Orodha Rasmi ya watu wanaopitia Maisha magumu nchini Tanzania

Huu sio utafiti bali ni story tu za kijiweni. Huna theory inayoku guide, huna methods za kuja na hitimisho lako, huna conceptual framework n.k n.k
Kifupi andiko hili ni misleading kwa kuwa halina basis pia linaweza kuleta taharuki na kuathiri afya za akili za watu zaidi.
 
Kinga'i na mahita umewasahau
 

Ukisema Waluguru ni wafupi au wapare hapo unazungumzia utafiti au Hali halisi?

Sio kila kitu kinahitaji Utafiti. Hizo methods,sijui guide na sijui Framework hayana maana kwenye elimu kitaaolojia.

Ndio maana wamasai hawajasoma ufugaji lakini wanawashinda wasomi wa SUA Kwa Uelewa wa mambo ya Mifugo.

Elimu uliyonayo ni nadharia tuu. Ukihitimu kozi ya kitaolojia ndio siku utajiona ulikuwa umesomea ujinga Huko chuoni na methods zako
 
Aliyesomea ujinga na mjinga nani mjinga?
 
Hahaha watu wanashindwa kuelewa hii kada ipoje,Ndo maana kila mara utasikia watu wanawaponda walimu.Walimu wenye msongo wa mawazo na fukara ni wale wanaoishi na kufanya kazi huko vichakani haijalishi anafundisha chuo,Secondary au Primary.
Hapo nikukosoe kidogo ndugu, walimu wanaofanya kazi machakani wanaheshimika, wana pesa kutokana na kufanya biashara na wanahusudiwa sana kifupi wana maendelea makubwa ukilinganisha na hao wa Dar, endelea kujidanganya
 
Haya ya ufupi na urefu , mwingine anaropoka Degree na Diploma huku mtaani hatuyaoni, Watu wanajichanganya maisha yanaenda kama kawaida ,

Kule makanisani, kwenye jumuia na vikoba watu wanaosikilizwa ni wale wenye ushawishi , exposure na uzoefu wa mambo bila kujali elimu zao na maumbo yao,

Hata wanaoongoza kupendwa na wanawake wengi hasa ni wale wenye kipato kikubwa bila kujali elimu zao na maumbile yao.

Huku mtaani Halisia wapo warefu na wachakarikaji pia warefu wapumbavu , wapo wafupi wachakarikaji na wafupi wapumbavu, je hamjui kuwa mwananamke mwenye akili hawezi mkubali mtu mrefu mpumbavu akamwacha mfupi mchakarikaji!

Malizieni kwanza degree zenu mrudi mtaani muone jinsi ulimwengu ulivyo.
 
Hapo nikukosoe kidogo ndugu, walimu wanaofanya kazi machakani wanaheshimika, wana pesa kutokana na kufanya biashara na wanahusudiwa sana kifupi wana maendelea makubwa ukilinganisha na hao wa Dar, endelea kujidanganya
Mkuu machaka yanatofautiana.Nadhani unazungumzia vijiji siyo mashenzini.Huko hamna cha biashara wala nini.Yaani unakuta Chaka zima lina duka moja na lenyewe linafunguliwa jioni na anaishia kuuza buku.Naongea from experience mkuu sema naogopa tu kutoa mfano halisi hapa watu wataaibika
 
Labda huo msamiati wa mashenzini umenishinda, ila walimu wengi wa vijijini wako njema sana, wana maendeleo makubwa, wanajitutumua watoto wao wanasoma shule nzuri huko mjini, wanatumia fursa za mashamba kuzalisha mazao na kuuza, ingawa walevi na waliopoteza mwelekeo nao wapo wengi pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…