Orodha mpya ya mafisadi hii hapa!

Orodha mpya ya mafisadi hii hapa!

MAJINA YA MAFISADI HAYA HAPA? Soma hadi mwisho utayapata.

Nimefikiria sana na sasa nimegundua kwanini sisi ni maskini wa kutupwa na tuna rasilimali za kutosha sana.Waswahili husema hakuna awali mbovu na alie juu mngoje chini.Sina uhakika kama hizi methali zina maan au la, au kila wakati halihuwa hivyo au wakati mwingine inakuwa tofauti. nafurahi kutaja mafisadi maana ndo chanzo cha umaskini wa nchi yetu.nina Imani sote tunapenda kuwajua,name nitawataja bila woga.fikra chanya huleta mawazo chanya na fikra hasi huleta mawazo hasi.huwezi kufika Moro toka Dar kama hujaanza kuondoka taratibu.

Kwa kawaida yangu napenda sana kulinganisha, kwa kitasha , tunasema Comperative analysis. Ni kwa kulinganisha tu utaweza kuelewa uko wapi na unapanda juu au unaanguka chini! Ni kwa kulinganisha tu utapata hasira ya maendeleo , ni kwa kulinganisha na aliekuzidi ndo utajua kama we ni kapuku au kabwela! Sasa naangalia umaskini wa nchi yangu ambao umeniathiri kwa kiwango kikubwa sana kiakili manake nimekulia kwenye umaskini na nazeeka kwenye umaskini! Hapana hapa kwenye kuzeeka kwenye umaskini ndo nina tabu napo manake nimekataa kata kata, sikubali kuwa masikini , napambana, napambana sana. Wajua , ili uwe na akili lazima usome ndugu zangu, si lazima usome vyote darasani!kila mtu hapa duniani analo la kukuambia na ukafunguka! Napenda kulinganisha kitu kikubwa na kidogo, nchi kubwa ilianza kuwa ndogo, maendeleo madogo yaligeuka kuwa maendeleo makubwa, siku moja Tanzania itakuwa zaidi ya Marekani,kama huamini basi nawe ni miongoni mwa watu wenye mawazo hasi na kawaida watu hawa hata kitu kidogo hushangaa kusikia kimewezekana.

Niliposema hakuna awali mbovu namaanisha kuna baadhi ya wabongo wenye bahati sana na ulaji wa keki ya taifa ambao waliwahi kuliona jua, na baadhi yao walifaidi maisha wakati wa ukoloni na wakaenda shule kwa pesa ya jasho la walalahoi wa bongo na bahati nzuri sana hawakufanya makosa, wakajichukulia vitu vya ‘wajinga ndio waliwao' na baada ya wao kuhitimu wakaanza kupeleka watoto wao huko nje walikoenda wao. Na kwa bahati ya mtende sasa wamesema haya nyie walalahoi someni hapa hapa kwenu na ni kwa mkopo! Mtalipa baada ya kupata ajira ambazo ziko hewani! Nilijiuliza sana kwanini sisi tulipe wao walisoma bure? Halafu tunamlipa nani na pesa ni ya kodi za watanzania wavuja jasho ? Swali zuri sana ni kwamba wao wamemlipa nani? Bahati nzuri tunafurahi sasa wanaanza kuchoka nasi tunaona mwanga wa angalau kupata nafuu , ila wapi bwana, jamaa wameanza kuwaweka watoto wao kwenye nafasi nzuri nzuri! High table!Hii dunia imejaa watu wasiomuogopa mungu!Yani unaiba kwa miaka nenda rudi unasahau kama utakufa na kuviacha vyote ulivyoiba na ataekuja vishika labda hutampenda? Nani anajua kuwa baba yake na Alexander The Great , kijana aliyejiita Lord of Asia , na kutawala sehemu kubwa , akitokea katika himaya ndogo ndogo tu ya Macedonia, alizikwa na vitu vyake miaka elfu mbili iliyopia? Hivi wajua kuwa miaka ya karibuni wamefukua kaburi lake huyu jamaa, anaitwa King Philips , jamaa wamechukua mali zake alizozikwa nazo!ni dhahabu tupu kila kitu!wameweka kwenye museum!

Hoja yangu kubwa leo ni sababu za umaskini wa bongo, ya kwanza na kubwa kuliko zote ni ubinafsi uliopitiliza na uliojificha wa baadhi ya waheshimiwa wa juu wa nchi, baadhi ya waheshimiwa wa juu wa nchi kupinga maendeleo ya nchi ili kutotaka kupoteza statuses zao katika jamii, tuna katabia ka kizamani sana , ka tunataka kuwa juu sisi tu kila siku, baada ya sisi kuchoka na kuzeeka sasa tunataka kuweka watoto wetu kwenye nyadhifa mbalimbali hata kama hawana karisma ya uongozi, baadhi ya waheshimiwa kuiba mali ya umma kwa miaka nenda rudi, baadhi ya waheshimiwa kujawa na mawazo mgando, baadhi ya watendaji kuendekeza rushwa iliyoota mizizi, udini uliojificha sana, upendeleo wa chini kwa chini sana katika maeneo ya elimu na ajira, ukabila uliojificha sana, misamaha ya kodi kwa miaka nenda rudi, udhibiti usioridhisha wa mapato na matumizi ya nchi, jitihada zisizoridhisha za kukuza uchumi , kutofufua viwanda, kilimo duni cha waheshimiwa walalahoi wa vijijini, kutokuwa na wivu wa maendeleo , kutoiga mazuri ya nchi zilizoendelea, kuoneana aibu kwa wezi na wazembe wa mali za umma, kuwapa vyeo vikubwa watu wasio na sifa, vihiyo , labda watu wasiostahili kuongoza inji! na mwisho kabisa kutotaja mafisadi wanaoifilisi nchi hii maskini sana yenye rasilimali nyingi ajabu .sijui kama tunajua wote kuwa ni aibu sana kwa bongo kuwa nchi maskini! Natamani kila mmoja wetu ataje orodha yake ya mafisadi wote wa bongo na WAUWAWE maana kutokana na wizi wao wa mali ya umma si na wao wanaua maskini kwa magonjwa na njaa na ujinga?! Naamini katiba mpya itakuwa mwarobaini wa umaskini wa bongo na labda itatenganisha mihimili mitatu ya nchi , ili kuwe na checks and balance! Ili tuendelee tunahitaji kuwekeza sana kwenye sayansi na technology.Orodha yangu iko chini!

Kimazabe mazabe tu mimi mtoto wa kapuku au kabwela ambae hana jina hapo bongo nami nimejikuta niko hapa Marekani ambako naishi kwasasa, nina kama miezi sita tu , sijaja huku kwa zile nafasi za baadhi ya wanaojiita vigogo wanawapa kwa upendeleo watoto wao waliofeli NECTA! nimekuja kwa mishe zangu tu!Ila kiukweli nasikia raha sana , kila kitu huku ni serious, kila mtu yuko bize na kazi yake na mambo yake,kila mtu ana ‘head phone' maana yake hataki ‘noise' kutoka nje! Nashangaa huku hakuna kushughulika na mwingine maana muda ni wa thamani sana , ukihangaika na mambo ya wengine ya kwako yatakushinda! Mimi ni mweusi kama giza la ‘usiku saba put together' au tuseme mweusi kama lami au chungu na niko katikati ya watu weupe ambao hakuna hata mmoja anaenitupia jicho hata sekunde moja popote ninapopita! Niko huru na mambo yangu huku ugenini! Kumbe ndo maana hatuendelei manake badala ya kupiga kazi , kujenga taifa , huwa tuna katabia ka kuwa bize kukagua wengine na kupayuka na kuwachongea wengine kwa bosi huku ‘viporo' vyetu hatujamaliza , tumezoea ‘zimamoto' na kufanya kazi kwa kukariri na mazoea , hatutaki mawazo mapya! Tunapenda kuishi kwa majungu kila kukicha , na bahati mbaya sana tulio na nafasi hizi za kidunia hatutaki na wengine wapate , na tuliobahatika vinafasi basi wimbo ni ule ule wa waheshimiwa wa kiafrika ambao katika nafasi tofauti walizonazo basi hawako tayari kamwe na wenzao wapate ukiranja!

Huku Marekani ni systems tu zinafanya kazi , nakaa kwangu nacheki kwenye website ‘bus la umma' litapita mda gani hapo nje kwangu na kweli mda huo nafika stendi bus linapita napanda na natumia kadi yenye nauli ya mwezi na ndani ya mabasi mara nyingi hakuna kondakta wa kukagua tickets kwa maana hiyo hakuna kuchelewa kwa basi kwenda linakoenda na ajabu kila mtu ana ticket (kadi) halali mfukoni hata kama hakuna ukaguzi wa nani kalipa nauli nani hajalipa!, hapa tena nakumbuka kuwa kumbe labda hatuendelei kwa kuwa hatuna utamaduni wa kupenda kulipa! Tunakwepa kodi , tunakwepa nauli kwa kujifanya ‘staff' , tunaficha mizigo ili tusiilipie! Tunakwepa kodi ya mabilioni ya kuendeleza nchi kwa nyaraka feki zinazoonesha mizigo tofauti na tuliyoagiza , baadhi yetu tunapenda kuomba na kupokea rushwa kama desturi sasa, tusipopewa rushwa hakuna kutoa huduma! halafu hivi ni nani alieanzisha mambo ya misamaha ya kodi Tanzania? Natamani kumjua mtu huyo! Hili ndo linaleta umaskini hapa bongo pamoja na ufisadi na ubinafsi! Mtu ni bilionea badala ya kumkamua eti tunamsamehe kodi? Huku Marekani na Ulaya anaepata pesa nyingi ndo analipa kodi kubwa! Bongo ni tofauti nadhani! Ili tuendelee ni lazima wote tulipe kodi na tulipe kutoka na kipato , hii ni opposite hapa bongo nadhani!

Huku Marekani na huko Ulaya nashangazwa na treni zinazopita mjini na nyuma yake magari yanapita! yaani reli na lami ziko sehemu moja! treni ikipita magari yanasubiri then nayo yanapita humo humo! najiuliza hivi sisi wabongo tuna shida gani? Hivi hatuwezi kuiga hata hili? Hivi hatuhitaji mapinduzi ya kifikra kweli? Hawa jamaa weupe wana tofauti gani na sisi zaidi ya rangi tu?najiuliza ni lini tutafika hapa! Hivi waheshimiwa wanaokuja Ulaya hawaoni haya maendeleo ? hivi hawapendi na kwao kukawa hivi one day? Hivi shida ya umaskini wetu ninini? Je tumeifahamu? Je tumeifanyia kazi? Au hatujali kwa kuwa baadhi yetu tunapata hongo na rushwa za kutosha kututunza sisi , watoto , wajukuu na vitukuu vyetu? Hatujali kwakuwa sisi ni wabinafsi wa kutupwa tunakula na kusaza na kulala pazuri ,labda wengine baadhi yetu tunalala pembeni ya bahari? Upepo mwanana ukipuliza? Sauti za mawimbi ya bahari zikitubembeleza tu na si kelele za watoto wadogo masikini wanaosikia njaa na kiu ya siku tatu! Tuna shida gani akaunti zetu zikisoma tarakimu ishirini na zaidi , tunaita vijisenti , huku bila aibu tukijua kabisa kuwa hayo mapesa ni ya ushuru unaotokana na majasho ya mababu na mabibi zetu walalahoi wa kule Ngerengere bush? Je kweli tunajua vumbi linalotimka huko vijijini? Je tunajua giza lilivyo huko vijijini usiku? Je tunajua maji wanayokunywa watu huko vijijini? Je sisi ni bora sana kuliko wao? Na je labda hatutakufa! Au tutakapokufa tutabeba mali zetu na kwenda nazo huko tuendako! Labda wengine tutaenda Jehannam! Na hatufikirii na hatujali! Who cares! Hivi wanapokuja wageni toka nje ya nchi hatuoni aibu na ‘haya' kwa umaskini huu na rasilimali zote tulizonazo?

Je tunatumia fursa za biashara vizuri mfano tunatumiaje bandari zetu kuvutia watumiaji kama Rwanda , Burundi, Congo, Zambia, Malawi , Uganda nk? Je kama kodi zetu ni kubwa kuliko za bandari za nchi jirani , kwanini hatushushi kodi zetu tupate wateja wengi tupige hela na kunyanyua uchumi wetu? Halafu hivi hawa wanyama pori tumebarikiwa tunawajali kweli?

Hivi tunapenda na wajukuu zetu waje waone Simba kama sisi tulivyolindiwa na mababu zetu? Hivi tunakubalije majangili wawamalize wanyamapori kila kukicha wanaua tu na askari wapo kibao makambini hatuwapeleki porini kulinda wanyama na mtu ana cheo kapewa dhamana na serikali kuwalinda! Big up sana kwa wamasai kwa kula ng'ombe tu na si wanyama pori maana tusingeona hata nyati mmoja , kule Ngorongoro jamaa wanaishi pamoja na hawa wanyama pori vizuri tu ila sisi tunatoka mjini na kwenda kuua wanyama pori kama tembo na twiga! Sasa najiuliza huyu waziri mhusika ana kazi gani wanyama wanaisha kwa kasi ya ajabu kule maporini!kila siku tunaona kwenye TV majangili wamekamatwa na nyara za serikali , wanapita wapi kuua wanyama? Maana yake askari wanyamapori hawatoshi sasa si waongezwe? Shida ni nini jamani mbona sielewi nchi yetu ina shida gani? Mpaka wanyama pori waishe ndo tujaze mabuku kuelezea sababu za kuisha wanyama porini? Hivi unajua raha ya kutembelea mbugani? Niulize mimi ambae TWIGA alikuja karibu sana na gari letu na Simba alipita mbele ya gari! Nilitamani nitoke nimshike sharubu! Ni raha ya ajabu!

Halafu sijui kama tunajiuliza kuwa katika miaka mia au mia mbili , nchi yetu itakuwa na mashimo na makorongo na mavumbi ya kiasi gani na huku kukiwa hakuna madini tena , AU HATUJALI KWAKUWA NASI TUTAKUWA VUMBI TU! swali kubwa la kujiuliza ni je nchi yetu na sisi wananchi tunafaidikaje na madini yetu kwasasa? Jibu ni lile lile ‘ubinafsi' tu ambao hauna faida , maana nasikia eti mtu mmoja anapata bilioni moja ya hongo na nchi inapoteza bilioni elfu kumi! Hivi ni nani anahusika kusaini mikataba hii ambayo haina faida kwa nchi! Je wakati wa kusaini hiyo mikataba ni vigezo gani vinatumika? Je kuna maslahi ya taifa hapo? Najiuliza sana mtu ana akili timamu eti amenunua maeneo na mapori nchi nzima na hayaendelezwi maana hahitaji kitu huko porini yeye yuko mjini anakula bata, anahitaji sehemu ndogo tu la ktanda kulala ! na nasikia ana magorofa kibao na magari hayana idadi, sasa mali zote za nini ndugu yangu unakufa unaviacha na uliiba pesa za umma kujipatia utajiri huu wenye laana!umewaweka watu wengi kwenye njaa , magonjwa , ujinga na umaskini , umesababisha wengi wafe kwa kukosa dawa hospitali nawe umeiba pesa zao!pesa ambazo zingejenga hospitali, lami, masoko, mashule, mabomba ya maji na madaraja wananchi wakafaidika!
Sasa najiuliza ni mfumo gani wa maisha tunaoufuata sasa , ubepari au ujamaa? je kwa wale ambao tumejaaliwa vijisenti na nafasi je tunapenda mfumo huu wa kundi la 'wachache' kuendelea kuwa juu na utajiri wa kutisha huku makapuku na makabwela kwa mabilioni wakifa na njaa na magonjwa na kujaa ujinga uliopitiliza? kumbe tunapenda mfumo huu wa nchi kuwa maskini uendelee ili tuendelee kuwa juu na makoti ,vitambi na statuses zetu? Je ni kweli bila kujua au kwa makusudi hatutaki utajiri na maendeleo ya nchi kwa sababu statuses zetu zinataathirika! tunapenda kuwa juu juu juu zaidi siku zote! Kumbe baadhi yetu tunapenda kutukuzwa na kulambwa miguu SIKU ZOTE huku nchi yetu ikiwa nyuma sana kimaendeleo na hatuoni aibu hata chembe! Kwa mawazo yangu , labda siko sahihi , au nimechanganyikiwa nahitaji mapumziko pale Lutindi au Mirembe hospital , eti nawaza kuwa sasa kwakuwa fursa za elimu ya juu na ajira ni chache vijana wote , labda tumegeukia kutembeza madawa ya kulevya kila mahali duniani , tuko bize na uzinzi, umalaya, ubakaji , kuvuta bangi na kuimba bongofleva music!

Mimi sijasikia kijana anataka kuwa ‘mkulima' manake hana ‘role model' ambae ni mkulima! Kuna watu wengine wa maana kabisa kwenye jamii wamegeukia kupeleka kuku kwa waganga wa kienyeji , na nini tunaona? Wanawanajisi watoto wao , mama zao , dada zao na binamu zao eti wapate utajiri? Sababu fursa za kiuchumi na ajira labda zimebanwa ili wachache tu wawe na uwezo ili tuwatukuze , kuwaimbia na kuwapigia makofi siku zote! kwa maana wakimaliza muda wao , watafuata watoto wao!Ninajaribu kuchunguza namna wenzetu wanatukuza , wanawekeza na kulea watoto? Watoto wao huku wanasoma vizuri , ‘wanakaa' kwenye mabasi, wanatembezwa mjini na vitoroli ., wanakula vizuri na zaidi ya yote wote wanacheza sana! Karibu kila mtoto huku ana vile ‘vitu vyao'wanaweka miguuni kuteleza barabarani, wengine wana vibaiskeli vya kuteleza kwenye lami! Watoto wako very happy! Hapa napo najiambia , kumbe ukitaka nchi iwe na maendeleo mahali pa kuanzia ni kwa kuwekeza kwa watoto , watoto wawe wasomi na wenye furaha, watoto wote nchi nzima! Si kubagua na kutoa fursa kwa watoto wachache wa Upanga na Oysterbay! Maana kila ofisi nchi nzima inahitaji mtu alielewa na kusoma vizuri!hao wa Upanga hawatakaa Lupembe na Mtakuja!

Kiukweli nashangaa sana huku Marekani , kila kitu nashangaa tu , nashangaa watu hawahitaji kununua magari kabisa na wana uwezo wa kutosha , kisa magari hayana kazi! kituo kimoja unapokaa panapita treni za mjini , mabasi lukuki kila dakika tano! Gari la nini? hakuna mtu anachelewa kazini sababu ya usafiri , uchumi unapaa sababu jamaa hawapotezi muda kama bongoland kutoka mbezi hadi posta masaa manne! eti kwetu ukiwa na gari watu wote wanakuita 'mzee' hata kama ni kijana! Ukiwa na kitambi unaitwa mkurugenzi wakati huku , unapelekwa hospitali na ambulance manake wewe ni mgonjwa una mafuta hayana kazi! Jamani tembeeni muone! Najiuliza hawa mabalozi wetu wako kila mahali duniani hawaoni haya maendeleo huko waliko? hawajisikii guilty wanaishi vizuri huku Marekani na Ulaya na kwao kuko nyuma sana kimaendeleo? je hawaleti changamoto kwa serikali angalau tuige yanayowezekana? kiukweli nimesikitika sana na umaskini wetu, hata usafiri wa umma unatushinda? nimekumbuka UDA ilikufa aisee! Kutokana na ulafi wetu tuliifilisi! Ila hongera sana Mwakyembe kwa treni ila inatakiwa iende kila mahali mf tegeta , kigamboni , mbezi nk, nimegundua ili tuendelee ni mpaka tuwe na uthubutu wa kujaribu mawazo mapya , KUJIPATIA SAYANSI NA TECHNOLOJIA YA KISASA NA UTAMADUNI WA KULIPA KODI NA KUAONDOKANA NA LAANA YA UBINAFSI na tuondokane na laana ya kujilimbikizia mali za umma na ubinafsi wa kula mali ya umma ndo tutaendelea na inawezekana kabisa kuendelea maana huku Marekani na Ulaya mbona imewezekana? ,

Najiuliza je huyu sijui CAG anafanya kazi yake vizuri ? je anakamata wezi kweli ? wezi wangapi wa mali ya umma wametupwa jela? siku moja nilimskia kiranja wetu katika hotuba ya mwezi akisema watajenga ofisi ya CAG kila mkoa, big up sana mkuu.mi nasubiri kuziona hizo ofisi na utendaji wake! Nimegundua ili tuendelee ni watu wote tujifunze kulipa kodi , kuacha kuiba pesa ya umma na kuacha ubinafsi,nasikia uchungu sana nimezaliwa kwenye umaskini na nazeeka kwenye umaskini!

Sasa nimewaza sana nitafikishaje ujumbe wangu huu, mimi natoka mikoani kama wakazi wa Dar mnavyopenda kutuita! Mnatuona washamba sana nasisi tunawaona nyie hivyo hivyo manake huku watu toka dunia nzima wanakuja kutalii tunakaa nao na kupata maujanja ! sasa huwa nikija jijini kwenu nikikaa siku moja tu nachoka sana , nachoka kupita kiasi kwa kila wakati niko makini najilinda nisiibiwe simu na pochi na ‘mateja' wenu na foleni zenu haziishi!sasa nakaa siku ya kwanza, siku ya pili bila kufukuzwa na mtu na bila kuwaambia wenyeji wangu ambao wao wanafurahia maisha yao jijini , huwa naenda Ubungo napanda Ngorika narudi zangu kaskazini! mnajua hapo kwenu DAR huwa najisikia kama niko JEHANAM kwa foleni zenu ambazo nyie wenyewe mmezizoea , magari yakisimama mnatoa magazeti mnaanza kusoma au kuongea na watoto wanaouza vitu barabarani! wengine labda mnapenda foleni , sijui! sasa jamani wadau chonde chonde nawaomba , nimepiga magoti nawaomba mchangie mada na nawaomba mfikishieni waziri wa usafirishaji ujumbe wangu , ni kuhusu foleni za Dar ni rahisi sana kuziondoa na kubaki historia , na hapo tutaendelea kidogo kidogo manake muda ni mali, unajua cha kufanya? HUU NI MRADI MKUBWA NA NCHI HAINA UWEZO LABDA!sasa dawa ni kuongea na China na Marekani maana wote ni marafiki zetu na wanatupenda na labda wanatugombania , wao wanajua kwa nini!, labda kwa maslahi yao, rasilimali zetu , sio mada yangu. Ninachosema ni kuwa hapo Dar kuna maeneo ya njiapanda kama kumi ya kujenga madaraja makubwa ya magari kupishana , yaani magari yanayotoka na kurudi upande mmoja yanapita juu na kushuka mbele ya njia panda na mengine yanaoenda na kurudi upande mmoja yanapita chini.Maeneo hayo ni Ubungo, Morocco, Movenpick , Tazara, Karume, Akiba, Mwenge,Magomeni, Faya na Kigogo n.k. Daraja kama hili pia linatakiwa kujengwa pale WAMI ili watu wasiendelee kuangusha magari na kufa! Hivi kati yenu nani amefika Delhi? ni jiji kubwa sana India lina miji miwili , Old and New Delhi, hakuna foleni hata chembe, ni njia hii wanatumia , madaraja ya kupanda na kushuka kila njiapanda , ! ila tena kwa bahati nzuri , kuna familia za mama , baba na watoto wao wanaishi chini ya madaraja haya na wana TV ! eti sasa na Uganda na Kenya nao wanatushinda? Wanayo madaraja baadhi ya njiapanda!

Naamini Mwakyembe na Magufuli wanaweza kufanikisha mradi huu wakiamua!nawakubali sana hawa waheshimiwa, maana kiranja mkuu najua atawasupport!Tukumbuke kila kitu kinaanza na idea ndogo tu! tembeeni muone ndugu zangu wabongo sio kazi muda wote kubishana tu tunabaki kuwa maskini hadi tunakufa! Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe. Tuone aibu kwa umasikini wetu huku tukiwa na rasilimali za ajabu , mfano mdogo tu , kila mtalii wa nje analipa dola 50 kuingia mbuga ya wanyama , je ni watalii wangapi wanaingia mbugani kwa siku , mbuga zote za Tanzania, hizo hela zote zinafanya nini? Tangu nimezaliwa sasa nina miaka 50 sioni chochote cha maana kwa mapato ya Tanzania , je misamaha ya kodi itaisha lini? Huku Marekani na Ulaya on daily basis watu wanadiscuss rushwa, utegemezi, umaskini , njaa na magonjwa ya nchi za Africa na Tanzania ikiwemo, wakati mwingine tunaambiwa tutoe maoni yetu , kiukweli tunasikia aibu sana!

Bado nakumbuka jamaa mmoja wa upinzani nikiwa naangalia kampeni kwenye tv mwaka 2010, alikiponda sana chama flani cha siasa kuwa badala ya kuondoa maadui watatu wa Tanzania ambao ni ujinga , umaskini , na maradhi , eti jamaa wameongeza adui wa nne , ufisadi! nadhani ni kweli labda!Bado najiuliza hao watu tunaoambiwa wameficha pesa Uswisi billions 360 ni kina nani? Kwanini hawatajwi? Kuna nini behind this issue? Hizo hela walitoa wapi? Ndo maana umaskini hauishi bongo aisee, ni mpaka siku tutaacha kuoneana aibu na kuficha mabaya ya wanaojidai wakubwa ndo maendeleo yatakuja! Ni mpaka siku tutawataja mafisadi wote na kiasi wanachoiba na siku tutaendelea ni ile siku ‘corruption' itaisha Tanzania! Swali kubwa ni kuwa nani ni ‘msafi' sasa amfunge paka kengele au nani hana ‘boriti' amtoe mwenzake kibanzi? Bado naamini maneno ya Mwalimu kuwa ili tuendelee tunahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora, but kwa Tanzania ya sasa everything here is questionable!

Bado najiuliza kuhusu ugunduzi wa gesi na mafuta, je hapa si ndo tunauaga umaskini? Mungu atupe nini tena wadanganyika, najiuliza kama mafisadi pia wako huku kwenye gesi na mafuta, kama na huku wameshatia mikono na miguu yao michafu yenye laana na dhambi za dhulma ya majasho ya walalahoi, basi tumekwisha! Naamini kiranja mkuu yupo makini kabisa , naamini Mungu atamsaidia atasimamia vizuri hizi rasilimali mpya zitutoe kimaso maso maana zingine ziko mifukoni mwa watu wazalendo wenye uchungu na nchi yao! Jamani tuthamini mawazo yetu , tuwe na uzalendo na nchi yetu , tuache kutoa, kupokea na kuomba rushwa, tumuogope Mungu na tuyafanyie kazi mawazo yetu ndugu zangu. Jamani haya ni mawazo yangu tu! Nawe toa mawazo yako kunipinga au kuniunga mkono ili siku moja nasi tupande haya mabasi ya kutembeza watalii huku ambayo yana ghorofa! Natamani kupita kiasi kiranja mkuu wetu na msaidizi wake wasome nakala hii, nawaamini sana hawa waheshimiwa , wako serious na maendeleo ya bongo , najua akisoma hizi thoughts lazima atafanya kitu ila naamini kuna baadhi ya watu wake , kundi kubwa au dogo labda , inawezekana siko sahihi lakini mimi naamini labda nadhani kuja jamaa siwajui wanamuangusha kwa makusudi kutokana na ubinafsi , umaimuna , tamaa na ulafi wao! Jamani tukumbuke tutafanya mbinu zote ila si kila mtu ameandikiwa na Mungu mkuu wa majeshi ya ardhini na majini na angani kuwa kiranja mkuu! Na bahati mbaya sana kuna matukio mabaya sana ya uvunjifu wa amani yanaendelea kwa kichaka cha dini! Hivi tumeshawakama wahusika? Naomba nipate maoni yako wewe ambae umesoma na kuelewa vizuri , nakuomba usiwe na papara, nakuomba usubiri wakati nakusanya orodha ya mafisadi wa muhimu , orodha ni ndefu sana ,nakusanya na ushahidi ndugu yangu ukitaka kula nguruwe chagua alienona, una haraka gani ndugu? Nakusanya orodha ya wahujumu uchumi wa taifa tangu tupate uhuru na naomba kwa ruhusa yenu niwataje mafisadi wote wanaosababisha umaskini wan chi yetu katika ukurasa wangu wa pili utakaokuja siku na saa ya mwisho wa mwezi huu , usikose kucheki JF upate majina wewe ukiwa wa kwanza, Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania. Naomba kutoa hoja!

Unaongea mambo mengi ya msingi lakini hayafanani na kichwa cha habari, kwa ufahamu wangu wa Kiswahili cha Mti wa Korosho. Orodha uhenda kwa namba sasa wewe umeweka story ndefu ambayo unaweza kutengeneza vile Vitabu vya Tsh.500 ukapata pesa ya kununulia Mboga
 
hongera mkubwa naona ume target sehemu yenye attention sana, unataka kutujuza then unatupiga changa la macho daa!wabongo bwana.
 
sasa umeona tatizo jingine la satanzania kwa nini masikini ni kama hawa hapa juu,hawapendi kusoma
 
Back
Top Bottom