Orodha ya wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya

Mkuu uko vizuri, hii game ya bongo unaonekana unaijua
waliozaliwa kati ya 1980 hadi 1995 walibahatika kushuhudia enzi ya dhahabu ya Bongo Flava, hasa kipindi cha 2000 hadi 2008 ambapo muziki ulikuwa umefika kileleni kwa ubora. Wakati huo muziki haukuwa wa kuburudisha tu, bali pia ulitoa elimu na ujumbe mzito kwa jamii. Kila msanii alikuwa na ladha yake ya kipekee, na maproducer wengi walikuwa wamesomea sound engineering Ulaya, jambo lililofanya kazi zitoke na ubora wa hali ya juu pamoja na ladha halisi ya Kitanzania.

Enzi hizo hakukuwa na smartphones wala internet labda uende internet café, Sehemu kubwa ya burudani ilikuwa ni muziki. Ilipofika jioni watu wanasubiri kwa hamu Top 10, na mida ya saa moja usiku wanamsubiri Sauda Mwilima kupitia Star TV. Pia kulikuwa na Top 10 ya wasanii wachache walioweza kutoa video, zikionyeshwa kupitia ITV 2, ambayo kwa sasa inajulikana kama East Africa TV. mkikutana mtaani, shuleni, n.k. muziki ulichukua nafasi kubwa kwenye mazungumzo.
 
Mkuu inaonekana kipindi ngoma inatoka ulikua na demu wako wa huko upareni (Gonja) ukawa unamuimbia sana 😀😀😀😀
Hata sikuwa na hizo mambo, ila hy ngoma ilinikaa sana kipindi hiko mpaka nikawa naiimba yote 😂
 
Ni kweli mkuu,

Nakumbuka miaka ile, home tulikua tuna record nyimbo kali za wasanii zinazopgwa redioni kwenye kanda,
Kukosekana kwa nternet wakati ule kulifanya radio na television kuwa kimbilio letu kubwa
Bongo fleva ya miaka ile nlikua naipenda sana
 
Mkuu unaweza ukataja ngoma ingine kali ya stopper ambayo tunaweza weka hapa zikakaa kwenye mzani mmoja
Zinaweza zisiwe kwenye mizania sawa coz kwenye Ngoma zake zote stopa hiyo ndio ngoma yake ya kumalizia show, wasanii wengi wako na Ngoma za namna hiyo.
 
Eleza pia wasanii hao WAKO wapi wanajishighulisha na nini
 
Huyu jamaa na ka sauti kake 😀
Ngoma zake zilzofanya pouwa ni

Nimpende nani na kuna ngoma moja kafanya na Juma nature
Hiyo nimpende nani ndio naijua Mimi😅😅... Kuna dogo nae alikua anatokea mwanza c sir madini nae alikua na Ngoma yake yakuitwa kifungo huru.
 
Yes ni kweli jamaa naye baada ya hii ngoma sijamskia tena
Ma dj na watangazaji wa kibongo wanabana sana.

Hawa ma dj na watangazaji wamekatisha ndoto za wasanii wengi sana.

Unakuta msanii anajichanga anaingia studio anarekodi ngoma kali.

Enzi hizo unakuta msanii anaishi pugu kajiungeni huko, au mbagala ndani ndani.

Labda mwingine katoka mkoani kafika dar kafikia kwa shangazi yake, hawezi hata kuomba nauli ana hela nusu ya kulipia studio tu.

Anaamka saa 10 alfajiri anaanza kutembea kwa mguu mpaka studio.

Studio ni mikocheni kwa master, bamaga kwa majani kinywele, au msasani mawingu studios.

Bongo records ilikua ni bamaga nyumbani kwao na majani

Unaambiwa ukifika Bongo records kwa majani, kwanza heshima iwe mbele kama mfuko wa shati.


Muulize afande sele pamoja na ustaa wake, aliwahi kupigwa makofi, kisa aliwasha bangi, pale studio uwani.

Ukifika unakaa nje ya geti,na sio nje ya geti uegemee ukuta wa studio nooo!!! Ni nje ya geti upande wa pili wa barabara

Akifungua geti, anakua ni kama mwalimu mkuu yupo asembo na nyie wasanii ndio wanafunzi mko upande wa pili wa road.

Akisimama pale nje ya geti anawaona wooote ule upande wa pili.

Ukiingia ndani hela yako unalipia kwa secretary, secretary mwenyewe kajala wa harmo, hacheki na wowote.

Msanii akifanikisha kurekodi process inakua ni hiyo hiyo kufuata ngoma yake studio.

Anaweka ngoma yake kwenye cd anapeleka redio, akifika redio kizungumkuti kinaanzia getini, mlinzi anataka umuungie ya vitumbua.

Ukishindwa kumshawishi vizuri, yawezekana cd yako ikaishia pale pale getini, simply anakwambia maelekezo yametolewa wasanii wakabidhi cd getini, na huwezi kumbishia.

Ukikivuka hicho kizingiti cha mlinzi, unaenda kukutana na secretary wa studio.

Huyu secretary siku hiyo itategemea na mood yake ipoje, unaweza ukampa cd, akaipokea halafu anatupia kwenye dust been na huwezi kumuuliza kitu.

Mtu wa mwisho hapo alikua ni dj au mtangazaji, ilikua ukimpa cd unamshikisha na vichenchi, anaweza akachukua hata namba yako ya simu.

Siku msanii upo zako harakati mara simu inapigwa ni dj, anakwambia leo ngoma yako itachezwa redioni kipindi fulani, kipindi chenyewe ni usiku na kweli unakuta unasifiwa hapo na mtangazaji husika kisha ngoma inagongwa lakini kwa sababu ni usiku mnene unakuta ngoma inasikilizwa na walinzi.

Hapo anakwambia uwe unanitumia vocha, ukituma vocha, ngoma ndio inachezwa, ila ukikausha na wao wanakausha
 
Yes, Na kwangu hadi leo Master J ndio Godfather wa hili game japo yeye hapendagi kabisa hizi debates, anaona zinampotezea muda tu haoni umuhimu wa kuitwa legend wala mambo ya heshima.

Bongo flava hapo zamani ilikuwa inaitwa "Muziki wa kufoka foka" kwasababu wasanii waasisi wa huu muziki wengi walikuwa wanarap, muziki ulionekana wa kihuni tu, mwanzo kabisa miaka ya 1980 mwishoni walikuwaga watoto wa kishua wanarap mistari yao kwa kiingereza ila kwa beats zilezile za wasanii wa Marekani, miaka ya 1990 wachache walijaribu kuimba kwa kiswahili kama kina Saleh Jabir na prodycers enzi hizo walikuwepo kina Bony Luv lakini huyu alikuwa na shughuli zake nyigine kama ku dj na pia alikuwa na shughuli zingine kwenye radio ya couds ilipofunguliwa na kusaga kwasababu walikuwa karibu sana, muziki huu bado ulikuwa hauna future, muziki ulikuwa haurusiwi kupigwa redioni.

Ndipo master J akathubutu kuingia kwenye uandaaji wa muziki kwa miguu yote miwili, baba yake alimtimua nyumbani, hakuweza kumwelewa kwasababu alimsomesha chuo Uingereza kwa pesa nyingi degree ya electronics na alikuwa na uwezo wa kumpachika Tanesco kwasababu alikuwa mkurugenzi ila Master alichagua kuandaa muziki ambao ulikuwa unaonekana wa kihuni, hauna future, wala pesa.

Kipindi anaanza ni yeye peke yake aliekuwa ana studio full time ya kuandaa muziki wa kizazi kipya, alikuwa anarekodi kwa kiasi kikubwa kwa kiswahili wasanii kama kina Sugu lakini pia alirekodi chache kwa kiingereza zilizokuwa hit mfano "Are You Down", iliyoimbwa na kundi la Deplowmatz mwaka 1997.

hapo baadae mziki ukaanza kuonekana angalau umepata direction, miaka ya 1999 hadi 2001 kukaongezeka producers, Tajiri mwenye radio flani alimleta na kumuajiri Mzungu Mikka Mwamba afanye kazi kwenye studio kwa mshahara, wakaja wengine kina P Funk, Enricco, n.k. hawa wote walisomea sound engineering.

Master J kazi aliyokuwa anaifanya mwanzoni sio kidogo, alipiga mzigo wa kufa mtu, kuandaa beats siku 3, kumix na kumaster siku 3, yeye mwenyewe, hapo baadae kidogo ndio akapata wasaidizi kina Ludigo kwenye hiphop, kina said kwenye upande wa nyimbo za gospel na bolingo, n.k. lakini bado aliendelea kutengeneza ngoma kibao tu.

Na hapo baadae miaka ya 2000s akaja kugundua kitu kingine kilichompa mkwanja mrefu kwa kazi ndogo tu, MATANGAZO, alijua kucheza na makampuni, tangazo moja tu lisilozidi hata dakika moja lilikuwa linaweza kumuingizia kipato kikubwa kuliko kuandaa album nzima ya muziki.

Mwaka 2008 aliachana rasmi na production, na kazi yake ya mwisho ilikuwa wimbo wa “Niite Basi” wa Joselin.
 
Alicom badae alitoa moyo ilisikika kimtindo.

Oten baada ya nicheki alikuja kutoa "mimi" alimpiga sana madogo afande sele humo ndani. Baadae alikuja kutoa "tuyasahau" ambayo alimshirikisha afande sele na suma lee. Ulikua wimbo rasmi wa kumaliza bifu lake na afande sele. Kuanzia hapo ndio akapotea kwenye game

Tng walikua na ngoma nyingine inaitwa "ling on it". Sikumbuki vzr ipi iliwahi kutoka kati ya hiyo na bongo.com lakin zote zilibamba.

Sema mkuu umetisha. Inaonekana umeanza kufatilia bongo fleva kitambo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…