Orodha ya Watanzania waliosimama kupinga uwekezaji wa DP World; tuwataje historia iwahukumu au kuwapa maua yao

Orodha ya Watanzania waliosimama kupinga uwekezaji wa DP World; tuwataje historia iwahukumu au kuwapa maua yao

Nawiwa kuweka hapa kumbukumbu za wote waliotetea na kupinga kwa nguvu zote uuzwaji wa bandari. Majina yao yakiwa hapa yatasaidia waandishi wa vitabu na makala kwa siku zijazo kupata refference na kuona kama maono yao ya kupinga yalikuwa sahihi au hayakuwa sahihi. Naomba nianze kuwataja wachache.
1. Natambua nguvu aliyotumia kijana Martini Maranja kusambaza uvumi wa mkataba ambao baadaye ilikuja kubainika mkataba ni uliovuja ulikuwa mkataba halisi.
2. Shangaz Maria Sarungi amefanya kazi kubwa kuhabarisha na kufungua majadiliano ambayo yameweza kusaidia kutoa elimu kwa umma lakini pia kuwafungua macho walio wengi. Mijadala yake imerekodiwa hivyo sauti na maandishi vitakuwa vimehifadhiwa vyema kwa matumizi ya baadaye
3. Freeman Mbowe alitoa hotuba kali na yenye kuchambua hoja mbalimbali ikiwemo kuweka msingi wa kilichozua mjadala mkubwa cha bandari za Zanzibar vs bandari za Tanganyika. Hotuba hiyo ilizaa mjadala mkali ambao bado hakuna aliyeweza kuuzima.
4. Dr. Wilbroad pamoja na kuwa balozi lakini alipoona hali si shwari aliweka utaifa mbele; akaweka diplomasia pembeni na kusimama kwenye nguvu ya imani yake hadi kukamatwa na uhaini. Aidha hata baada ya kuwekwa mahabusu bado msimamo wake haukubadilika.
5. Wakili Mwabukusi aliyeshirikiana na wasomi baadhi kwenda kuupinga mradi huu mahakama nao wanastahili kuandikwa kwa njia nyingine.
6. Majaji wakiongozwa na Jaji Ndunguru historia itawakumbuka kwa kupinga vipengele vya mkataba kwa maandishi; hukumu yao inasaidia taifa kuandika kwa manufaa ya kizazi cha kesho kuhusu aina ya watawala na wasomi waliokuwemo karne ya 21.
7. Mhe. Jaji Warioba na Butiku wanawasilisha wazee wachache ambao walitoka adharani na kusema kwa hili hapana.
8. Karibu wa TEC ( Mzee wetu Kitima) ametimiza wajibu wake; ameweka kumbukumbu zote muhimu kwa niaba ya TEC pamoja na kutupa majina ya waliosimama kiroho kupinga mkataba huu.
9. Tundu Lisu sina haja hakumweleza sana kwa sababu hata nisipoeleza anajieleza kwa historia yake juu ya rasilimali za Taifa.
10. Godbless Lema kwenye hili yupo ila hayupo kwenye vibe kiviile..........

Tuendelee tuwaleta wanaoitwa majasiri leo kwa kumbukumbu za kesho: yawezekana wanaona vyema au wamepotoka hivyo tujipe muda wakuwatambua ili kesho tuwakumbushe au tuwakumbuke
Katika umoja wao unaweza tu kusema ni CHADEMA na washirika wake basi.
 
Naomba kuongeza wafuatao walipaswa kucheza namba za awali kabisa kwenye list
11. MDUDE
12. Prof. Anna Tibaijuka
13. Askofu Bagonza
14. Halima Mzee
15. Ester Matiku
16. Baadhi ya JF members
18. Getrude Mongela
19. Luaga Mpina japo kagusa hi game kwa mbaaliiiii akanywea
20. John Pambalu/Mnyika/Salm Mwalimu
21. Kuna yule mzee wa Mbeya alitupiga sana shule akipinga watanzania kuitwa wezi ( ntamwita mzee mwenye exposure yake)
22. Askofu Shoo kagusa huu mpira kwa kauli moja kubwa " wanaopinga wasiitwe wadini"
24. TEC kwa mara nyingine nawapa chapter nzima kwenye kitabu cha ujasusi wa bandari kutoka kwa Eriko Nyerere
25. Mzee Shivji
26. Profesa Assad alijitahidi ila..............mtieni ngumu arudi kwenye reli
 
Back
Top Bottom