Bongo tuna changamoto ya marefa sio wa kike wala ya kiume, ila mazombie ya simba na yanga wako bize kupigizana kelele, leo simba akipewa penati yanga kelele chungumzima, kesho yanga akipewa goli la mkono simba kelele kutwa kucha.
Na hapa ndipo viongozi na wanasiasa wabongo wanapotumia huu mwanya.
Ila mtu ambae unaangalia boli la majuu, ukitizama marefa kule unaona kabisa hawa wetu ni takataka kweli kweli,
Maamuzi yao ya offside ni hovyo, yaani kila kitu hovyo hovyo.
Kwa mtu mwenye ujinga wa uyanga na usimba Ukitizama game ambazo hazihusishi simba na yanga, yaani wacheze jkt na Dodoma jiji labda, ndio utaona matatizo yao vizuri