Orodha ya makao makuu ya mikoa ambayo bado yapo nyuma kimaendeleo

Orodha ya makao makuu ya mikoa ambayo bado yapo nyuma kimaendeleo

mkata uzi

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2025
Posts
3,253
Reaction score
9,736
  1. Mpanda – Katavi

    mkoa huu ni miongoni mwa mikoa mipya, hivyo miundombinu ya kiutawala, biashara, huduma za jamii na uwekezaji bado inaendelea kujengwa.

    Pamoja na kuwa na fursa kubwa katika kilimo, mifugo na maliasili, uchumi wa mji bado unakuwa taratibu. Umbali kutoka vituo vikubwa vya biashara na miundombinu ya usafirishaji pia unaweza kuwa sababu inayopunguza kasi ya ukuaji wa sekta binafsi.

  2. Lindi
    Lindi ni miongoni mwa miji ya zamani nchini, lakini licha ya historia yake ndefu kama kituo cha utawala na biashara, maendeleo yake ya mijini yamekuwa ya taratibu.


  3. Bariadi – Simiyu
    Bariadi ni mfano wa mji ambao bado unaonekana kuwa katika hatua za kujijenga kama makao makuu ya mkoa mpya. Tayari kuna miundombinu ya usafiri na elimu inayoongezeka, pamoja na uwekezaji katika huduma mbalimbali. Kuna stendi ya mabasi ya kisasa pamoja na chuo cha IFM, Hivyo japo kimaendeleo bado ipo nyuma, ukuaji wake unaleta matumaini

  4. Musoma – Mara

    ni makao makuu ya mkoa mkongwe wa Mara, Kiujumla mkoa huu wote upo nyuma licha ya kuwa sehemu alikotokea baba wa taifa, Kistratejia mkoa huu unaweza kuokolewa pale ambapo utajengwa uwanja wa ndege wa Serengeti katika mji wa Mugumu, hili likifanikiwa hata makao makuu ya mkoa yanaweza kukua kwa ogezeko la watalii na fedha za kigeni.

  5. Vwawa – Songwe
    Vwawa ni kesi ya kipekee. Kimkakati, Mkoa wa Songwe una nafasi kubwa sana kutokana na mpaka wa Tunduma, biashara kati ya Tanzania na Zambia, pamoja na korido ya usafirishaji ya Tanzania–Zambia.

    Kwa mtazamo wa kibiashara, Tunduma inaonekana kuwa na nguvu kubwa zaidi ya kiuchumi kuliko Vwawa kwa sababu ya shughuli za mpakani na biashara ya kimataifa. Ndiyo maana kuna hoja kwamba Tunduma ingekuwa na mantiki kubwa kama makao makuu ya mkoa.

    Hata hivyo, sababu ya kuchagua Vwawa kama makao makuu inaweza pia kueleweka katika mtazamo wa kiutawala, kwani serikali inaweza kutaka kutenganisha makao makuu ya mkoa na mji wa mpakani

  6. Singida

    Singida ni miongoni mwa makao makuu ya mikoa mikongwe ila bado ipo nyuma kimaendeleo, Jiografia yake ya kuwa ndani ya mkoa wenye ukame inachangia kuwa mji unaokuwa taratibu.

MIKOA AMBAYO ILIKUWA NYUMA HAPO ZAMANI ILA IMEANZA KUPIGA HATUA

Sumba Wanga - Sumba Wanga mliyoijua hapo zamani na sasa ni vitu viwili tofauti, Sumba wanga ya sasa ina afadhali, haina vigezo ya kuingia kwenye list ya makao makuu yaliyochoka

Kigoma - Huu ni mji unaokuwa kwa kasi kubwa sana, sio ile mliyoijua zamani,

Bukoba - Ni mji ambao umeendelea kwa kiasi chake, Kuna malls zinajegwa, kuna Meli kubwa sana inafanya trip kwend Mwanza, kuna Bandari, Kuna airport, Barabara zinajengwa, Shule zinazidi kujaa, n.k.

Shinyanga - Haina vigezo vya kuingia kwenye miji duni, ipo viiwango vyenye unafuu

Njombe na Songea - Ni miji ambayo ipo nyuma lkini haijachoka kivile hadi iingizwe kwenye list
 
Dodoma imejengwa na Mafisadi, kila ukipita hili gorofa la waziri, sijui chawa gani
Dodoma inajengwa na itaendelea kujengwa zaidi kwa sababu Serikali imeamua kuhamishia shughuli zake kuu huko, ni sawa na Abuja ya Nigeria, wazee wa fursa wameshaanza kujenga majengo mapema, wakijua kuwa baadaye watayakodisha kwa wizara na taasisi za Serikali.
 
Back
Top Bottom