Osama El Baz bingwa wa propaganda za maigizo

Osama El Baz bingwa wa propaganda za maigizo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
BINGWA WA PROPAGANDA OSAMA EL BAZ WA MISRI

Osama El Baz hujapata kukutana na mtu kama huyu.

Achilia mbali kuwa alikuwa ni Mmisri.

Wamisri wana sifa ya maneno matamu na ghilba.

Osama El Baz aliongeza kwa kuwa alikuwa mhitimu wa Harvard Law School na akafanyakazi kwa karibu sana na Anwar Sadat ndani ya ofisi ya Rais wa Misri.

Osama alikuwa bingwa wa vituko na propaganda akili yako haiwezi hata kufikiri nini aliweza kufanya tena kwa ufanisi wa hali ya juu sana.

Leo nikiangalia video mitandaoni ya wakuu wakijichanganya na wananchi wa kawaida nacheka hadi machozi yananitoka najiambia nani kawafunza hawa hizi staili za Osama El Baz?

Anwar Sadat ataonekana katika runinga anapita mahali kama Forodhani.

Ghafla anatokea mtu anasimamisha msafara wa rais.

Gari ya Rais inasimama na Sadat anatoka nje kusalimiana na yule mtu dakika mbili jamaa anamshika mkono rais anamkaribisha kwenye mshikaki meza ipo jirani hapo kiasi cha hatua tatu nne hivi.

Rais ataonyesha kusita lakini jamaa anamshikilia.

Haupiti muda watu waliokuwa jirani wamemzunguka Rais Anwar Sadat wanampa mkono wanasalimiana kwa bashasha.

Hapo watu wa TV weshafika wanapiga picha na wanamsikia jamaa anamwambia Sadat, ‘’Mtukufu Rais tafadhali karibu angalau upate kikombe cha kahawa dakika tatu tu tafadhali sana.’’

Sadat anakubali anakaa kwenye benchi.

Jamaa anapiga oda ya kahawa lakini anongeza na vitu vingine.

‘’Lete na mshkaki na mfungie Rais na ngisi na pizza ampelekee mama na watoto nyumbani.’’

Wapiga picha hapo wanapigana vikumbo.

Sadat uso mzima umejaa tabasamu.

Camera zinachukua kila kitu.

Dakika kumi hazifiki Sadat kanyanyuka kaingia ndani ya gari lake wasaidizi wake wamembebea zawadi za ngisi na pizza alizopewa na ‘’wananchi,’’ msafara unaondoka unayoyoma katikati ya mji wa Cairo.

Taarifa ya habari saa mbili usiku Sadat yuko kwenye channel zote wananchi wanamuona akijumuika na wananchi kwenye kijiwe cha kahawa na pizza.

Kazi ya Osama El Baz huyo.

Mtu huyu alikuwa bingwa wa mabingwa wa propaganda.

Unaweza ukasema kweli ile yote.

Wapi ndugu yangu yote ile kapanga Osama lakini si wengi wenye kutambua hilo hata wajanja walikuwa wanaingizwa mjini.
 
Vingine vya kuvijua kuhusu Osama El-Bazi
1. Alikuwa mshauri mkuu wa Rais Hosni Mubarak
2. Alikuwa Balozi wa Kwanza mdogo kutokea Misri
3. Alikuwa akifanya Kazi Buchani Marekani wakati anasomea PhD yake pale Harvard
4. Alikuwa Ni mmoja kati ya Watu muhimu kabisa katika kuleta mapatano ya Misri na Israeli Pamoja na Jordan.
 
Back
Top Bottom