Hii Ring on it ni kali kweli nlisahau kabisa, Asante kwa kukumbushaKuna wasanii hapo umewakosea sana mfano TNG Squad hawakuhit na ngoma Moja tu ya Bongo dot com Bali walikua na ngoma zingine mfano Ring on it ilivuma hata kuliko Bongo dot com...
O Ten alikua na mapini mengi tu mfano sifa kumi za demu, Mkuu wa mkoa na Akipendacho Binti...
AisehYes, Na kwangu hadi leo Master J ndio Godfather wa hili game japo yeye hapendagi kabisa hizi debates, anaona zinampotezea muda tu haoni umuhimu wa kuitwa legend wala mambo ya heshima.
Bongo flava hapo zamani ilikuwa inaitwa "Muziki wa kufoka foka" kwasababu wasanii waasisi wa huu muziki wengi walikuwa wanarap, muziki ulionekana wa kihuni tu, mwanzo kabisa miaka ya 1980 mwishoni walikuwaga watoto wa kishua wanaimba kwa kiingereza kwa beats za wasanii wa Marekani, miaka ya 1990 wachache walijaribu kuimba kwa kiswahili kama kina Saleh Jabir na watayarishaji enzi hizo walikuwepo kina Bony Luv lakini huyu alikuwa na shughuli zake nyigine kama ku dj na pia alikuwa na shughuli zingine kwenye radio, muziki huu bado ulikuwa hauna future, muziki ulikuwa haurusiwi kupigwa redioni.
Ndipo master J akathubutu kuingia kwenye uandaaji wa muziki kwa miguu yote miwili, baba yake alimtimua nyumbani, hakuweza kumwelewa kwasababu alimsomesha chuo Uingereza kwa pesa nyingi degree ya electronics na alikuwa na uwezo wa kumpachika Tanesco kwasababu alikuwa mkurugenzi ila Master alichagua kuandaa muziki ambao ulikuwa unaonekana wa kihuni, hauna future, wala pesa.
Kipindi anaanza ni yeye peke yake aliekuwa ana studio full time ya kuandaa muziki wa kizazi kipya, alikuwa anarekodi kwa kiasi kikubwa kwa kiswahili wasanii kama kina Sugu.
hapo baadae mziki ukaanza kuonekana angalau umepata direction, miaka ya 1999 hadi 2001 kukaongezeka producers, Tajiri mwenye radio flani alimleta na kumuajiri Mzungu Mikka Mwamba afanye kazi kwenye studio kwa mshahara, wakaja wengine kina P Funk, Enricco, n.k. hawa wote walisomea sound engineering.
Master J kazi aliyokuwa anaifanya mwanzoni sio kidogo, alipiga mzigo wa kufa mtu, kuandaa beats siku 3, kumix na kumaster siku 3, yeye mwenyewe, hapo baadae kidogo ndio akapata wasaidizi kina Ludigo kwenye hiphop, kina said kwenye upande wa nyimbo za gospel na bolingo, n.k. lakini bado aliendelea kutengeneza ngoma kibao tu.
Na hapo baadae miaka ya 2000s akaja kugundua kitu kingine kilichompa mkwanja mrefu kwa kazi ndogo tu, MATANGAZO, alijua kucheza na makampuni, tangazo moja tu lisilozidi hata dakika moja lilikuwa linaweza kumuingizia kipato kikubwa kuliko kuandaa album nzima ya muziki.
Mwaka 2008 aliachana rasmi na production, na kazi yake ya mwisho ilikuwa wimbo wa “Niite Basi” wa Joselin.
Mkuu unahisi ni kwanini mpaka leo watu wengi wanaona P funk majani ndo Godfather kwa upande wa Producers?Yes, Na kwangu hadi leo Master J ndio Godfather wa hili game japo yeye hapendagi kabisa hizi debates, anaona zinampotezea muda tu haoni umuhimu wa kuitwa legend wala mambo ya heshima.
Bongo flava hapo zamani ilikuwa inaitwa "Muziki wa kufoka foka" kwasababu wasanii waasisi wa huu muziki wengi walikuwa wanarap, muziki ulionekana wa kihuni tu, mwanzo kabisa miaka ya 1980 mwishoni walikuwaga watoto wa kishua wanarap mistari yao kwa kiingereza ila kwa beats zilezile za wasanii wa Marekani, miaka ya 1990 wachache walijaribu kuimba kwa kiswahili kama kina Saleh Jabir na prodycers enzi hizo walikuwepo kina Bony Luv lakini huyu alikuwa na shughuli zake nyigine kama ku dj na pia alikuwa na shughuli zingine kwenye radio ya couds ilipofunguliwa na kusaga kwasababu walikuwa karibu sana, muziki huu bado ulikuwa hauna future, muziki ulikuwa haurusiwi kupigwa redioni.
Ndipo master J akathubutu kuingia kwenye uandaaji wa muziki kwa miguu yote miwili, baba yake alimtimua nyumbani, hakuweza kumwelewa kwasababu alimsomesha chuo Uingereza kwa pesa nyingi degree ya electronics na alikuwa na uwezo wa kumpachika Tanesco kwasababu alikuwa mkurugenzi ila Master alichagua kuandaa muziki ambao ulikuwa unaonekana wa kihuni, hauna future, wala pesa.
Kipindi anaanza ni yeye peke yake aliekuwa ana studio full time ya kuandaa muziki wa kizazi kipya, alikuwa anarekodi kwa kiasi kikubwa kwa kiswahili wasanii kama kina Sugu lakini pia alirekodi chache kwa kiingereza zilizokuwa hit mfano "Are You Down", iliyoimbwa na kundi la Deplowmatz mwaka 1997.
hapo baadae mziki ukaanza kuonekana angalau umepata direction, miaka ya 1999 hadi 2001 kukaongezeka producers, Tajiri mwenye radio flani alimleta na kumuajiri Mzungu Mikka Mwamba afanye kazi kwenye studio kwa mshahara, wakaja wengine kina P Funk, Enricco, n.k. hawa wote walisomea sound engineering.
Master J kazi aliyokuwa anaifanya mwanzoni sio kidogo, alipiga mzigo wa kufa mtu, kuandaa beats siku 3, kumix na kumaster siku 3, yeye mwenyewe, hapo baadae kidogo ndio akapata wasaidizi kina Ludigo kwenye hiphop, kina said kwenye upande wa nyimbo za gospel na bolingo, n.k. lakini bado aliendelea kutengeneza ngoma kibao tu.
Na hapo baadae miaka ya 2000s akaja kugundua kitu kingine kilichompa mkwanja mrefu kwa kazi ndogo tu, MATANGAZO, alijua kucheza na makampuni, tangazo moja tu lisilozidi hata dakika moja lilikuwa linaweza kumuingizia kipato kikubwa kuliko kuandaa album nzima ya muziki.
Mwaka 2008 aliachana rasmi na production, na kazi yake ya mwisho ilikuwa wimbo wa “Niite Basi” wa Joselin.
Ni Mkorea na Gangnam ni mji wa matajiri nchini KoreaUko mbele kuna huyu muhuni wa kutoka japan nafikiri, alikua na hit yake inaitwa gangnum style. Alikimbiza dunia nzima baada ya hapo akapotea mpaka leo hatujui yuko wapiView attachment 3549751
Enika ana ngoma ingine changanya changanya nayo ni kaliSijamuona Renee Lamira alitoa kibao chake cha Fitina baadae Ngoma ya kwetu (huu wimbo naupenda sana) akapotea jumlaaa,
Hafsah Kazinja alivyotoa Pressure kimyaaaaaa
EMan alivyomuimbia Farida wake akalala mbeleee,
Enika alilalamika Baridi kama hii hakusikika tena sijui aliganda?
Kuna huyu kijana Ibrah Tz zao la THT alivyootoa wimbo wake Nilipize ukaumiza sana masikio yetu kwenye ringtones za simu hajarudi tenaa naona aliamua kulima mapenzi yalimgaragaza,
Haka ka Farida na songi lake la Pesa, kalivyoipata na mziki kakautia kwenye dustbin
Alitoa nyingine Inaitwa Hangover alimshirikisha Snoop Dogg nayo namba zake sio habaUko mbele kuna huyu muhuni wa kutoka japan nafikiri, alikua na hit yake inaitwa gangnum style. Alikimbiza dunia nzima baada ya hapo akapotea mpaka leo hatujui yuko wapiView attachment 3549751
PNC ft. Mr. Blue - MbonaKama kuna wengine nimewasahau ongezea kwenye comment
Oya hizo ni ngoma za kuanzia 2018,2019,2020 hadi 2024 kuelekea juu ni za juzi tu hapo sio za miaka ya 2000 kwenda chini, kingine usichojua cha kuongezea ngoja nikuweke sawa kidogo au nikufumbue macho, hizo hit song sio zote ila kwa asilimia kubwa zinakua uwakilishi wao ila melody na mpangilio wa nyimbo unakua chini ya maandalizi ya mtu mwingine ambae anafanya arrangements za nyimbo husika, sasa baada ya nyimbo kutoka na kufanya vizuri anaepewa credits ni msanii alieimba anasahaulika alietunga wimbo na kufanya arrangements za hio nyimbo, nazungumzia behind the scenesGigy money-Nampa papa
Gigy naye alibahatisha hii ngoma moja na mpaka leo hana ngoma ingine kali kama hii
Lody music - Kubali
Huyu bwana mdogo hii ngoma aliitendea haki sana, baada ya hapo kajitahidi kurudi lakini wapi
Kontawa ft Nay wa mitego- Champion
Baada ya champion,sijawahi kuskia ngoma ingine kali kutoka kwa huyu bwana mdogo, ngoma zote anazotoa ni average, sahv kinachomfanya aendele ku rotate ni content zake anazofanya instagram ila huku kwenye music simuoni kama ana safari ndefu
Dayoo - Mwaka wa kuforce
Baada ya mwaka wa kuforce dayoo hajaweza kutoa hit nyingine mpaka leo japo anapambania nafasi
Basi utakua ni mdogo wetu... ngoja nikupe mistari mitatu..Hii siifaham ngoja niiskilize pengine labda naijua
KUna ngoma ilikua mwaka 1995 kwenye uchaguzi....Oya hizo ni ngoma za kuanzia 2018,2019,2020 hadi 2024 kuelekea juu ni za juzi tu hapo sio za miaka ya 2000 kwenda chini, kingine usichojua cha kuongezea ngoja nikuweke sawa kidogo au nikufumbue macho, hizo hit song sio zote ila kwa asilimia kubwa zinakua uwakilishi wao ila melody na mpangilio wa nyimbo unakua chini ya maandalizi ya mtu mwingine ambae anafanya arrangements za nyimbo husika, sasa baada ya nyimbo kutoka na kufanya vizuri anaepewa credits ni msanii alieimba anasahaulika alietunga wimbo na kufanya arrangements za hio nyimbo, nazungumzia behind the scenes