escrow one
JF-Expert Member
- Nov 29, 2014
- 1,473
- 2,868
Ifuatayo ni orodha ya makocha ambao walipewa jukumu la kuzinoa timu kutokana na umahiri wao ktk soka lkn wakashindwa kufikia yale mafanikio yaliyotarajiwa na wengi
1. DAVID MOYES (Man U)
Pamoja na umahiri wake akiwa Everton FC lakin viatu vya Sir. Alex Ferguson vilikua vikubwa sana kwake pale OT. Aliiongoza Man U kwenye mechi 51 akishinda 27, Draw 9 na akipokea vipigo 15. Kwa Mara ya kwanza tangu 1995 Man U ilishindwa kufuzu UCL huku ikikamata nafasi ya 7 EPL.
2. GARY NEVILLE (Valencia)
Kwa umahiri wake wa kuchambua soka pale sky sports na umahiri wake wa kusakata kabumbu ulitosha kumpa ajira pale Valencia. Tofauti na matarajio ya wengi aliiongoza Valencia kupata point 14 tu ktk mechi 16 za ligi huku akipata kipigo cha mbwa koko toka kwa Barcelona (7-0) kwenye Copa Del Rey
3. HERVÊ RENARD (Lille)
Kwa mafanikio makubwa aliyoyapata Africa kwa kuziongoza Zambia(2012) na Ivory Coast(2015) kutwaa kombe la AFCON, Lille ya ufaransa hawakua na wasiwasi kumpa kibarua. Lkn aliwaacha watu midomo wazi pale alipoiongoza timu hiyo kupata point 13 ktk mechi 13 hivyo kupewa red card na mwajiri wake.
4. FABIO CAPELLO (England)
Akiziongoza kwa mafanikio makubwa sana klabu za AC Milan, Real Madrid, Roma n.k. England haikupepesa macho kumpa Capello timu ya taifa mwaka 2008 kwa matarajio makubwa ya kutwaa kombe la dunia 2010 pale kwa Madiba South Africa. Pamoja na kuiongoza England kufuzu WC lkn hali ilikua mbaya kwake kwani ktk makundi alishinda mechi 1 tu ( huku timu ikifunga goli mbili pekee kwenye mechi 3) hata hivyo alifanikiwa kufuzu 16 bora alipopata kichapo cha 4-1 toka kwa Wajerumani. Hii ilipelekea abwage manyanga kuwakwepa Waingereza waliokua wamechefukwa mno.
5. FRANK DE BOER (Inter Milan & Crystal Palace)
Ukitaja makocha wenye mkosi De Boer hakosi. Ingawa aliiongoza Ajax kwa mafanikio lkn Inter ilikua kubwa sana kwake. Aliiongoza Inter ktk mechi 14 ( akishinda 5, Draw 2 na akipgwa 7) hivyo kuiacha Inter Milan nafasi ya 12 kwenye msimamo wa serie A. Pia aliiongoza Crystal Palace mechi 5 akishinda 1 na kupata vipigo 4. Hii imepelekea waajiri wengi msimu huu kutomfikiria kabisa kumpa kandarasi.
6. MART NOOIJ (Tanzania)
Akiajiriwa Mara tu baada ya uongozi wa Malinzi kushika hatam ili kuisaidia stars kufuzu AFCON na CHAN. Hakuna sifa ambayo Nooij hakupewa na TFF pamoja na waandishi wa habari. Lkn ktk mechi 18 alizoiongoza stars alishinda 3 pekee, draw 6 na VIPIGO VITAKATIFU 9.
.
Karibuni tuongeze idadi.
7.
8.
9.
10.
N.B. Orodha hii imeangalia performance ya kocha katika timu husika aliyotajwa hapo. Anaweza kua alifanya vizuri timu fulani ila hapo akashindwa kupata mafanikio.