Orodha ya wasanii waliotoa hit moja kali kisha wakapotea kimyakimya

Badae alitoa hit nyingine alimshirikisha afande sele na suma lee inaitwa tuyasahau
 
Nilikuwa nakapenda sn haka kaFatma kwa sauti yake tamu wakati huo nipo university but celebrities hawashikiki, nasikia kakapata mzungu kaharibu na kuachia kanasota kitaa tu mida hii

Sauti yake inapatikana tena kwenye eno mic ya ziggy d
Enhee! Aisee, eno mic umenikumbusha🙏..

Fatma alikuwa ana sauti nzuri sana... kwa production za miaka ile kutoa hio sauti alikuwa talented...

Kiukweli jinsi alivyo tamba miaka ile, ilikuwa ngumu sana kumuweka kwenye 18... alikuwa hashikiki..
 
Kuna sehemu anasema alikamatwa akapeleka selo. Wakati anaingia wafungwa wenzake wakawa wanamshangilia mwali mwali mwali
Nimekaa vibaya sana Dizzo,nilipokua police nilifikiri kazi ya upolice ni yangu pekeangu, na nikifa nitazikwa na magwanda yangu, krauni langu na pingu zangu, kumbe nilikua najidanganya najichanganya,, nimekamuakamua sana, hakuna cha maana nilichofanya zaidi ya ugimbi sana sana bia na komoni
 
Kuna wasanii hapo umewakosea sana mfano TNG Squad hawakuhit na ngoma Moja tu ya Bongo dot com Bali walikua na ngoma zingine mfano Ring on it ilivuma hata kuliko Bongo dot com...

O Ten alikua na mapini mengi tu mfano sifa kumi za demu, Mkuu wa mkoa na Akipendacho Binti...
 
Father G - Binti mlokole
 
Nyimbo moja ama Album moja? Mfano Tng album nzima ilikua Kali sio Bongo dot com pekee, Ring on it pia ilikua nzuri Sana.

Offside trick pia Wana nyimbo nyingi Sana usisahau hawa ndio wameimba BATA na Mzee Yusuf, Amada umelewa na bi kidude etc .

Sema list nzuri,
 
Wakongwe tunakumbuka mbali sana enzi zile ushindani wa mziki ulikuwa mkali sana kila mtu alikuwa na staili yake ya pekee hawaigani mziki ulinoga.
Kuna baadhi ya nyimbo ilikuwa nikizisikia nilikuwa naburudika na kucheka kwa pamoja maana zilitungwa kwa staili kama ya Komedi ila kwa kutumia akili nyingi.
Kwa mfano nyimbo ya kali P ilikuwa nikisikia ile mistari yake jinsi alivyoitunga na ile lafudhi aliyoitumia kama ya Kikerewe au Kijita hasa hasa pale aliposema,
"Mimi na mwenzangu tukaiba virungu vya polisi na kwenda kuuza kwa mama ntilie ili wafanye kuni wapikie chakula,ilikuwa ni kinyume cha sheria mimi na mwenzangu tukashikwa na kupelekwa jela,kule jela tukakutana na wale watu tuliowasingizia kesi zamani,wengine walikuwa Manyampara,mimi kwa vile nilikuwa bondia wakaniogopa wakaniachia,yule mwenzangu wakamng'ang'ania kisha wakawa wanashangilia,Mwala,Mwala,Mwala.
Ilikaa vibaya ile siku tuliyemkamata mchina anayecheza kareti,huha mastaa,mimi na mwenzangu tukala mashuti kisha tukatoka nduki"
Yaani nyimbo zao ilikuwa ukisikiliza unapata hisiq kama unaiona muvi kabisa.
 
Kama unamjua mtaje. Huyu msani aloimba ati, nimelewaa nimelewa, nimelewa sana nimelewa, nimekunywa pombe nimelewa,..... Na sauti nyingne ya kilevi anaitwa nani bandugu
 
Kama unamjua mtaje. Huyu msani aloimba ati, nimelewaa nimelewa, nimelewa sana nimelewa, nimekunywa pombe nimelewa,..... Na sauti nyingne ya kilevi anaitwa nani bandugu
Hii sijaweza kuijua
 
Jamaa waliutendea haki muziki
 
Ni kweli ila kwa mimi naona samaki ndo ili take over
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…