Orodha ya bandari kavu za magari Dar es salaam.

Orodha ya bandari kavu za magari Dar es salaam.

BabaMorgan

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2017
Posts
4,869
Reaction score
13,137
Kutokana na ufinyu wa eneo la bandari ya Dar es salaam ambayo kwa Sasa lipo chini ya uendeshaji wa DP World imefanya bandari kushirikiana na wadau wa sekta binafsi katika kutoa huduma za kibandari.

Unapoagiza gari kutoka nchi za nje unaweza kulipokea bandarini TPA ama bandari yoyote kavu kati ya hizi.

1. TALL hii ipo gerezani kariakoo mtaa wa shauri moyo inasemekana ni ya kigogo mstaafu ambaye alishawahi kushika nyadhifa kubwa serikalini na kwenye chama.

2. FARION ipo Serengeti ikiwa imepakana na shule ya kibasila

3. FAB Inapatikana Mbagala kizuiani changamoto ya hii ICD imepakana na viwanda vya cement na pumba kitu kinachopelekea magari kuchafuka kutokana na vumbi ila wamiliki wa hiyo ICD wanaingia gharama ya kuyaosha magari.

4. DARSTAR hii ipo Buza kwa Mama kibonge.

5. DEUMEUM ipo Tabata Matumbi.

6. BLOOMER Tabata Mwananchi

7. ROUTE MASTER Inapatikana Mwenge karibu na Coca-cola

8. SSA Banda la ngozi

9. As Fast Kigamboni baada ya kuvuka darajan unaingia njia panda ya tumbi

10. GALCO ya tajiri GSM Inapatikana kigamboni kituo SIDO

Hizo ndio ICD za magari najua wapo wenye ujuzi mkubwa zaidi yangu ningependa kufahamu ni vigezo gani vinatumika ili kuipa ICD meli.
 
Katika hiyo list iliyotaja sidhani kama IPO nyingine..
Hata Mimi nilishangaa agent wangu alivyoniambia gari yangu IPO tabata matumbi nakumbuka zamani kilakitu tulikuwa tunamaliza bandarini.
Kwenye hizi ICD ndipo wizi wa vitu vidogodogo utaanzia ebu fikiria gari inatoka bandarini huku mshale wa mafuta ukiwa empty Hadi tabata alafu baada ya hapo itoke tena Hadi kituo cha mafuta huku ukiwakwepa bodaboda na bajaj.

Kungekuwa na ICD kubwa pale kurasini inayomeza magari yote ingekuwa poa sana
 
Usalama kimsingi ni mdogo Kuna vitu vidogo vidogo vinavyowezekena kubebwa vinachukuliwa na baadhi ya madereva wasio waaminifu.

Lakini katika vitu vinavyopewa kipaumbele na wamiliki wa hizo ICD ni kukomesha wizi lakini sio rahisi kumdhibiti mwanadamu
 
ICDV ni salama kama bandarini, msiogope location zilipo kama gari ukiagiza itashuka na utapokea kama ulivyoagiza.

Endapo utakuta kitu kipo tofauti una haki ya kudai. ICDV inaendeshwa kwa sheria na kusimamiwa na Tasac &TRA. Kitendo cha dereva kuiba wheel spaner, Jack au triangle kinamkosesha mmiliki wa ICDV sifa na kuingia kwenye kosa la kuhujumu uchumi leseni yake inaweza kufungiwa.

Saizi operators wa ICDV wapo strictly sana, ndio maana wengine wanapotoa gari bandarini huwa na escort ya walinzi na wanaenda kwa convoy
 
Katika hiyo list iliyotaja sidhani kama IPO nyingine..
Hata Mimi nilishangaa agent wangu alivyoniambia gari yangu IPO tabata matumbi nakumbuka zamani kilakitu tulikuwa tunamaliza bandarini.
Kwenye hizi ICD ndipo wizi wa vitu vidogodogo utaanzia ebu fikiria gari inatoka bandarini huku mshale wa mafuta ukiwa empty Hadi tabata alafu baada ya hapo itoke tena Hadi kituo cha mafuta huku ukiwakwepa bodaboda na bajaj.

Kungekuwa na ICD kubwa pale kurasini inayomeza magari yote ingekuwa poa sana
ICDV kubwa zina mobile car ya kubeba mafuta kwa gari ambazo zinakata mafuta na wanaomba gatepass wanaingia mpaka bandarini kwa ajili ya kuzipa mafuta.Pia wanakuwa na battery booster kwa ajili ya magari yaliyokuwa low battery wakati wa kuwasha.

Gari zenye matatizo huvutwa na gari nzima, mpaka ICDV na mteja siku ya kuchukua atarekebisha mwenyewe.
 
mafuta wanakuwekea kwa gharama za nani?
 
mafuta wanakuwekea kwa gharama za nani?
Gharama zao, mafuta yanawekwa kidogo ya kutoka Bandari kwenda ICDV husika. Ndio maana sheria ya kumiliki ICD inatakiwa eneo lisizidi umbali wa 30km kutoka Bandarini
 
Ya kwanza na ya pili kwenye list zilikuwa kama simefungwa miaka ya miwili au mitatu kurud nyuma
 
Kuna ICD moja hapo dereva alikimbia na gari ndogo wakati wa kupeleka, gari ilitafutwa haikuonekana. Hiyo ICD ikazuiwa kwa muda saizi kama inafanya basi wako kwa uangalizi
 
Back
Top Bottom