Orodha ya Wanawake kumi (10) mashujaa na viongozi bora kuwahi kutokea Tanzania

Abraham Lincolnn

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2018
Posts
2,754
Reaction score
4,975
10. Liti Kidanka.
download (25).jpeg

Mzaliwa wa Singida Tanganyika miaka ya 1860 na mwaka 1903 aliongoza majeshi ya jadi dhidi ya uvamizi wa Wajerumani hadi mwaka 1907 ambapo alikatwa kichwa na Wajerumani na mpaka leo hii fuvu la kichwa chake liko huko Ujerumani. Aliunganisha watu na alitumia nyuki kupambana na wakoloni. Ni shujaa, mzalendo na mtu aliyepinga uvamizi na dhuluma .

9. Mwami Theresa Ntare IV
download (26).jpeg

Alikuwa kiongozi wa kabila la Waha mkoani Kigoma, alikuwa mwanamke wa kwanza Mwanasheria baada ya uhuru, alisoma nchini Uingereza,alimsaidia Mwalimu Nyerere Mambo mengi sana wakati wa kudai uhuru, pia aliunganisha dola ya Burundi na Rwanda yaani Rwanda_Urundi territory na dola ya Buha. Alikuwa kielelezo cha ushujaa katika uongozi,aligoma kuolewa yaani kumfuata mwanaume kwa sababu za kulinda himaya ya Buha. Ingawa wanaume walimfuata kwao Buha na akawaoa.

8. Bi. Mwamtoro bint Chuma

7. Dr. Hellen Kijosimba

6. Fatma Amour .

Mwanamke shujaa kwenye mapinduzi ya Zanzibar, alikuwa mstari wa mbele. Wanawake wengi walikuwa nyuma kwenye mapinduzi ya Zanzibar isipokuwa yeye.

5. Lucy Lameck.
download (27).jpeg

Waziri wa kwanza mwanamke Tanganyika baada ya uhuru. LUCY LAMECK MWANAMKE WA KWANZA KUWA WAZIRI TANZANIA, BARABARA YA UJERUMANI KUPEWA JINA LA LUCY LAMECK.

Lucy Lameck anakumbukwa kama mwanamke aliyetoa mchango mkubwa katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika, akiungana na mwanamke mwingine maarufu Bibi Titi Mohamed.

Bi Lucy alikuwa ni mwanasiasa na mwanaharakati. Alipinga ukoloni wa Uingereza, alipinga ubaguzi na alikuwa mtetezi mkubwa wa wanawake.

Ushujaa huo umelifanya taifa la Ujerumani kubadili jina la mtaa wa Wissmann na kupewa jina la Mtanzania huyu.

Katika siasa za Tanganyika kabla na baada ya uhuru 1961, jina la Lucy Lameck liliingia katika kundi la wanasiasa maarufu kama Oscar Kambona, Lawi Sijaona, Nsilo Swai, Tewa na wengine walikuwa katika baraza la kwanza la mawaziri la Tanganyika na baadaye Tanzania.

Akiwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Wanawake-UWT, alijiamini kisiasa cha kukabiliana na wanasiasa wanaume katika kile kinachojulikana kama 'mfumo dume' wa wakati huo.

Harakati zake katika TANU

Tanganyika African National Union (TANU) kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hiki na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.

TANU chini ya waasisi wake wa wakati huo kiliendesha harakati za kudai uhuru wa taifa la Tanganyika dhidi ya Ukoloni wa Uingereza. Harakati hizo ndizo zilizoliibua jina la Lucy Lameck.

Baada ya kumaliza mafunzo ya uuguzi 1950, Lucy alikataa kufanya kazi katika mfumo wa matibabu wa kikoloni wa Uingereza na kuchagua kufanya kazi ya ukarani.

Katika kitabu cha 'Nyerere and Africa: End of an Era', mwandishi Godfrey Mwakikagile anaeleza, "tawi la TANU Moshi lilipofanya mkutano wake wa kwanza, mmoja wa wahudhuriaji alikuwa ni mwanamke kijana aliyeitwa Lucy Lameck".

Akitokea katika familia ya wakulima kwao Moshi, akiwa bado kijana hakuachwa tena nyuma katika mapambano ya kudai uhuru.

Lucy alikuwa mwanamke msomi ndani ya TANU. Kwa kushirikiana na wanawake wengine Halima Selengia, Amina Kinabo, Mama Bint Maalim waliifanya TANU kuwa na nguvu Moshi.

Katika matawi yote ya TANU Tanganyika, hakuna tawi lililopata nguvu kutoka kwa wanawake kama tawi la Moshi Mjini. Akina Mama hao walileta ngoma ya Msanja ambayo ilichangamsha chama.

Baadae Lucy kwa ufadhili alisoma katika Chuo cha Ruskin, huko Oxford, Uingereza na chuo kingine huko Michigan, Marekani kabla ya kurudi Tanzania na kuingia katika siasa moja kwa moja.

Bi Lucy alikuwa mpinzani wa wazi wazi wa ukoloni. Katika mahojiano yaliyochapishwa Febuari 1960 na jarida la Jet la nchini Marekani, aliulaumu ukoloni kwa umasikini uliokuwepo Tanganyika.

Katika mahojiano Lucy alieleza juu ya ukoloni wa Uingereza kuwa, "utaondoshwa na kurudishwa England hivi punde".

SIASA BAADA YA UHURU

Mwaka 1960 aliingia kwa mara ya kwanza katika Bunge la Tanganyika baada ya kuteuliwa na Waziri Mkuu wa wakati huo Mwalimu Julius Nyerere kuwa Mbunge, kabla ya kuchaguliwa na wananchi katika Bunge la Kitaifa la Tanzania mwaka 1965.

Mwaka 1962 aliandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Waziri, akishika nafasi ya waziri mdogo wa Shirika na Maendeleo ya Jamii 1965 hadi 1970. Kisha aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya kati ya 1970 na 1972.

Lucy Selina Lameck Somi alizaliwa mwaka 1934 na kuaga dunia Machi 1993. kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake ikiwemo uthubutu na alitetea watoto wa kike kupelekwa shule.

4. Gertrude Mongella
20250210_160953.jpg

Gertrude Ibengwe Mongella
( Makanza ; alizaliwa 13 Septemba 1945) ni mwanasiasa Mtanzania ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Bunge la Afrika na alikuwa rais wa Tume ya umoja wa Afrika kuanzia 2003 hadi 2008.Ni mengi makubwa mno aliyoyafanya kama kiongozi ambayo kwa utendaji wake mkubwa wenye kutukuka amekuwa mmoja kati ya tunu na viongozi bora kabisa kuwahi kutokea barani Afrika.

3. Asha-Rose Mtengeti Migiro
images - 2025-02-10T123319.333.jpeg

(aliyezaliwa 9 Julai 1956) ni mwanasiasa na mwanadiplomasia ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012. Aliteuliwa kuwa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu VVU/UKIMWI barani Afrika tarehe 13 Julai 2012

2.SharIffa bint Mzee
download (28).jpeg

Mama huyu alikuwa miongoni mwa wapigania uhuru na waanzilishi wa TANU, alikuwa miongoni mwa wanawake waliokuwa karibu sana na Mwl Nyerere na alishirikiana naye kwa kiasi kikubwa katika kupigania uhuru.

1.Bibi Titi Mohammed.

20250210_125254.jpg

Mwanamapinduzi, mpigania uhuru na mtunza fedha wa TANU, alitoa sehemu ya nyumba yake kuwa ofisi ya TANU, alizunguka nchi nzima kunadi chama na gari ya mume wake ilikuwa inatumiwa na Mwalimu Nyerere. Haitoshi kueleza mchango wa Bibi Titi Mohammed.
 
Attachments

  • 20250210_125254.jpg
    20250210_125254.jpg
    43.3 KB · Views: 2
10. Liti Kidanka.
View attachment 3231804

Mzaliwa wa Singida Tanganyika miaka ya 1860 na mwaka 1903 aliongoza majeshi ya jadi dhidi ya uvamizi wa Wajerumani hadi mwaka 1907 ambapo alikatwa kichwa na Wajerumani na mpaka leo hii fuvu la kichwa chake liko huko Ujerumani. Aliunganisha watu na alitumia nyuki kupambana na wakoloni. Ni shujaa, mzalendo na mtu aliyepinga uvamizi na dhuluma .

9. Mwami Theresa Ntare IV
View attachment 3231805

Alikuwa kiongozi wa kabila la Waha mkoani Kigoma, alikuwa mwanamke wa kwanza Mwanasheria baada ya uhuru, alisoma nchini Uingereza,alimsaidia Mwalimu Nyerere Mambo mengi sana wakati wa kudai uhuru, pia aliunganisha dola ya Burundi na Rwanda yaani Rwanda_Urundi territory na dola ya Buha. Alikuwa kielelezo cha ushujaa katika uongozi,aligoma kuolewa yaani kumfuata mwanaume kwa sababu za kulinda himaya ya Buha. Ingawa wanaume walimfuata kwao Buha na akawaoa.

8. Bi. Mwamtoro bint Chuma

7. Dr. Hellen Kijosimba

6. Fatma Amour .

Mwanamke shujaa kwenye mapinduzi ya Zanzibar, alikuwa mstari wa mbele. Wanawake wengi walikuwa nyuma kwenye mapinduzi ya Zanzibar isipokuwa yeye.

5. Lucy Lameck.
View attachment 3231845
Waziri wa kwanza mwanamke Tanganyika baada ya uhuru. LUCY LAMECK MWANAMKE WA KWANZA KUWA WAZIRI TANZANIA, BARABARA YA UJERUMANI KUPEWA JINA LA LUCY LAMECK.

Lucy Lameck anakumbukwa kama mwanamke aliyetoa mchango mkubwa katika harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika, akiungana na mwanamke mwingine maarufu Bibi Titi Mohamed.

Bi Lucy alikuwa ni mwanasiasa na mwanaharakati. Alipinga ukoloni wa Uingereza, alipinga ubaguzi na alikuwa mtetezi mkubwa wa wanawake.

Ushujaa huo umelifanya taifa la Ujerumani kubadili jina la mtaa wa Wissmann na kupewa jina la Mtanzania huyu.

Katika siasa za Tanganyika kabla na baada ya uhuru 1961, jina la Lucy Lameck liliingia katika kundi la wanasiasa maarufu kama Oscar Kambona, Lawi Sijaona, Nsilo Swai, Tewa na wengine walikuwa katika baraza la kwanza la mawaziri la Tanganyika na baadaye Tanzania.

Akiwa mmoja wa viongozi wa ngazi ya juu wa Umoja wa Wanawake-UWT, alijiamini kisiasa cha kukabiliana na wanasiasa wanaume katika kile kinachojulikana kama 'mfumo dume' wa wakati huo.

Harakati zake katika TANU

Tanganyika African National Union (TANU) kilikuwa chama kilichotawala Tanganyika na Tanzania hadi muungano wa chama hiki na Chama cha Afro-Shirazi cha Zanzibar na kuunda Chama cha Mapinduzi (CCM) mwaka 1977.

TANU chini ya waasisi wake wa wakati huo kiliendesha harakati za kudai uhuru wa taifa la Tanganyika dhidi ya Ukoloni wa Uingereza. Harakati hizo ndizo zilizoliibua jina la Lucy Lameck.

Baada ya kumaliza mafunzo ya uuguzi 1950, Lucy alikataa kufanya kazi katika mfumo wa matibabu wa kikoloni wa Uingereza na kuchagua kufanya kazi ya ukarani.

Katika kitabu cha 'Nyerere and Africa: End of an Era', mwandishi Godfrey Mwakikagile anaeleza, "tawi la TANU Moshi lilipofanya mkutano wake wa kwanza, mmoja wa wahudhuriaji alikuwa ni mwanamke kijana aliyeitwa Lucy Lameck".

Akitokea katika familia ya wakulima kwao Moshi, akiwa bado kijana hakuachwa tena nyuma katika mapambano ya kudai uhuru.

Lucy alikuwa mwanamke msomi ndani ya TANU. Kwa kushirikiana na wanawake wengine Halima Selengia, Amina Kinabo, Mama Bint Maalim waliifanya TANU kuwa na nguvu Moshi.

Katika matawi yote ya TANU Tanganyika, hakuna tawi lililopata nguvu kutoka kwa wanawake kama tawi la Moshi Mjini. Akina Mama hao walileta ngoma ya Msanja ambayo ilichangamsha chama.

Baadae Lucy kwa ufadhili alisoma katika Chuo cha Ruskin, huko Oxford, Uingereza na chuo kingine huko Michigan, Marekani kabla ya kurudi Tanzania na kuingia katika siasa moja kwa moja.

Bi Lucy alikuwa mpinzani wa wazi wazi wa ukoloni. Katika mahojiano yaliyochapishwa Febuari 1960 na jarida la Jet la nchini Marekani, aliulaumu ukoloni kwa umasikini uliokuwepo Tanganyika.

Katika mahojiano Lucy alieleza juu ya ukoloni wa Uingereza kuwa, "utaondoshwa na kurudishwa England hivi punde".

SIASA BAADA YA UHURU

Mwaka 1960 aliingia kwa mara ya kwanza katika Bunge la Tanganyika baada ya kuteuliwa na Waziri Mkuu wa wakati huo Mwalimu Julius Nyerere kuwa Mbunge, kabla ya kuchaguliwa na wananchi katika Bunge la Kitaifa la Tanzania mwaka 1965.

Mwaka 1962 aliandika historia ya kuwa mwanamke wa kwanza kuteuliwa kuwa Waziri, akishika nafasi ya waziri mdogo wa Shirika na Maendeleo ya Jamii 1965 hadi 1970. Kisha aliteuliwa kuwa Naibu Waziri wa Afya kati ya 1970 na 1972.

Lucy Selina Lameck Somi alizaliwa mwaka 1934 na kuaga dunia Machi 1993. kuna mengi ya kujifunza kutoka kwake ikiwemo uthubutu na alitetea watoto wa kike kupelekwa shule.

4. Gertrude Mongella
View attachment 3231993

Gertrude Ibengwe Mongella
( Makanza ; alizaliwa 13 Septemba 1945) ni mwanasiasa Mtanzania ambaye alikuwa rais wa kwanza wa Bunge la Afrika na alikuwa rais wa Tume ya umoja wa Afrika kuanzia 2003 hadi 2008.Ni mengi makubwa mno aliyoyafanya kama kiongozi ambayo kwa utendaji wake mkubwa wenye kutukuka amekuwa mmoja kati ya tunu na viongozi bora kabisa kuwahi kutokea barani Afrika.

3. Asha-Rose Mtengeti Migiro
View attachment 3231849

(aliyezaliwa 9 Julai 1956) ni mwanasiasa na mwanadiplomasia ambaye alikuwa Naibu Katibu Mkuu wa umoja wa mataifa kuanzia mwaka 2007 hadi 2012. Aliteuliwa kuwa Mjumbe Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu VVU/UKIMWI barani Afrika tarehe 13 Julai 2012

2.SharIffa bint Mzee
View attachment 3231858

Mama huyu alikuwa miongoni mwa wapigania uhuru na waanzilishi wa TANU, alikuwa miongoni mwa wanawake waliokuwa karibu sana na Mwl Nyerere na alishirikiana naye kwa kiasi kikubwa katika kupigania uhuru.

1.Bibi Titi Mohammed.

View attachment 3231989
Mwanamapinduzi, mpigania uhuru na mtunza fedha wa TANU, alitoa sehemu ya nyumba yake kuwa ofisi ya TANU, alizunguka nchi nzima kunadi chama na gari ya mume wake ilikuwa inatumiwa na Mwalimu Nyerere. Haitoshi kueleza mchango wa Bibi Titi Mohammed.
Mambo yale yale ya Kibanga Ampiga Mkoloni!
 
Juzi namuuliza Dkt. Gwajima D kwanini wameamua kuweka picha ya samia kwenye vazi watakalotumia kusherekea siku ya wanawake duniani...?

Akanipa jibu jepesi sana eti kwa vile sisi tumepiga hatua kubwa sana kwenye kumnyanyua mwanamke kisiasa hadi kufikia hatua ya kuwa na raisi mwanamke kitu ambacho nchi zingine wameshindwa...!! Hivyo basi eti samia ndio kielelezo cha mafanikio ya maazimio ya Beijing conference.

Ni jibu ambalo limekaa kichawa sana, hapa Tanzania kuna wanawake wengi sana mashujaa waliofanya makubwa na kuacha legacy kuliko hata huyo Samia mwenyewe, na pia vile vile siku ya wakawa inatakiwa iguse mafanikio ya mwanamke kwenye kila angle sio kwenye siasa tu....

Anyway hii nchi sio wazee, sio vijana, sio wanawake sio wanaume yaani kila binadamu ameamua kuwa chawa....
 
Umewaweka kwenye list hadi mafisadi waliotuharibia katiba mpya wakishirikiana na mafisadi Samwel Sita na Endrew Chenge
Yaani unamtaja Asha Rose Migiro wakati alishiriki kuteketeza zile bilioni 600+ za katiba mpya akiwa na mwenyekiti Samia Suluhu Hassan
 
Back
Top Bottom