Orodha ya Wabunge "Mabubu" Wakiwa Bungeni!

Orodha ya Wabunge "Mabubu" Wakiwa Bungeni!

KILITIME

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2009
Posts
265
Reaction score
18
Ndugu WanaJF,
Ifuatayo ni orodha ya waheshimiwa wanaotuwakilisha Bungeni lakini hawajawahi kuuliza swali lolote katika Bunge lililoanza mwaka 2005 na kumalizika mwakani! Kwa ujumla wabunge 89 kati ya 323 hawajawahi kuuliza swali lolote la msingi. Hata hivyo kuna Mbunge mmoja aendaye kwa jina la Rostam Aziz hajawahi kuuliza swali la msingi wala la nyongeza wala mchango wowote! Huyu tunaweza kusema amevunja rekodi ya kuwa mwakilishi bubu bungeni!
Kwa upande wa mawaziri Mh William Ngeleja ameuliza maswali ya msingi 3 peke yake katika Baraza la Mawaziri! Orodha yenyewe hii hapa:

  1. N'hunga, Juma Suleiman
  2. Kwegyir, Al-Shymaa John
  3. Makamba, Col.Lt. Yusufu
  4. Ishengoma, Dr. Christine G.
  5. Bukwimba, Lolesia Jeremiah Maselle
  6. Mukasa, Oscar Rwegasira
  7. Werema, Frederick Mwita
  8. Makinda, Anne Semamba
  9. Karamagi, Nazir Mustafa
  10. Abdallah, Anna Margareth
  11. Kigoda, Dr. Aisha Omar
  12. Burian, Dr. Batilda Salha
  13. Daftari, Dr. Maua Abeid
  14. Bendera, Joel Nkaya
  15. Kamala, Dr. Diodorus Buberwa
  16. Khatib, Hassan Rajab
  17. Kusila, William Jonathan
  18. Maghembe, Prof. Jumanne Abdallah
  19. Mahanga, Dr. Milton Makongoro
  20. Marmo, Philip Sang'ka
  21. Mbega, Monica Ngezi
  22. Mongella, Ambassador Getrude Ibengwe
  23. Mrema, Felix Christopher
  24. Msekela, Dr. James Alex
  25. Mwakyusa, Prof. David Homeli
  26. Azizi, Rostam Abdulrasul
  27. Lukuvi, William Vangimembe
  28. Khatib, Muhammed Seif
  29. Nagu, Dr. Mary Michael
  30. Mwandosya, Prof. Mark James
  31. Kapuya, Prof. Juma Athuman
  32. Ngasongwa, Dr. Juma Alifa
  33. Mungai, Joseph James
  34. Magufuli, John Pombe Joseph
  35. Mwapachu, Harith Bakari
  36. Cheyo, Gideon Asimulike
  37. Lowassa, Edward Ngoyai
  38. Chenge, Andrew John
  39. Khatib, Abdisalaam Issa
  40. Mudhihir, Mudhihir Mohamed
  41. Pinda, Mizengo Kayanza Peter
  42. Mhita, Zabein Muhaji
  43. Chiligati, Capt. John Zefania
  44. Msabaha, Dr. Ibrahim Said
  45. Mwinyi, Dr. Hussein Ali
  46. Chibulunje, Hezekiah Ndahani
  47. Abdulaziz, Mohammed Abdi
  48. Kimbau, Halima Omar
  49. Kabaka, Gaudentia Mugosi
  50. Sitta, Margaret Simwanza
  51. Mahiza, Mwantumu Bakari
  52. Meghji, Zakia Hamdani
  53. Ngombale-Mwiru, Kingunge –
  54. Simba, Sophia Mattayo
  55. Mtemvu, Abbas Zuberi
  56. Msolla, Prof. Peter Mahamudu
  57. Kagasheki, Ambassador Hamis Suedi
  58. Katagira, Eustace Osler
  59. Mohamed, Salim Yussuf
  60. Chami, Dr. Cyril August
  61. Iddi, Ambassador Seif Ali
  62. Chiza, Christopher Kajoro
  63. Msambya, Manju Salum Omar
  64. David, Dr. David Mathayo
  65. Chikawe, Mathias Meinrad
  66. Wasira, Stephen Masatu
  67. Mussa, Omar Sheha
  68. Mkulo, Mustafa Haidi
  69. Lotto, Sameer Ismail
  70. Saddiq, Suleiman Ahmed
  71. Kombani, Celina Ompeshi
  72. Ghasia, Hawa Abdulrahman
  73. Masha, Lawrence Kego
  74. Kawambwa, Dr. Shukuru Jumanne
  75. Sumry, Abdallah Salum
  76. Nchimbi, Dr. Emmanuel John
  77. Shibuda, John Magale
  78. Salum, Salum Khamis
  79. Sitta, Samuel John
  80. Mzee, Omar Yussuf
  81. Cheyo, John Momose
  82. Mwang'onda, Thomas Apson
  83. Mohamed, Mohamed Aboud
  84. Sumari, Jeremiah Solomon
  85. Membe, Bernard Kamillius
  86. Diallo, Dr. Anthony Mwandu
  87. Mwangunga, Shamsa Selengia
  88. Ali, Ali Haji
  89. Suleiman, Ali Haroon
 
Attachments

Wadau wanaJF, leteni hoja, hawa wahishimiwa kazi yao ni kukomalia posho mbili mbili na kusahau kilichowapeleka mjengoni?
 
who cares?

Halafu wakishaongea ndio iweje?

kama wananchi wanaowawakilisha wameridhika nyie kinawauma nini?

Halfu dunia hii ya leo sio sifa kusifiwa kwa kuongea bali kwa kutekeleza yale ambayo Mbunge katumwa na wananchi kuwafanyia
 
]who cares?
Halafu wakishaongea ndio iweje?
kama wananchi wanaowawakilisha wameridhika nyie kinawauma nini?
Halfu dunia hii ya leo sio sifa kusifiwa kwa kuongea bali kwa kutekeleza yale ambayo Mbunge katumwa na wananchi kuwafanyia[/QUOTE]

Inamaana we hujui mbunge ana kazi gani bungeni
Haya yupo ambeye hajauliza swali la msingi, swali la nyongeza hata hajachangia lolote duh! unataka kusema hajatumwa na wananchi???????????????
 
who cares?
Halafu wakishaongea ndio iweje?
kama wananchi wanaowawakilisha wameridhika nyie kinawauma nini?
Halfu dunia hii ya leo sio sifa kusifiwa kwa kuongea bali kwa kutekeleza yale ambayo Mbunge katumwa na wananchi kuwafanyia[/QUOTE]

Who cares??
Eboo mbona kwenye vyombo vya habari wanaongea???
ni kutetea maslahi yao binafsi! Wajameen tuwe makin na wawakilishi wetu hawa ndio chanzo cha makundi.
faraja ya mwananchi yeyote mwenye akili ni kusikia anvyowakilishwa na kutetewa bungeni! kwani bunge ni siri??? nashukuru mbunge wa jimbo langu si miongoni!
 
Hii list itakuwa edited by Six mwenyewe ndio maana jina lake halipo kwenye main list huku la Naibu Spika likibaki. Wengi wa hawa ni Mawaziri au wakuu wa mikoa, wao wako ndani ya mihimili miwili kati ya mitatu kwa wakati mmoja, yaani ni legislature kama wabunge na wakati huo huo ni executive kama mawaziri, hivyo hawana sababu ya kujiuliza maswali, wao maswali yao ni majibu moja kwa
Moja.

. Wdng Spika
 
Moja[/QUOTE]

yawezekana lakini!!!!!!!!!!
Mbona Mh Waziri Wiliam Ngeleja ameuliza maswali???????????
 
Mie sometimes hukaaga nikajiulizaga maswali ya baadhi ya thread na faida kwa wananchi nisipate jibu. Ok assume wao ni wabunge mabubu so what!!!

Haujui action speaks louder than word?? sasa pengine jamaa ni mtendaji mzuri na sio msemaji mzuri mliuliza kwanini hajauliza maswali? Je ububu wao huwasaidia wananchi waliomchagua au hapana kwasababu kuna wabunge wengine ni kama waswahili wa pwani maneno mengi vitendo hamna je ipi sasa faida kuwa na maneno mengi vitendo hamna? au kuwa na vitendo vingi maneno machache????
 
Hivi kwani kuongea sana ndiyo maana yake unatoa point sana au?....na hao wanaouliza maswali bungeni wamewafanyia nini wananchi wao?au ni wanpiga longo longo ili mradi wajulikane wako bungeni?....Acheni hizo hao mabubu sasa ndiyo watendaji kazi wazuri sana.

I salute you mdondoaji umetoa point!...Hureeey!
 
Eboo mbona kwenye vyombo vya habari wanaongea???
ni kutetea maslahi yao binafsi! Wajameen tuwe makin na wawakilishi wetu hawa ndio chanzo cha makundi.
faraja ya mwananchi yeyote mwenye akili ni kusikia anvyowakilishwa na kutetewa bungeni! kwani bunge ni siri??? nashukuru mbunge wa jimbo langu si miongoni!

HUYU ANAYETAKA KILA ANAYEONGEA NDO AONEKANE NI MCHAPA KAZI ANA MATATIZO KATIKA AKILI YAKE. NATAKA NIKUAMBIE KWAMBA, KUKAA KIMYA HAINA MAANA HUTIMIZI WAJIBU WAKO, NA KUMBUKA DEBE TUPU HALIISHI KUTIKA.

UNAWEZA KUKAA KIMYA LAKINI SHUGHULI ZAKO ZINAKWENDA, HIVI UKISHAONGEA BUNGENI HALAFU WANANCHI WAKO HAWAONI UNALOLIFANYA KUHUSU JIMBO LAKO NDO WASEME WALIKUPELEKA BUNGENI UKAWE "MPAYUKAJI" KWA KILA LINALOTOKEA AU LINALOZUNGUMZWA?

KAONI KWENYE MAJIBO YA HAO UNAOWASEMA NI MABUBU BUNGENI HALAFU NENDA KWA WALE UNAOWAITA WASEMAJE.

KAMA HUJAFANYA UTAFITI USIPELEKE VIDOLE VYAKE KWENYE KOMPYUTA NA KUANDIKA UPUUZI KAMA HUO.
 
Labda tungeuliza ni wabunge wangapi wamepeleka miswada binafsi [ private motions] bungeni na imepitishwa kuwa sheria.Kusimama na kusema "mimi nashauri ....." kama wanavyofanyaga haina maana yoyote.
 
mkuu list yote mbona ni government tupu....!nani amuulize nani, wanaulilzana wakiwa wanakunywa kahawa jioni!
 
Mimi nahisi hawa wabunge mabubu bungeni wanamnukuu Newton kivitendo. Kwa kuwa wanafahamu Newton alikuwa genius na hakuwahi kuongea bengeni japo alikuwa mbunge ndio maana na hawa wanagombea u-genius kwa ukimya!!!
 
who cares?

Halafu wakishaongea ndio iweje?

kama wananchi wanaowawakilisha wameridhika nyie kinawauma nini?

Halfu dunia hii ya leo sio sifa kusifiwa kwa kuongea bali kwa kutekeleza yale ambayo Mbunge katumwa na wananchi kuwafanyia

Pasco said:
Hii list itakuwa edited by Six mwenyewe ndio maana jina lake halipo kwenye main list huku la Naibu Spika likibaki. Wengi wa hawa ni Mawaziri au wakuu wa mikoa, wao wako ndani ya mihimili miwili kati ya mitatu kwa wakati mmoja, yaani ni legislature kama wabunge na wakati huo huo ni executive kama mawaziri, hivyo hawana sababu ya kujiuliza maswali, wao maswali yao ni majibu moja kwa
Moja.

Mbona na la mkewe limo!? Read btn lines gentleman!

Mdondoaji said:
Haujui action speaks louder than word?? sasa pengine jamaa ni mtendaji mzuri na sio msemaji mzuri mliuliza kwanini hajauliza maswali? Je ububu wao huwasaidia wananchi waliomchagua au hapana kwasababu kuna wabunge wengine ni kama waswahili wa pwani maneno mengi vitendo hamna je ipi sasa faida kuwa na maneno mengi vitendo hamna? au kuwa na vitendo vingi maneno machache????

Mbunge siyo mtendaji, na akitenda hatakuwa mwakilishi wa wananchi. Kwani itakuwa ni rushwa.

Guys, Mngesoma majukumu/kazi za mbunge ktk Katiba ya Muungano msingepost hz weak excuses. Ni ngumu kutekeleza majukumu ya kikatiba ya mbunge kama hutoi michango bungeni. Shame!
 
Hivi tuseme wabunge wasiouliza maswali ya msingi wananchi wa majimbo yao hawana kero ambazo zinahitaji majibu au ufumbuzi toka Serikalini?
 
Pia tunaomba oroza ya wana JF ambao ni mabubu... 🙂 tehtehteh
 
Pia tunaomba oroza ya wana JF ambao ni mabubu... 🙂 tehtehteh

Absolute! teehee teeeheee haaahaaaa khaaaaaaa
vp ilipata orodha ya wana JF ambao ni mabubu??
maana kuna mijitu itakwambia nao wanafaa duh
ripo rijamaa moja rimeweza hata kusema hata yule ambaye hajauliza swali la msingi, hata la nyongeza
kubwa zaidi hata hajawahi kuchangia eti anafaaaa
mhhhh ringekua karibu yangu ningetaka ripimwe akili!
 
Back
Top Bottom