[emoji2][emoji2][emoji2]thibitisha Kama hayupo
Akiwa hayupo kuthibitisha kwamba hayupo hakupo moja kwa moja kwa sababu hayupo ili athibitishwe kwamba hayupo.
Ni kama vile ambavyo huwezi kunipa fingerprints za mtu ambaye hayupo, ili uthibitishe kwamba hayupo.
Hayupo, sasa hizo fingerprints za uthibitisho kwamba hayupo utazipata wapi?
Sasa hapa ni kamam umenipa kazi ya kukupa fingerprints za mtu ambaye hayupo, ili nithibitishe kwamba hayupo. Nitakupaje fingerprints za mtu ambaye hayupo?
Ila anathibitishika kifalsafa kwamba hayupo kwa contradictions za dhana ya kuwepo kwake, kama vile the problem of evil.
Uthibitisho wa kifalsafa wa kwanza, uwepo wa ubaya unaonesha Mungu mjuzi wa yote, mweye uwezo wote na upendo wote hayupo
1. Mungu anasemwa kuwa ni mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote.
2. Mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote haruhusu ulimwengu uweze kuwa na mabaya, atakataa kuumba ulimwengu unaowezekana kuwa na mabaya.Hataruhusu mabaya yawezekane popote.
3. Ulimwengu huu una mabaya.
4. Mungu hayupo
Uthibitisho wa Kifizikia.
1. Mungu anasemwa kuwa ni upeo wa ukamilifu na utakatifu usioweza kuharibika.
2. Kifizikia ukamilifu na utakatifu usioweza kuharibika unapimwa kwa entropy
3. Entropy ikiwa ndogo zaidi, ndivyo ukamilifu na utakatifu unavyokuwa mkubwa Zaidi.
4. Upeo wa entropy kuwa ndogo zaidi ni kutokuwapo chochote.
5. Kama entropy kuwa ndogo zaidi ni upeo wa ukamilifu/ /utakatifu na ni kutokuwapo chochote, na Mungu ni upeo wa ukamilifu pia, habari nzima ya kuwepo Mungu inakuwa sawa na kutokuwepo chochote.
6. Mungu ni kutokuwepo popote
7. Mungu hayupo kwa sababu tupo na ulimwengu haujajawa na kutokuwepo chochote popote.
8. Mungu hayupo kwa sababu kama kuwapo Mungu ni kutokuwapo chochote, kuwapo kwa Mungu ni kutokuwapo kwa Mungu.
9. Asili inakataa ombwe, hata linaloitwa ombwe linazaa "virtual particles" muda wote, isitoshe lina space, kutokuwapo chochote maana yake hata space haipo.
10 Kichwa hakijakuuma tu bado?