Hii ni orodha iliyotolewa kwa Juni 2026. Kuwa na Sarafu yenye thamani kubwa kunazinufaisha sana nchi za Afrika kwa kushusha gharama za bidhaa zinazoingizwa kutoka nje, kudhibiti mfumuko wa bei, na kuongeza kuaminika kwa wawekezaji.
Kuimarika kwa thamani ya cedi ya Ghana na sarafu ya Zambia hivi karibuni kumetokana na kupatikana kwa urahisi kwa fedha za kigeni, kufanya vizuri sokoni hasa kimataifa na kuongezeka kwa biashara ya madini ya shaba.
Nchi nyingi za Afrika zinategemea sana bidhaa zinazotoka nje ya nchi, ikiwa ni pamoja na mafuta, mitambo, dawa, na vifaa vya viwandani.
Sarafu ya nchi inapokuwa imara, bidhaa zinazoingizwa kutoka nje zinakuwa nafuu zaidi, jambo linaloshusha bei za bidhaa hizo kwa wafanyabiashara na wahitaji.
Kutobadilika badilika kwa viwango vya kubadilishia fedha kunawavutia wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, kwani kunapunguza hatari zinazotokana na kuyumba kwa thamani ya sarafu.
Ukiangalia orodha hii, hakuna hata nchi moja kutoka Afrika Mashariki hivyo inaonyesha ni jinsi gani serikali zetu au nchi zetu zinahitaji kufanya mabadiliko kwa kiasi kikubwa hasa kwenye upande wa uchumi. Ushahidi mkubwa tumeona namna ambavyo zimeyumba ghafla tu shida ya mafuta ilivyoanza, bei ikaongezzeka, gharama za maisha kwa wananchi pia imeongezeka. Hivyo anayeumia zaidi ni mwananchi wa kipato cha chini.
Source: Business insider Africa