa Mara kaskazini mwa Tanzania na katika matembezi yangu hayo kuna baadhi ya mambo nimeyaona ambayo yanaweza kuwasaidia wale wenye mitaji wanaohitaji kufanya biashara.
1. Kufungua supermarket-Eneo la Mugumu ambako nimefanya kautafiti haka nimegundua kuna supermarket moja tu ambayo ni ndogo na wala haikidhi mahitaji ya wakaazi wa eneo hilo. kwani ukiweza kufungua supermarket ambayo itakua kubwa yenye hadhi karibu sawa na Nakumatt utakua tayari umemaliza soko la hivi vi min supermarket ambavyo havina hata jokofu. Kwa upande wa masoko naweza kusema yapo sababu kuna mahoteli ya nyota tano ambayo yana camp ndani ya hifadhi ya serengeti na mji wa karibu ni mugumu baadhi yazo ni SAYARI,BUSHTOPS,KURIA HILLS N.K nimejaribu kufuatilia hadi kwenye mahoteli haya ambako nimepata majibu ya kwamba wao wananunua vitu vyao Arusha na vinasafirisha hadi hotelini kwa grarama ya 1.5 hadi 2ml kwa trip moja. hivyo ukiweza kufungua supermarket eneo hili tayari utajipatia wateja wa kudumu.

2.Kufungua kiwanda kidogo cha mikate-katika sekta hii pia nimeona kuna shida sababu wakaazi wa eneo hili wanategemea mikate kutoka arusha ambako kuna umbali zaidi ya km 400 au inayotoka mwanza na Musoma, hivyo ukiweza kufungua kajikiwanda kako maeneo haya tayari utakua kwenye njia sahihih ya kuaga umaskini.
kwa sasa ni hayo tu nikipata muda nitaendelea na mengine..AHSANTENI
 
Wewe unaishi Mugumu? Make huko ndo mitaa yangu, na ni kweli kuna furusa nyingi sana, huko hivyo Changamkia, mimi mwenyewe kuna program moja niko nayo huko
 
Hawa ndio watu tunawahitaji TZ/ JF na Social media nyingine.

Watu waozungumzia fursa .

Big up saana.

Najua nisipofanyia kazi mm hii fursa , nitamshirik Rafiki , jirani na hata ndugu kuendeleza gurudumu la kujikwamua kwenye umaskini.
 
Wewe unaishi Mugumu? Make huko ndo mitaa yangu, na ni kweli kuna furusa nyingi sana, huko hivyo Changamkia, mimi mwenyewe kuna program moja niko nayo huko

Mkuu kama uko mugumu, utakuwa msaada sana kwangu....
mkuu nataka nianzishe program ndogo ya kuzalisha sabuni hpo wilayani.
Naomba mwongozo wako...
 
Nachepuka kidogo kwenye topic,hiv kiwanda kidogo cha mikate kina cost around shilling ngapi?
 
Hapana kiongozi siishi maeneo hayo ila ni kati ya sehemu ambazo nimefanikiwa kuzitembelea na nikaona kuna fursa nyingi za biashara na bado watu hawajaamka kuzichangamkia. Anyway hata tarehe 20 mwezi huu nitakua mugumu @Chasha Poultry Farm
 
Vile vile katika maeneo haya ukiweza kufanya kilimo cha mboga mboga unaeza kupiga hatua sababu mahoteli mengi upande huu yanatumia ndege kufanya usafirishaji wa mboga mboga kutoka arusha. baadhi ya mboga nizo ni kama cauliflower,cellery,baby marrow,broccol,chines cabbage,cucumber,egg plant,french beans,fresh asparugus,garlic,yellow peper,green pepper,red pepper etc
 
chasha mugumu mitaa yako ni ipi mi niko mitaa ambayo jamaa anazungumzia ya supermarket nahamu sana ya kukuona ndugu maana uwa napenda sana post zako kama hutojari nijuze nakuonaje mkubwa nitashukuru sana nipate japo nanafasi ya kuiona hiyo program yako ya hapa mugumu.

Mkuu makazi yangu ni Arusha, Ila hata Mugumu huwa natia timu make ni Home, ila 98% ya kazi zangu na life yangu ni Arusha, Mugumu nilikuwepo last year mwezi wa 10. nitafute kwenye 0767-69-1071
 
Back
Top Bottom