ozone layer
JF-Expert Member
- Oct 27, 2021
- 471
- 1,935
Fbme bank ilikua dili zao kupitia madalali wa kizungu..Nakubaliana nawe mkuu, ndiomana ilifikia kipindi rate MG alikuwa akimpa vijembe JK lakini kutokana na uwelewa mdogo wa watu walikuwa walimchukulia ni kama chuki za kisiasa tu kumbe Kuna makubwa katika kulea utoroshaji wa rasilimali za nchi.
Si tumeambiwa task force zimefutwa Mambo yaende kwa taratibu na sheria!!!?Wakasema kwakuwa tayari lipo katika mikono ya kikosi maalumu (task force) kinachoshughulikia haya masuala basi wao wanashindwa kuweka mkono.
Task Force za kodi, kuna maeneo huwezi kufuta TF kwa usalama wa nchi. Hata hii issue ndio maana kaa la moto, lina macho mengi.Si tumeambiwa task force zimefutwa Mambo yaende kwa taratibu na sheria!!!?
RIP Magufuri, japo alichofeli ni kuua demokrasia kwa kutulea bunge la ovyo na kutesa watu.Hakika mkuu kuna muda mtu unatamani ungekuwa na mamlaka makubwa ili urekebishe mambo lakini ndio hivyo. Tunaletewa mpaka yaliyowazi sasa ya DP World ni jinsi gani tunaonekana watanzania tumelala katika ulimwengu huu.
Iliyo futwa ni TRA task force, lakini Police task force bado inaendelea na op kama kawaidaSi tumeambiwa task force zimefutwa Mambo yaende kwa taratibu na sheria!!!?
Acha upumbavu,haya ndio matokeo ya wengi humu kutokujua how to read to understand, hii issue ni mwendelezo wa uchunguzi ule wa to smuggling cigarettes from Zimbabwe to south africa, then malipo Dubai, watu weusi ni shida dunia hii maana ni corrupted, greedy na washenzi,(only Botswana kuna uafadhali wa hili na corruption its almost ni zero)uchaguzi umeingiaje hapa. tunza heshima yako
Ila Bongo haitajwi kabisa au sisi ni kunguru?Gold Mafia: Huduma ya utakatishaji fedha – Uchunguzi Uliofanywa na Al Jazeera
Waandishi wa habari undercover wanajifanya kuwa majambazi wenye dola bilioni moja za pesa chafu zinazohitaji kusafishwa. Wanapata upenyo kwa wanachama wa Afrika wa Gold Mafia na kurekodi mikutano ya siri na viongozi wa uhalifu. Balozi Mkubwa wa Afrika anatoa huduma ya kutakatisha pesa chafu...www.jamiiforums.com
Sent using Jamii Forums mobile app
Aiseeeeee !!!Haya ni matokeo ya ule uchunguzi wa Aljazeera kuhusu kutakatisha pesa haramu kupitia biashara ya haramu na ni Syndicate kubwa yenye mtandao mkubwa wenye pesa ndefu na ikiwahusisha vigogo wa Kisiasa
Kesi ishamalizwa?Hatari sana, ila kesi ndogo sana...
tunaomba picha plzHuyu ni Mmiliki wa Sharjah Trading (nitaeleza kwa undani kuhusu hii kampuni).
Miaka michache iliyopita wakati wa utawala wa Magufuli alikamatwa, akafunguliwa kesi ya utakatishaji fedha akafanya plea bargaining, ikakubaliwa - akalipa faini na kuachiwa.
Ramla alikamatwa juma lililopita, siku ya Alhamisi akawa anashikiliwa Cetral Police Mwanza.
Anamiliki Bureau De Change pale Mwanza ila anafanya biashara zake hadi mkoa wa Geita.
Hadi anakamatwa, alikuwa na pesa nyingi za kigeni ambazo hakuwa amezibadilisha na alikuwa anazitumia kununua madini aina ya dhahabu katika ‘black market’ kisha yeye analipwa 2-4% katika kila manunuzi.
Katika kuhangaika kwake ili ajinasue akawasiliana na Waziri na Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini. Wao kwa kuanzia wakamkatalia. Wakasema kwakuwa tayari lipo katika mikono ya kikosi maalumu (task force) kinachoshughulikia haya masuala basi wao wanashindwa kuweka mkono.
Wakajaribu kumwona RC Shigella awasaidie. Akakataa ila Jumatatu ya wiki hii akawapigia, akawaambia anaweza kuwasaidia lakini ‘lazima wafanye jambo’ (PCCB fuatilieni, maafisa wenu wana taarifa).
Wakawa wanahaha waweze kumwona kijana mmoja mtoto wa Kigogo mkubwa ambaye walielekezwa na Waziri mmoja kuwa wafanye hivyo, akiwaaminisha ndio pekee anayeweza kuwasaidia ndugu yao akaachiwa ila kwa kijana huyo wakagonga mwamba.
Sasa, leo vyanzo vyangu vinaonyesha Ramla kapewa shitaka la kununua dhahabu bila kufuata utaratibu. Kashapelekwa Geita na ana simu anawasiliana na watu wake.
Kuna kila dalili hela imetolewa katika mchakato huu.
Mumewe amegoma kutoa hela zake akisema zitumike za mtuhumiwa mwenyewe na katoa msimamo kuwa hata akifungwa yeye hajali. Watoto ndio wanahaha kumtoa mama yao.
Swali: Kina nani wako nyuma ya mama huyu?