Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Orodha ya wasanii wenye majina makubwa lakini kiuhalisia hawana vipaji

Kipindi sugu anasikika redioni alikua ndo msanii pekee hvyo ilikua ni laIma askike coz hapakua na mpinzani , ndo maana aliishia kutamba 2000 baada ya vipaji halisi kuibuka , kina prof jay, ngwair, jay moe, FA na wengine kibao
Ukitaka kujua sugu hakua na takent ,tangu walianza kina prof jay sugu hakusikika tena , mpaka akaanza kulalamika kuwa anabaniwa ikafika kipindi wakaunda kundi la Ant virus na labda nkukumbushe tuu wasanii wote aliounda nao Ant virus hawana vipaji vya muziki
Punguza ujinga aisee! unafahamu Sugu aliondoka Bongo miaka ya 2000 kupiga Deiwaka ulaya huko!?
 
Kwa kuwa banana hana hit song so banana siyo msanii wa muziki hahaaaa....some people are dumb as hell...
So what about Jermaine Fox, RZA, Fifty, Wayne????
 
Kuna watu wengi hawajui wanachokizungumza. Na wengine hawajui muziki. Usanii una mambo mengi. Usanii wa muziki pia unaambo mengi kuna utunzi/uandishi, uimbaji, ualimu wa sauti, kurap, au kufanya mziki ktk style fulani au utamaduni fulani. Mfano Saida Karoli, wanne star, mpoto nk.

Hao na wengine wengi tunawaita wasanii wa muziki kwa kuwa muziki au wanachokifanya (uimbaji ni zao la sanaa).

Sasa kuwakubali au kutokuwakubali lazima uweke vigezo vyako au mkubaliane ktk vigezo ili tuelewane. Mfano kuna msanii Mimi naweza kumfahamu lakini mtoa mada au mchangiajiwingine asimfahamu. Mfano Naomisia msanii wa muziki lakini na uhakika wengi hawamfahamu. Sasa kama kigezo ni kufahamika na watu je huyo hatoweza kuwa msanii???

Kuna inshu ya kutoa hitkali. Hiti Kali kwa nani?
Juzi hapa kuna tunzo za hip-hop na kila mtu kazibeza. Maana yake waliozotoa waliona zinastahilo lakini wengi wameona hazistahili. Maana yake unaweza kumuona Ray-Van mkali mi nikakwambia Aslay ni mkali kwa Hawa vijana wabana pua. Mwingine akamkubali Harmonize kwa kuwa amepambana na system akatoboa yaani kipaji na upambani vinaweza kutumika kama kigezo, ila kwa nani?

Mi ntamkubali Suma mnazareti kwa Flow...we utamkubali Roma kwa ujumbe lakini mwingine atasema Roma hawezi badilika beat ni sawa tempo moja...

Kikubwa mkubaliane ktk vigezo. The means justifies the end...hivyo yaani...
UNaweza ukatusaidia vigezo mkuu, ila kamwe Sugu hawezi kuwa Tier 1.
Anarap kama Ngonjera......
Mfano, hii ni moja kati ya Verse zake, unaona jinsi anavyo babaika kutafuta mistari.
Nadhani ameimba na FA.

Msanii wa kwanza kuwa CEO/
Na kama ulikuwa hujui habari ndio hiyoo/
Na sikufoji vyeti kufikia hatua hiyo/
Mitaa inanikubali kwenye position hiyo/
 
So aliyeimba sumu ya Teja naye siyo msanii kwa kuwa hana hit song?
Au buibui aliyebaniwa Ruge akapigwa pini station zote au MB Dogg aliyepigwa pin na Fella naye hana kipaji
 
Kalapina,

Huyu jamaa mbali na kuwa na harakati nyingi akiwa pamoja na kundi lake la Kikosi cha mizinga .ukweli ni kwamba hana kipaji cha music. Alipata umaarufu coz ametoka kipindi wasanii ni wachache

Sugu

Huyu jamaa ana majina kibao kama Mr two, jongwe, too proud na sasa anajiita Taita licha ya kuwa na heshima kama moja ya waasisi wa music wa hiphop tanzania , ukweli ni kwamba hana kipaji cha music

Jaffarai

Huyu ni moja ya member wa wateule alitamba na wimbo wa niko bize .lakini hakuweza kudumu kwenye game kwa muda mrefu kutokana ukweli hana kipaji

Mchizi mox

Huyu pia ni member mwingine wa wateule ngoma zake zilizowahi kupata airtime ni mambo vp na chupa nyingine . lakini uwezo wake ni wa kawaida sana

Mike tee mnyalu

Huyu jamaa alipata airtime miaka ya zamani kwa ngoma zake lakini ukimskiliza ni wazi hana uwezo kabisa. Ni moja kati ya wasanii ambao huwa wanaandikiwa

Soggydog hunter

Huyu jamaa bora angebaki kwenye u presenter tuu huku kwenye music aliforce tuu hana uwezo kabisa ana ngoma nyingi ila iliyopenya ni kibanda cha simu pekee yake

Bou nako

Huyu alikua member wa N2N lakini tangu hakua na uwezo kabisa .nafkir wana walimbeba tuu kutokana na love .ila kwenye music jamaa hana kipaji

Fido vato

Huyu member wa vatokoko soldiers ni empy kabisa , analazimisha fan tuu ila ukweli anaujua kuwa hana uwezo wowote ule zaidi ya kujikuta gangstar

Kr mulah

Huyu ndio founder wa style ya kucheza Mapanga . ameanza sanaa muda mrefu sana lakini ukimskiliza utagundua jamaa hana uwezo wowote kwenye music kwa kifupi hana kipaji

Mh temba

Huyu ni member wa TMK wanaume family mwanzoni alibahatisha ngoma kama tatu zikaenda mjini, baadaye akaja kuungana na chege wakatoa hadi album..ila ukimfuatilia vizur jamaa hana
uwezo kabisa

Rich one

Huyu pia ni member wa TMK alitamba na ngoma moja aliyomshirikisha Juma nature inaitwa hatuna kitu.baada ya hapo hajawai kutoa hitsong tena, Jamaa anasifika kwa utapeli wa kuandaa show na wasanii fake huko mkoani afu anapiga hela

Dudu baya

Huyu jamaa aliotea ngoma kama tatu tuu ambazo zilimtambulisha vyema kwenye game .lakini alipata jina kwakua kipindi anatoka hapakua na upinzani mkali kama ilivyo sasa

Dark master

Huyu ndo muhasisi wa Chamber squard Nampa heshima kubwa sana kwa kuweza kuiweka dodoma kwenye ramani ya muziki , Lakini tukiongelea uwezo binafsi .jamaa anauwezo wa kawaida sana

John mjema,

The late John mjema alitamba na wimbo wa wachumba 30. Na ngoma zingine alizofanya kwenye kundi lao aliokua na kina the late steve 2kna buibui .lakini tukimzungumzia binafsi kimuziki jamaa hana kipaji cha muziki

Maujanja suppliers

Hawa jamaa nawakubali kwa harakati zao za street lakini kwenye music watupishe hawana vipaji .lakini wao wamekua wanalalamika wanabaniwa kitu ambacho sio ukweli

Kama unafuatilia music wa bongo fleva utakua unakubaliana na mimi hawa jamaa hawana talent za music kabisa
Temba na Mnyalu hapana umewaonea
 
UNaweza ukatusaidia vigezo mkuu, ila kamwe Sugu hawezi kuwa Tier 1.
Anarap kama Ngonjera......
Mfano, hii ni moja kati ya Verse zake, unaona jinsi anavyo babaika kutafuta mistari.
Nadhani ameimba na FA.

Msanii wa kwanza kuwa CEO/
Na kama ulikuwa hujui habari ndio hiyoo/
Na sikufoji vyeti kufikia hatua hiyo/
Mitaa inanikubali kwenye position hiyo/
I take him as a very good rapper I made it very clear. Mtu anayemuona hafai kuwa raper mzuri atoe vigezo. Mtu akituhumu aupe na vigezo.
Kwa mfano wako hapo juu maana yake ni kwamba unakubali kweli anaweza kurap ila uandishi wake hujaukubali kwa kuwa ameshindwa kubalance vina...yaani analazimisha vina. Kama hiko ndo kigezo chako weka wazi then wadau waanze kutumia kigezo Cha vina kum characterize Sugu. That is my point.
 
So hana kipaji cha ku rap?
Kama hana. Hana kama nani?
Yaani sugu hajui kulinganisha na nani? Wakati gani?
Tuna face Chache za Hiphop Bongo zilizofika juu Nyingi ziliishia kati. Kwa kutumia hizo hizo chache.
Prof jay >>>> Sugu
FA>>> Sugu
Fid>>>>Sugu
Nikki mbishi >>>> Sugu

Ni wengi, nikisema nitaje hapa nitataja karibu wasanii wote wa hiphop.

Japo ukiangalia wote hapo ni wadogo zake, lakini wmemzidi kila kitu kimuziki ukiondoa mafanikio binafsi.
Ameanza mapema anaweza jitetea technology ilikuwa ndogo bongo.

Lakini hata ukiskiliza album yake ya 2004 mbona bado uwezo ni mdogo? Amefanya kolabo na kina FA lakini wamemfunika kwenye ngoma zake mwenye.

Anastahili heshima kwa alichofanya, ni kati ya watu waliolay Njia lakini hii haiongezi chochote kwenye kipaji chake.
Staili yake ya kurap kama Ngonjera au mashairi ya "Malenga wapya" kulazimisha vina hakuna mtu atamsikiliza zama hizi.

Naskiliza album yake " Mimi" saiv, Alijitahidi kuongelea topics za msingi. Ila uwasilishaji doh hapana. Mashairi ya cheka cheka like.
 
Punguza ujinga aisee! unafahamu Sugu aliondoka Bongo miaka ya 2000 kupiga Deiwaka ulaya huko!?
Sasa sugu kwenda nje kupiga deiwaka inatuhusu nn sisi mashabiki ambaye tunajua wazi hana kipaji cha muziki..

Kadri unavozidi ku comment ndo unazidi kuonyesha upumbavu wako na ushamba .
 
Kwa kuwa banana hana hit song so banana siyo msanii wa muziki hahaaaa....some people are dumb as hell...
So what about Jermaine Fox, RZA, Fifty, Wayne????
Tatizo la kuvamia treni kwa mbele ....unaonyesha ulivo mpumbavu
 
Katika wote hao sugu, sugu hajui mziki, hajui kuimba, hana kipaji zaidi ya kujisifu tena hata kujisifia kwenyewe ktk nyimbo zake ni ujinga tu.

Kuna watu watafikiria labda na chuki nae ila ukweli ni kwamba hajui kabisa wala hajui mziki, mashabiki zake wengi ni kwasababu za kisiasa tu hakuna lingine
 
UNaweza ukatusaidia vigezo mkuu, ila kamwe Sugu hawezi kuwa Tier 1.
Anarap kama Ngonjera......
Mfano, hii ni moja kati ya Verse zake, unaona jinsi anavyo babaika kutafuta mistari.
Nadhani ameimba na FA.

Msanii wa kwanza kuwa CEO/
Na kama ulikuwa hujui habari ndio hiyoo/
Na sikufoji vyeti kufikia hatua hiyo/
Mitaa inanikubali kwenye position hiyo/
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] yan verse mbovu kichizi afu kuna majinga hapa yanasema jamaa ana talent
 
Mchizi Mox anasema kuwa Majani hakupenda vile jamaa anavyoimba kwa kukoroma, akamshauri abadili na kuimba kwa sauti ya kawaida, Mchizi Mox akakataa. Majani akafanikiwa kumbadilisha Jay Moe, huyu ndio akaanza kuimba hivi tulimvyomsikia katika nyimbo zake, ila nae awali alikuwa akitoa sauti ya kukoroma kama Mox.

Hata hivyo Majani hakuwahi kusema kuwa Mox hana kipaji, ila aliona kibiashara atazingua. Mtazamo aliokuwa nao Majani hata mimi nilikuwa nao wakati naanza kumsikia Jose Chameleon na ngoma yake Mama Mia. Niliona ni msanii mwenye sauti mbovu na hawezi kutoboa kumbe sikuwa sawa. Ilikuwa ni mtazamo wangu tu na sio kuwa jamaa hakua na kipaji, sasa the same goes kwa Mox et al
Aisee! Wewe game hii unaifahamu. Hakuna ulichokosea hapo. Ni kweli kabisa.
 
So aliyeimba sumu ya Teja naye siyo msanii kwa kuwa hana hit song?
Au buibui aliyebaniwa Ruge akapigwa pini station zote au MB Dogg aliyepigwa pin na Fella naye hana kipaji
We unazidi kuonyesha ujinga wako , yan msanii akishindwa kupata airtime basi kabaniwa na ruge
Haya sasa ruge ameshafariki , huyo buibui mwambie atoe kazi zake zipate airtime
 
Temba na Mnyalu hapana umewaonea
Hawa jamaa , waulize producers wanavyopata tabu nao studio kwenye kurecord ...hawana uwezo hata kuingiza voko ni shida
 
Back
Top Bottom