Orijino Komedi kujikita kwenye kilimo

Orijino Komedi kujikita kwenye kilimo

Freeland

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2012
Posts
14,481
Reaction score
10,227

Kundi maarufu la vichekesho nchini la Olijino Komedi sasa limeamua kuingia kwa nguvu katika biashara ya kilimo.

Wasanii hao wamekabidhiwa Matrekta saba aina ya Sonalika DI 50 RX na Kampuni ya Quality Extended Enterprise ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilimo.

Baada ya kuyanunua, Orijino Komedi walikabidhiwa Mtrekta hayo yenye thamani ya Sh milioni 170 katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Quality Extended Enterprise yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar.

Kiongozi wa Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki' alisema kuwa hatua hiyo ni moja ya malengo yao ya kimaendelo waliyokuwa wamejiwekea hapo hawali wakati walipokuwa wakianzisha kundi hilo.

Alisema malengo yao yalikuwa ni kuhakikisha wanafikiwa zaidi kimaisha lakini pia wanakuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine hapa nchini.

"Tulianzisha kundi hili siyo kwa ajili ya buradani pekee lakini pia kwa ajili ya maendeleo yetu binafsi hivyo baada ya kupata matrekta haya tutajikita rasimi katika kilimo.

"Tayari tumesha mashamba mkoani Mbeya na Iringa lakini pia tupo katika mazungumzo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuf Makamba ili aweze kutupatia shamba jingine huko kwao mkoani Tanga ili tuweze kutimiza ndoto zetu," alisema Siki.

Kundi la Olijino Komedi linaundwa na wasaanii saba ambao ni Seki, Mpoki, Joti, Masanja, Wakuvanga, Macklegan pamoja na Vengu.

Source:
Salehe Jembe Blog
 
Kiukweli kati ya wasanii wanaojitahidi sana kwa Bongo kwenye Tasnia ya uigizaji basi hawa Vijana ni moto sana. Na pamoja na mafanikio yao ila hawana zile mambo za skendo sana na kutokea kwenye magazeti sana.
Mimi kiukweli nawapa hongera, wanafanya yaliyo bora
 
Hongera zao kwa kuona fulsa zingine (uzuri wa kilimo cha kisasa tz nzima yaweza kulishwa na watu wa5 tu)
 
Halafu hawa jamaa wako effected sana na Comedy.. hebu waone hapo juu wanavyocheka! Yaani kuwatazama tu ni burudani..!!!

BACK TANGANYIKA
 
hongera zao sana ila wangekamata na fursa kama mwenzao mkandamizaji wakawa wachungaji ingekua safi kabisa maana kwa mkwanja hakuna anaenusa hata nusu
 
Hongereni sana Original Comedy mnaonyesha kua sanaa nikazi kama kazi zingine kwa maendeleo na kujituma kwenu katika maisha yakila siku. Hope wengine watajifunza kupitia kwenu
 
management is the key for success of everything
seki is highly creative and innovative
awajaendekeza uzinzi na skendo ni watu wa kazi jifunzen kwao
 
Watu walishaanza kuamini kuwa "Education is the only to success", mara akazaliwa Bakhresa, sasa ukweli unajulikana.
 
Nawakubali sana hawa jamaa hata km elimu yao ndogo but kimafanikio hata sifikii robo, huwa nawatzama sana saa 3usiku tbc, big up orijinal comedy.
 
watu kama hawawezi kutusumbua na michango ya india. safi.
 
Safi sana vijana wa kisasa na wa kuigwa miaka michache ijayo mtakua wakina Mengi wengine.

Nafikiri Masanja ndio direct motivation towards thIs success na vyema na nyie mmechukua hatua kumfuata wengine. Kibongobongo wangekalia kumpiga majungu na wivu lakini nyie mmeamua kufuata his footprint. Big-up
 
Kundi maarufu la vichekesho nchini la Olijino Komedi sasa limeamua kuingia kwa nguvu katika biashara ya kilimo.

Wasanii hao wamekabidhiwa Matrekta saba aina ya Sonalika DI 50 RX na Kampuni ya Quality Extended Enterprise ya jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kilimo.

Baada ya kuyanunua, Orijino Komedi walikabidhiwa Mtrekta hayo yenye thamani ya Sh milioni 170 katika hafla iliyofanyika makao makuu ya Quality Extended Enterprise yaliyopo barabara ya Nyerere jijini Dar.

Kiongozi wa Orijino Komedi, Sekioni David ‘Seki’ alisema kuwa hatua hiyo ni moja ya malengo yao ya kimaendelo waliyokuwa wamejiwekea hapo hawali wakati walipokuwa wakianzisha kundi hilo.

Alisema malengo yao yalikuwa ni kuhakikisha wanafikiwa zaidi kimaisha lakini pia wanakuwa mfano wa kuigwa kwa vijana wengine hapa nchini.

“Tulianzisha kundi hili siyo kwa ajili ya buradani pekee lakini pia kwa ajili ya maendeleo yetu binafsi hivyo baada ya kupata matrekta haya tutajikita rasimi katika kilimo.

“Tayari tumesha mashamba mkoani Mbeya na Iringa lakini pia tupo katika mazungumzo na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mzee Yusuf Makamba ili aweze kutupatia shamba jingine huko kwao mkoani Tanga ili tuweze kutimiza ndoto zetu,” alisema Siki.

Kundi la Olijino Komedi linaundwa na wasaanii saba ambao ni Seki, Mpoki, Joti, Masanja, Wakuvanga, Macklegan pamoja na Vengu.

Source:
Salehe Jembe Blog

Wana mbegu?mimi ni wakala maarufu wa mbegu nchini
 
Haya ndo tunayoyataka sisi. Siyo Ali Kiba kutwa kushinda bondeni Jangwani na masela tu wana happy na zao Iringa.
 
Back
Top Bottom