- Waanze kugomea ruzuku kwanza kama kweli they are for real!
Respect.
FMEs!
Bora ulivyosema kuwa si lazima hao uliowataja katika mfano wako. Kwani nafikiri pia watajitokeza watu kusema kuwa hao hawakipendi Chama fulani na wana msimamo wa kuchukia wadau fulani wa uchaguzi. Hili tatizo nafikiri jibu lake ni kubakia katika misingi mikuu- nayo ni Tume Huru na kufuata sheria za uchaguzi kwa mujibu wa Katiba. Usihukumu watu kabla ya kufanya kazi yao kwa hisia tu. Hivyo ni sahihi Rais (Siyo Mwenyekiti wa CCM kama unavyotaka tuamini) kwa mujibu wa Katiba kama akiwa ni (institution) kuendelea kuchagua tume, Mwenyekiti na Wajumbe wa Tume hiyo kwa mujibu wa katiba. CUF na Lipumba wao hawana mpya. Wanataka Tume ibadilishwe ili waingizwe Wajumbe ambao tayari wana msimamo wa kulinda na kuyatetea maslahi ya Chama fulani (CUF), Hapo huo Uhuru wa Tume uko wapi. CUF wanatuyumbisha Bwana. Nasikitika kuwa mfano wako wa DRC haukidhi haja hapa. DRC ilikuwa katika crisis. Tz haiko katika mazingira hayo.Pakacha,
Wapinzani kule DRC walikuwa na malalamiko kama haya katika uchagizi mkuu wa 2006, serikali ikaona hebu imchague mtu ambaye ataaminiwa na wadau wote, akamteua Askofu Apolinary Malumalu kuwa kiongozi wa tume, na wacongo wakafanya angalau kitu kinaitwa uchaguzi,sisemi na tz wafanye kama congo lakini uwepo mchakato wa kuteua tume itakayoridhiwa na vyama vyote na wadau wengine wa uchaguzi, wajumbe wachekechwe na watoke katika makundi ¨"fair" katika jamii,kama taasisi za haki za binaadamu mfano akina mama Kidjo Bisimba, Prof. Haroub Othman etc namna kama hiyo(si lazima wawe hao,lkn wanaweza kuwa kama hao).
Naona unajizonga Ndugu yangu. Kama ni ridhaa ni ya wananchi wa Tanzania na siyo ya Vyama vya siasa. Na wananchi wa Tanzania hawawezi wote kukaa kufanya mchakato na kusema wanateua Tume. Hivyo Mwakilishi wao (U-rais) unafanya hivyo. Huo mchakato unaoutaka wewe ni upi? Seif amewakoroga kule Zanzibar. na matokeo yake ZEC siyo ZEC na kamwe haiwezi kufanya kazi zake kwa mujibu wa Katiba.Pakacha,
lakini uwepo mchakato wa kuteua tume itakayoridhiwa na vyama vyote na wadau wengine wa uchaguzi, wajumbe wachekechwe na watoke katika makundi ¨"fair"
Pakacha,
Tume itakayoridhiwa na vyama vya siasa(wafuasi wao ni wananchi) na wadau wengine wa uchaguzi(wataowakilisha makundi mengine ya kijamii), hapa wananchi watakuwa wameshirikishwa. Ninachokusudia hapa ni kuwa kabla ya kuingia katika gemu, washiriki wote wakubaliane mwamuzi yupi ni muafaka ili mwisho wa mchezo pasiwepo malalamiko ya upendeleo.
tusikatae kuwa tokea mfumo wa vyama vngi urejee tume imekuwa ikichangia matatizo mengi yanayoepukika katika kuendesha zoezi la uchaguzi.