Orodha ya majukwaa muhimu ya kutembelea kila siku hapa hapa JF

Orodha ya majukwaa muhimu ya kutembelea kila siku hapa hapa JF

Fundi manyumba

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2018
Posts
3,799
Reaction score
8,063
JamiiForums watu wanazidi kuongezeka hasa vijana hivyo tunazidi kuongezeka Kwa idadi kubwa sana.

Sehemu yenye watu wengi kama hivi ni lazima kuna kuwa na watu wenye tabia mbali mbali na michango tofauti tofauti.

Michango hiyo inaweza kuwa positive au negative kwako inategemea ni vipi utachukua na kufanyia kazi.

Michango hiyo kama kijana unaweza tumia kuimarisha mawazo yako ili kukuabiliana na matatizo mbali mbali au changamoto.

Sasa kama kijana mwenzangu (Hustle) ambaye unatumia mitandao kwa positive way achana na kuwa chawa au kuomba omba pesa unaweza pata mawazo mbali mbali ambayo yatakujenga basi huna budi kuwa na ufuatiliaji wa haya majukwaa japo kila siku ambazo utaingia..

Sio lazima usome deep ila unaweza fanya skimming tuu.

Unaweza kuta headline ambayo itakufungua kitu fulani.

Kwa kuanza tu ili kujifunza mambo mbali mbali hasa hapa JF basi muhimu kupita (Kuchungulia) humu kila siku:

1.Jamii Health (Jukwaa la Afya):

Kijana mwenzangu hapa utapata hint mbali mbali za afya

Najua unajua hili jukwaa ila nakuambia hii sasa.

Sio kila taarifa inaweza kurushwa kule hoja mchanganyiko.

Sio kila taarifa inaweza kuwa trending

Hivyo kupitia hili jukwaa unaweza oata hint mbali mbali kama kijana hustle sisi mtaji wetu ni afya hivo unapoweka mazoea kupitia hapa unaweza pata kitu..unaweza pata hata hofu kutokana na michango ya watu ambayo itakupelekea wewe kuacha tabia hiyo mbaya.

2.Jukwaa la Biashara, Uchumi na Ujasiriamali:

Mkuu hata kama wewe umeajiliwa na una costant nzuri ya pesa usiache pitia hapa.

Unajua hapa kuna hint mbali mbali za biashara na ujasiriamali.

Wewe huko ulipo kuna watu wengi nyuma yako huwenda ikawa ndugu zako ambao wapo katika system ya biashara mbali mbali hivo michango mingi huku inaweza kukujenga wewe au hata huyo jirani yako.

Najua msaada wa mawazo hasa kwa mtu anaye jielewa ni bora zaidi kuliko hizo pesa.

Kuna watu wana kazi zao ujue ila katika familia unakuta yeye ndie tegemezi katoboa yeye ila wengine huku nyuma wanajitafuta je uwezi pitia hapa ukapata wazo la kufanya wengine wainuke ili na wewe majukumu yapungue..

Una shemeji yako hapo hom kafeli form 4 yupo yupo tuu.

Pitia hapa pata wazo la kitu furani rudi mtaani anza research ndogo ndogo muwezeshe..

3.Jukwaa la Ajira na Tenda :

Kwa wale ma hustler wenzangu tujue kila siku kuna ajira mbali mbali achana na kusema huku hakuna connection No zipo ila tu ni vile hatujawa serious.

Amini Kwamba... Kuna watu wanapata connection za kazi kupitia nyuzi za watu wengine .. mfano kuna mtu kaandika uzi anatafuta kazi lakini katika comment unakuta jamaa kazi nyingi zimepatikana je hapo vipi na wewe uwezi kupata...

Kuna huyu Jamii Opportunities japo anatoaga kazi kwa kutishia amani sana lakini ni za kawaida sana ni vile anaweka manjonjo mengi..

Lakini hapa pia kama wewe ushajipata kama mzee wetu hapo Grahams unaweza pata kijana wa kukufanyia kazi mbali mbali hapa hivo ni wewe tuu tena kwa bei safi kabisa.

4. Trending:

Hili sio jukwaa ila ni kipengere tu ambacho unaweza kuta trending mbali mbali za nyuzi ambazo zimekua ziki jadiliwa mda huo hapa ni muhimu sana kama kijana ambaye unakuja na kutoka na una kazi zako maalumu basi hapa panakufaa sana tena sana..

Sasa wakuu tupate kujua ni Kwa namna gani unaweza kunufaika kwa kuwa member ambaye unafata haya makukwaa hapo juu

1- Unakua conscious sana kwani uwezi kuwa kijana wa hovyo hovyo maana unakua unajua mengi

2- Connection za kutosha kuna watu humu wana connection mbali mbali lakini pa kuwakuta ndio mziki.

Sasa wewe komaa kule chitchat kutwa kuangalia picha za warembo duniani alafu utegemee kupata connection ndugu...

Ndoto na malengo yako huhitaji ukweli, haki, upendo na akili (maarifa na ujuzi) kisha huhitaji muda ambao utazitimiza.

"Everything you see and perform are equally in magnitude from point of judgment" DR HAYA LAND
 
Back
Top Bottom