Kufuatia mapitio yaliyofanywa na Wizara ya Afya kwenye Orodha ya Taifa ya Dawa Muhimu (NEMLIT) kwa kujumuisha muunganiko, muundo na nguvu kwa dawa 178, NHIF imejumuisha dawa hizo kwenye Kitita chake cha Mafao cha Mwaka 2023.
Hatua hii inaongeza wigo wa aina za dawa zenye muundo, nguvu na muunganiko mbalimbali hivyo kuwapa Watoa huduma wigo mpana wa kuandika dawa na wanachama kuendelea kupata huduma stahiki za matibabu kwa kuzingatia miongozo ya tiba nchini.
Ili kuona dawa hizo tafadhali tembelea tovuti ya Wizara ya Afya www.moh.go.tz