NB: Unaweza pia soma >
Biashara za kufanya kwa mtaji mdogo wa elfu 10 mpaka 50
======
Ni muda sijaandika uzi katika jukwaa hili, nimepata msukumo leo baada ya kisa kilichotokea apa katikati na kunifanya nione
umuhimu wa
kukumbushana lakin pia iwe kichocheo cha
kuamsha tafakuri katika maamuzi yetu kweny biashara zetu.
Iko hivi, mwaka juzi nilipata simu kutoka kwa mentor wng na kwa ufupi alisema kuwa kuna kijana amempatia mawasiliano yangu na
kunitaka nionane nae. Kweli siku hiyohiyo kijana yule alinipigia na baada ya mazungumzo alitaka kuja ofisini kwa ajiri ya swala lake lakini nilimkatalia kutokana na ratiba ya siku hiyo. Tulipanga siku ya kuonana na nilichogundua kwa mazungumzo ya simu tu kuwa jamaa ana 'mizuka'.
Siku iliwadia tukaonana na baada ya salam na stori kidogo nilimuuliza kuhusu kiini cha sisi kukutana. Kijana huyu ambae wakati wote alikuwa 'mchangamfu' alinieleza kuwa ana 'Project' ambayo amekuwa akifanyia tafiti kwa muda mrefu na kuwa amepata '
wazito' ambao wako tayari kuwekeza kwnye project hiyo. Kwaiyo alikuwa ana hitaji mtu ambae atamsaidia katika mawazo ya namna ya kuongeza na kuboresha project hiyo.
Wakati huu tunaonana jamaa alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni ya mentor wng na hivyo alikuwa amemuomba amsaidie katika hilo. Kwasababu mentor hakuwepo nchini wakat huo na kulikuwa hakuna dalili yotote ya kurejea karibuni, ali m-direct jamaa kwangu kwa ajiri ya kazi hiyo.
Nilipata muda wa kupitia
mpango wake biashara ('business plan') na baada ya maswali niliyomuuliza kujibiwa kwa usahihi na kwa uwazi kabisa (labda sababu alipewa assuarance na mentor wangu). Binafsi niliona kabisa huyu ni mtu ambae kafanyia tafiti wazo lake sio zile
'empty set', hivo sikushangaa yeye kushawishi wazito kwa haraka.
Sote tunafaham kinachovutia kwenye
business plan ni kipengere cha '
financial statement' (projections) na apa ndipo nilipogundua
dosari kubwa. Pamoja na wazo kuwa zuri
ila hesabu za
makadirio ya
mapato na
matumizi zilikuwa
kinadharia sana yaani '
they were simply based on fantasie rather than reality'. kwa lugha ya kichumi alitumia kitu kinaitwa '
haphazard approach' sina tafsir nzur ya kiswahil lakin itoshe kusema
alijipendelea faida sana
kinyume na hali halisi.
Hata nilipojaribu kukadiria
degree of operating revenue bado nilikuwa nagota kwenye
hasara tu. Na kwa mtazamo wangu nilijaribu kumwelesha kuwa kwa '
uchumi wa awamu hii' itakuchukua almost miaka 4 na kitu kufika ata ile hatua ya
break even yaani gharama za
uzalishaji ziwe
sawa na
mapato.
Kauli zangu zilianza kufifisha tabasamu la 'amigo' na kwa muda tulipishana sana lakin tukaafikiana kuwa 'tutengeneze'
leap of faith hypothesis yaani 'mikakati' ya muda yenye
ufanano na lile
wazo kuu kama
kujaribu soko kabla ya kuingiza mtaji wote. Haikuwa rahisi kwa siku iyo basi tukaachana na mimi nilitimiza ahadi yangu ya kumtumia mawazo yng kwa email.
Tuliendelea kuwasiliana kwa yeye kuni update maendeleo ya hiyo project yake, nikiwa
nafaham anafanyia kazi yale 'tuliyokubaliana' na baada ya muda mawasiliano yalikatika kabisa na mim nikawa nilisha sahau kabisa.
Ni mpaka juzi ikiwa ni takriban mwaka toka tuwasiliane nimepata email yake nikiwa safarin ambayo ndio
imenifanya niletee uzi huu. Huyu bwana baada ya mawasiliano yetu yeye aliendelea na project yake kama alivokuwa amepanga awali ata labla ya kukutana na mim. kifupi alikuwa yuko '
obsessed' sana na ile
'perfect idea' yake kiasi kwamba ilimfanya kipofu hata kushindwa kuona reality. Kwaiyo yeye alikuwa anatafuta tu mtu wa ziada
kumbariki na si
kukosoa.
Sasa project ina mwaka na kitu na hawajaweza ku cover ata gharama za uendashaji, na wale wazito wame mkalia kooni hajui afanye nini. Ingawa ni mwaka tu na kwa sisi wazoefu tunasema ni mapema kutoa judgement lakini
still chances of survival are limited
kweli hali ya
biashara mtaani ni
mbaya bidhaa
haziuziki lakin
je unauza bidhaa sahihi kwa wakati huu?? usije ukawa una lalamikia kumbe bidhaa unazouza ww watu
hawazihitaj wakat huu.
kila
awamu huja na
changamoto zake na hata
matumizi ya watu
hubadirika hivyo ni kazi yako wewe mjasiriamali kuwa mwepes wa
kung'amua nyakati na
kubadilika pale upepo wa
mabadiliko uvumapo.
Pesa kwa sasa imekuwa
adimu na zile chache
walizonazo watu wanatumia kwa
mahitaji yao ya
msingi au zile
huduma/
bidhaa ambazo wana
urahibu/addiction.
Swali la
kujiuliza katika mahitaji yao ya maingi wewe unawazuia nini??.
Je
unafahamu kuwa kuna bidhaa ambazo ni addiction kwa watumiaji??
Kwa muktadha wa maswali hayo, mjasiriamali mwenye kiwanda chako au biashara ili uweze kupata
uhakika wa
mzunguko wa fedha ni lazima bidhaa/huduma zako zizunguke kwenye maeneo hayo
mawili.
Mahitaji ya msingi yanafahamika, apa nita
gusia zaidi upande wa
biashara/bidhaa zenye
urahibu.
Neno
urahibu limekuwa likitumika sana kuelezea kuhusu
utegemezi wa madawa ya kulevya, Lakin ni
nadra kulisikia kwenye
bidhaa/huduma tunazotumia kila siku.
Basi chukua hii kutoka kwangu(
THE LIST) na utizame ni namna unaweza kupiga pesa.
**
Apa ntakupa THE LIST ya biashara/huduma ambazo zitakuhakikishia uhakika wa soko ata katika ichumi uliodorora**
Kwa namna ambayo itadizain mpango wako wa biashara basi hakikisha unazunguka kwenye zile bidhaa au huduma ambazo hutengeneza urahitbu kwa mteja baada ya muda wa matumizi.
Kwa
muktadha huo, hii ni orodha ya
sekta mbalimbali ambazo unaweza ukabuni
bidhaa|huduma ambayo afe kipa afe beki lazima
itanunuliwa tu.
Sekta ya urembo na utanashati
-urembo na utanashati ni tabia ambayo si rahisi kuiacha, hii ni kwa wadau wa rika zote..waume kwa wake.
kuna biashara nyingi ambazo unaweza ukafaanya ndani ya kipengere hiki zaidi tizama ni vitu gani watu hutumia zaidi, mafuta, perfumes, mawigi, viatu, saloon n.k
Vilevi na hasa pombe.
Urahibu wa pombe wala hauhiitaj maelezo mengi, sekta hii yenyew iko wazi ata mitaani uko..yaani vyuma vimekaza lakin bar zinajaa
Apa unaweza buni wine yako mwenyew, wakala wa jumla wa pombe, kufunvua bar au grocery
Michezo
Kwa bongo mpira wa miguu una wapenzi wengi na ww unaweza kutengemeza pesa kupitia urahibu huu kwa kufungua betting centre, gori la kuonyesha mpira, kuprint tshirts, video games uko iswazi n.k
Repairing centre..
kipini hiki badala ya mtu anununue gari au simu mpya ni bora atengeneze ile ya zamani, wekaza eneo kwa ku kutoa hizo huduma.
Huduma za Vyakula
Sekta hii kwa maneno ya
Mo anasema kwa
mtu yeyote anaetaka utajiri Africa basi awekeze katika matumbo ya watu. Kwa maneno hayo ni dhahiri sekta hii ina wateja wengi sana na ni ngumu kuyba ata uchumi ukiyumba vipi.
Ni sekta pana inayoanzia kwa mkulima, sokoni, kiwandani mpaka kwa mlaji. Sasa katika chain yote hiyo wewe unachangia vipi?
Itaendelea...
Nikukumbushe Mjasiriamali mwenzangu
huna sababu ya kushindwa kuingiza faida ya laki moja au zaidi kwa siku kwa
kisingizio uchumi umeyumba. Ukiona unalalamika basi
kuna kitu unafanya sio sahihi.
Haya ni
mawazo ya
kivitendo kutoka kwa mjasiriamali (
THE LIST) na sio
falsafa mfuu au
porojo za semina uchwara..
yanatekelezeka!!
Haki za
umiliki zote
zimehifadhiwa
THE LIST.