Orville Lynn Majors: Je alikuwa ni Malaika wa kifo……!

Orville Lynn Majors: Je alikuwa ni Malaika wa kifo……!

msafi nakubaliana na wewe kuhusiana na nchi yetu kuwa na upungufu mkubwa wa wataalamu wa kitabibu, lakini sidhani kama ni vyema kukubali tu kirahisi watu waendelee kupoteza maisha kwa uzembe wa wataalamu hao wasiozingatia ukomo wa kiwango chao cha utaalamu.
Kila mtaalamu ana limitation zake kwa hiyo mtu kukurupuka na kufanya kazi ambayo hana utaalamu nayo eti kwa sababu tu alikuwa na nia nzuri ya kumtibu mgonjwa, hilo haliwezi kukubalika, siku hizi sayansi na teknolojia imekua sana kuna mitandao ya mawasiliano ambayo inaweza kurahisisha mawasiliano kati ya wataalamu wetu hawa na kubadilishana uzoefu.

Ni mpaka pale mtu anakapokuwa convicted kwa makosa ya aina hiyo ndipo wataalamu wachache wasiofuata maadili ya kazi zao watakaposhtuka na kujua kwamba ipo sheria na inafanya kazi......
lakini tukinyamaza kimya itakuwa ni business as usual.............

Kuna uzembe mwingi sana katika hospitali za binafsi, hapo ndipo kilipo kichaka cha wataalamu hawa feki wanaodhulumu roho za watanzania masikini....
watu wanaona kabisa kwamba hawana utaalamu wa kumtibu mgonjwa, lakini watamuweka hapo ili kuongeza mapato yao, na mgonjwa akionekana kuzidiwa kabisa, ndipo hutoa ruhusa apelekwe kwenye hospitali ya rufaa wakati huo ishakuwa too late, mgonjwa anafariki, tamaa ya fedha walio nayo wamiliki hawa wa hospitali binafsi inasababisha umauti wa mgonjwa huyu.

Ipo sheria na inafanya kazi, watanzania inabidi sasa tuamke hata kama itakuchukua miaka kumi, lakini lazima huyo daktari au mmiliki wa hospitali wa- face consequences

Hapo haswa ndipo panapotakiwa watu wafunguke na waweze kuset standard kwa kumpeleka mtabibu hata mmoja tu mahakamani. Tuache kubebana.
Na hivi vihospital nichinja chinja kwelikweli.

Natamani hii ungeitoa kwenye gazeti hasa yale yanayosomwa na watu makini ili tuweze kuibua hisia na kuungana kwa pamoja kuhakikisha matukio ya kutibu bila utaalam au kutibu kwa uzembe yanapungua au yanakoma kabisa.
 
Back
Top Bottom