Orodha ya wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya

Orodha ya wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya

Kuna wasanii hapo umewakosea sana mfano TNG Squad hawakuhit na ngoma Moja tu ya Bongo dot com Bali walikua na ngoma zingine mfano Ring on it ilivuma hata kuliko Bongo dot com...

O Ten alikua na mapini mengi tu mfano sifa kumi za demu, Mkuu wa mkoa na Akipendacho Binti...
Hii Ring on it ni kali kweli nlisahau kabisa, Asante kwa kukumbusha
 
Eleza pia wasanii hao WAKO wapi wanajishighulisha na nini
Mkuu labda wengine wana taarifa za hawa wasanii aje atueleze sahv wanaendelea vipi, ila naamini wengi sahv wako taabani
 
Yes, Na kwangu hadi leo Master J ndio Godfather wa hili game japo yeye hapendagi kabisa hizi debates, anaona zinampotezea muda tu haoni umuhimu wa kuitwa legend wala mambo ya heshima.

Bongo flava hapo zamani ilikuwa inaitwa "Muziki wa kufoka foka" kwasababu wasanii waasisi wa huu muziki wengi walikuwa wanarap, muziki ulionekana wa kihuni tu, mwanzo kabisa miaka ya 1980 mwishoni walikuwaga watoto wa kishua wanaimba kwa kiingereza kwa beats za wasanii wa Marekani, miaka ya 1990 wachache walijaribu kuimba kwa kiswahili kama kina Saleh Jabir na watayarishaji enzi hizo walikuwepo kina Bony Luv lakini huyu alikuwa na shughuli zake nyigine kama ku dj na pia alikuwa na shughuli zingine kwenye radio, muziki huu bado ulikuwa hauna future, muziki ulikuwa haurusiwi kupigwa redioni.

Ndipo master J akathubutu kuingia kwenye uandaaji wa muziki kwa miguu yote miwili, baba yake alimtimua nyumbani, hakuweza kumwelewa kwasababu alimsomesha chuo Uingereza kwa pesa nyingi degree ya electronics na alikuwa na uwezo wa kumpachika Tanesco kwasababu alikuwa mkurugenzi ila Master alichagua kuandaa muziki ambao ulikuwa unaonekana wa kihuni, hauna future, wala pesa.

Kipindi anaanza ni yeye peke yake aliekuwa ana studio full time ya kuandaa muziki wa kizazi kipya, alikuwa anarekodi kwa kiasi kikubwa kwa kiswahili wasanii kama kina Sugu.

hapo baadae mziki ukaanza kuonekana angalau umepata direction, miaka ya 1999 hadi 2001 kukaongezeka producers, Tajiri mwenye radio flani alimleta na kumuajiri Mzungu Mikka Mwamba afanye kazi kwenye studio kwa mshahara, wakaja wengine kina P Funk, Enricco, n.k. hawa wote walisomea sound engineering.

Master J kazi aliyokuwa anaifanya mwanzoni sio kidogo, alipiga mzigo wa kufa mtu, kuandaa beats siku 3, kumix na kumaster siku 3, yeye mwenyewe, hapo baadae kidogo ndio akapata wasaidizi kina Ludigo kwenye hiphop, kina said kwenye upande wa nyimbo za gospel na bolingo, n.k. lakini bado aliendelea kutengeneza ngoma kibao tu.

Na hapo baadae miaka ya 2000s akaja kugundua kitu kingine kilichompa mkwanja mrefu kwa kazi ndogo tu, MATANGAZO, alijua kucheza na makampuni, tangazo moja tu lisilozidi hata dakika moja lilikuwa linaweza kumuingizia kipato kikubwa kuliko kuandaa album nzima ya muziki.

Mwaka 2008 aliachana rasmi na production, na kazi yake ya mwisho ilikuwa wimbo wa “Niite Basi” wa Joselin.
Aiseh
 
Yes, Na kwangu hadi leo Master J ndio Godfather wa hili game japo yeye hapendagi kabisa hizi debates, anaona zinampotezea muda tu haoni umuhimu wa kuitwa legend wala mambo ya heshima.

Bongo flava hapo zamani ilikuwa inaitwa "Muziki wa kufoka foka" kwasababu wasanii waasisi wa huu muziki wengi walikuwa wanarap, muziki ulionekana wa kihuni tu, mwanzo kabisa miaka ya 1980 mwishoni walikuwaga watoto wa kishua wanarap mistari yao kwa kiingereza ila kwa beats zilezile za wasanii wa Marekani, miaka ya 1990 wachache walijaribu kuimba kwa kiswahili kama kina Saleh Jabir na prodycers enzi hizo walikuwepo kina Bony Luv lakini huyu alikuwa na shughuli zake nyigine kama ku dj na pia alikuwa na shughuli zingine kwenye radio ya couds ilipofunguliwa na kusaga kwasababu walikuwa karibu sana, muziki huu bado ulikuwa hauna future, muziki ulikuwa haurusiwi kupigwa redioni.

Ndipo master J akathubutu kuingia kwenye uandaaji wa muziki kwa miguu yote miwili, baba yake alimtimua nyumbani, hakuweza kumwelewa kwasababu alimsomesha chuo Uingereza kwa pesa nyingi degree ya electronics na alikuwa na uwezo wa kumpachika Tanesco kwasababu alikuwa mkurugenzi ila Master alichagua kuandaa muziki ambao ulikuwa unaonekana wa kihuni, hauna future, wala pesa.

Kipindi anaanza ni yeye peke yake aliekuwa ana studio full time ya kuandaa muziki wa kizazi kipya, alikuwa anarekodi kwa kiasi kikubwa kwa kiswahili wasanii kama kina Sugu lakini pia alirekodi chache kwa kiingereza zilizokuwa hit mfano "Are You Down", iliyoimbwa na kundi la Deplowmatz mwaka 1997.

hapo baadae mziki ukaanza kuonekana angalau umepata direction, miaka ya 1999 hadi 2001 kukaongezeka producers, Tajiri mwenye radio flani alimleta na kumuajiri Mzungu Mikka Mwamba afanye kazi kwenye studio kwa mshahara, wakaja wengine kina P Funk, Enricco, n.k. hawa wote walisomea sound engineering.

Master J kazi aliyokuwa anaifanya mwanzoni sio kidogo, alipiga mzigo wa kufa mtu, kuandaa beats siku 3, kumix na kumaster siku 3, yeye mwenyewe, hapo baadae kidogo ndio akapata wasaidizi kina Ludigo kwenye hiphop, kina said kwenye upande wa nyimbo za gospel na bolingo, n.k. lakini bado aliendelea kutengeneza ngoma kibao tu.

Na hapo baadae miaka ya 2000s akaja kugundua kitu kingine kilichompa mkwanja mrefu kwa kazi ndogo tu, MATANGAZO, alijua kucheza na makampuni, tangazo moja tu lisilozidi hata dakika moja lilikuwa linaweza kumuingizia kipato kikubwa kuliko kuandaa album nzima ya muziki.

Mwaka 2008 aliachana rasmi na production, na kazi yake ya mwisho ilikuwa wimbo wa “Niite Basi” wa Joselin.
Mkuu unahisi ni kwanini mpaka leo watu wengi wanaona P funk majani ndo Godfather kwa upande wa Producers?
 
Sijamuona Renee Lamira alitoa kibao chake cha Fitina baadae Ngoma ya kwetu (huu wimbo naupenda sana) akapotea jumlaaa,

Hafsah Kazinja alivyotoa Pressure kimyaaaaaa

EMan alivyomuimbia Farida wake akalala mbeleee,


Enika alilalamika Baridi kama hii hakusikika tena sijui aliganda?

Kuna huyu kijana Ibrah Tz zao la THT alivyootoa wimbo wake Nilipize ukaumiza sana masikio yetu kwenye ringtones za simu hajarudi tenaa naona aliamua kulima mapenzi yalimgaragaza,

Haka ka Farida na songi lake la Pesa, kalivyoipata na mziki kakautia kwenye dustbin
 
Mwanangu umejitahidi sana umetaja ngoma nyingi sana za wana walokuja na kupotea kwa ngoma moja, mmoja wa ulowasahau ni Toxy Star ft Alikiba Pretty Girl, DJ Yusuph Mbele kwa Mbele..ila kuna wana umewaonea walikaapo kwenye game kwa ngoma zingine kali tu. Mfano sajna alikaa na Mganga pia, huyo Mataluma iliishi na Kasindela. Dani msimamo pia alikua na ngoma inaitwa MIC ilikua kali pia.. Hao Offside Trick walifanya vizuri tena na ngoma ya kuitwa Bata waloifanya na mzee Yusuph, Amini alitoa ngoma na Linah, iliishi sana tuu pia alitoa ngoma ingine iliitwa Ni wewe, November au December pia ilifanya poa... Coyo alitoa ngoma na Nandy ilimpa jina vizuri sana kwenye game inaitwa Binadamu niishie hapo...
 
Sijamuona Renee Lamira alitoa kibao chake cha Fitina baadae Ngoma ya kwetu (huu wimbo naupenda sana) akapotea jumlaaa,

Hafsah Kazinja alivyotoa Pressure kimyaaaaaa

EMan alivyomuimbia Farida wake akalala mbeleee,


Enika alilalamika Baridi kama hii hakusikika tena sijui aliganda?

Kuna huyu kijana Ibrah Tz zao la THT alivyootoa wimbo wake Nilipize ukaumiza sana masikio yetu kwenye ringtones za simu hajarudi tenaa naona aliamua kulima mapenzi yalimgaragaza,

Haka ka Farida na songi lake la Pesa, kalivyoipata na mziki kakautia kwenye dustbin
Enika ana ngoma ingine changanya changanya nayo ni kali
 
Ila all in all zamani ni zamani wewe sikiliza beats za way back halafu sikiliza hii mi-beats ya siku hizi haieleweeki hakuna mpangilio wa vinanda, drums, keyboard, guitar, yaan ni palangu palangu tu ili mradi AI kafanya yake imeisha hio, kizazi cha GMO
 
Gigy money-Nampa papa

Gigy naye alibahatisha hii ngoma moja na mpaka leo hana ngoma ingine kali kama hii

Lody music - Kubali

Huyu bwana mdogo hii ngoma aliitendea haki sana, baada ya hapo kajitahidi kurudi lakini wapi

Kontawa ft Nay wa mitego- Champion

Baada ya champion,sijawahi kuskia ngoma ingine kali kutoka kwa huyu bwana mdogo, ngoma zote anazotoa ni average, sahv kinachomfanya aendele ku rotate ni content zake anazofanya instagram ila huku kwenye music simuoni kama ana safari ndefu

Dayoo - Mwaka wa kuforce

Baada ya mwaka wa kuforce dayoo hajaweza kutoa hit nyingine mpaka leo japo anapambania nafasi
Oya hizo ni ngoma za kuanzia 2018,2019,2020 hadi 2024 kuelekea juu ni za juzi tu hapo sio za miaka ya 2000 kwenda chini, kingine usichojua cha kuongezea ngoja nikuweke sawa kidogo au nikufumbue macho, hizo hit song sio zote ila kwa asilimia kubwa zinakua uwakilishi wao ila melody na mpangilio wa nyimbo unakua chini ya maandalizi ya mtu mwingine ambae anafanya arrangements za nyimbo husika, sasa baada ya nyimbo kutoka na kufanya vizuri anaepewa credits ni msanii alieimba anasahaulika alietunga wimbo na kufanya arrangements za hio nyimbo, nazungumzia behind the scenes
 
Sema kitambo msanii kutoboa lazima uwe na mashairi na flow ya kueleweka kizazi kilionekana cha wahuni lakini hizo nyimbo kwa wakati huu zinafaa hata kusikilizwa kwenye nyumba za ibaada
 
Hii siifaham ngoja niiskilize pengine labda naijua
Basi utakua ni mdogo wetu... ngoja nikupe mistari mitatu..

"Kila leo nafikiria, sanaaa, pengo gani limeacha historia, sanaaa.....


Hii nyimbo ilitoka nadhani 2003-2004 ilikua inagombaniwa na makundi mawili waswahili na wengine nimewasahau....

Ilikua kali sana mzeee
 
Oya hizo ni ngoma za kuanzia 2018,2019,2020 hadi 2024 kuelekea juu ni za juzi tu hapo sio za miaka ya 2000 kwenda chini, kingine usichojua cha kuongezea ngoja nikuweke sawa kidogo au nikufumbue macho, hizo hit song sio zote ila kwa asilimia kubwa zinakua uwakilishi wao ila melody na mpangilio wa nyimbo unakua chini ya maandalizi ya mtu mwingine ambae anafanya arrangements za nyimbo husika, sasa baada ya nyimbo kutoka na kufanya vizuri anaepewa credits ni msanii alieimba anasahaulika alietunga wimbo na kufanya arrangements za hio nyimbo, nazungumzia behind the scenes
KUna ngoma ilikua mwaka 1995 kwenye uchaguzi....

Ilitoka track moja inamdiss Mrema...

Tulikua tunaimba

Big ripopa na padili Mrema ana dhiki ametoka uwaziri anagombea urais...

Oya ni kitambo nilikua kachalii
 
Back
Top Bottom